Sema yupo vzr, usitake kulazimisha watu kuwa ni zaidi ya Aslay at kwa hizo nyimbo mbili tu. Aslay anajua mzk ni nini, na ana uzoefu, hana papara na mashairi yake yanagusa kila rika. Sikiliza Ndoa usiitie doa aliyoimba na Khadija Kopa, mashairi ya Aslay hayaendani kabisa na umri wake. Huyo Diamond mwenyewe nyimbo zake hazigusi sn jamii ukilinganisha na Aslay. Utunzi wa nyimbo km Libebe wa Beka ni BigG ambao hauna muda mrefu masikioni mwa wasikilizaji, Nyimbo nyingi za Aslay zitaweza kusikilizwa hata baada ya kizazi chetu. Beka ana vocal nzr lkn, mzk sio hicho tu, wenye vocal nzr ni wengi lkn wanafanya mzk kawaida mf. Barnaba, Bel9, Qchila, Rubby, Linex nk. Diamond hana vocal ya ajabu wala mashairi ya maana sn lkn angalia alikofika!. So Beka ni mwimbaji mzr km wengine, sio lazima umshindanishe na mwenzie ili kumuelezea. Mzungumzie yeye km yeye. Km unata kuwashindanisha basi fanya hivyo siku moja af uone nani atashinda. Huyo Beka alipotoa Libebe, alipokua anahojiwa na Radio alikuwa akimnanga Aslay, lkn Aslay alikaa kimya tu. Baada ya Aslay kuanza kutoa nyimbo moja baada ya nyingine, beka huyo huyo akaanza kumsifia Aslay kupitia Gazeti. Na Bado Aslay alisikika akisema Beka ni mtu wangu. So Usipende kulazimisha watu wafikiri unavofikiri wewe