Mashabiki wa Simba SC Kuweni Makini katika hili

lil wayne

JF-Expert Member
Apr 15, 2016
992
904
Salamu wanajamvi.

Ningependa kuchukua nafasi hii kuwashauri sana mashabiki wa Simba. Nahitaji pia wawe makini sana katika hili.

LigiKuu ya Tanzania Bara imefika kikomo, na Klabu ya Simba ipo kwenye Maandalizi ya msimu ujao wa ligi kuu, wakati huo huo timu ya Yanga SC ipo kwenye pilika za kusaka Ubingwa wa Shirikisho la barani Afrika.

Kinacho onekana sasa ni hali ya hatari sana kwa Mashabiki wa Simba kwa kutokuwa na umakini na ufuatiliaji wa mambo na masuala ya msingi sana yanayo endelea kwenye Klabu yao ya Simba SC ktk kipindi hiki cha maandalizi ya timu yao (Kwa ajili ya Msimu 2016/17)

Mashabiki na wapenzi wengi wa klabu ya Simba SC wako busy kufuatilia kinachoendelea kwa jirani.... Ukizingatia Jirani yao yupo busy kwenye majukumu ya Kimataifa.

Hali hii(Mashabiki wa Simba kutofuatilia timu yao) inasaidia sana Viongozi wa Klabu yao kufanya maamuzi ambayo si salama kwa klabu kwa ajili ya maandalizi ya Kikosi bora cha msimu Ujao. (Kila mtu anajua sifa za viongozi wa simba).

Mtakuja kushtuka muda ambao tunauita "Its too Late". Nakuanza kulaumu uongozi mzima kwa maandalizi hafifu.

Nina wasiwasi mkubwa sana kwamba Simba SC ya msimu ujao kuwa kama Hii ya msimu ulioisha.

Kuweni Makini watani zetu, sio kwamba hatupendi mfuatilie kilicho cha Yanga bali tunataka msimu Ujao msifuate mkumbo wa viongozi wenu wanao singizia watani zenu wanafanya vyema kutokana na kubebwa na Malinzi.

Epukeni sana sifa za Arsenal inapokuja suala la Mataji. Yanga hairudi nyuma tena, Huu ni mwendo Mdundo.

Nawasilisha...!
 
Shabiki ana maamuzi kwenye klabu wanaishabikia, unadhani wao wanaweza wataamua nini kwenye usajiri.
Na kwa kulitambua hilo ndio maana viongozi wanafanya wanavyotaka kama kumwacha Amis Tambwe na kuchukua magarasa .
 
Na kwa kulitambua hilo ndio maana viongozi wanafanya wanavyotaka kama kumwacha Amis Tambwe na kuchukua magarasa .
Hili ndilo ninalo maanisha.... Yaani utakuta Viongozi wanafanya wanayo yaona ni bora sana kwao na sio kwa manufaa ya klabu.

Na kwa jinsi mashabiki wa Simba SC walivyo mazuzu hayapati hata muda wa kujua kipi kinaendelea klabuni kwao... Wako busy mara ohh yabga hiv ohh Yanga vile...
 
Shabiki ana maamuzi kwenye klabu wanaishabikia, unadhani wao wanaweza wataamua nini kwenye usajiri.
Kwani klabu ya Simba na Yanga inamilikiwa na tajiri....?

Kwani haina wanachama...?

Wanachama wenyewe wako busy kushadadia ya mtani wake.... Ila yanayoendelea klabuni hawaya jui....
 
Na kwa kulitambua hilo ndio maana viongozi wanafanya wanavyotaka kama kumwacha Amis Tambwe na kuchukua magarasa .
Sikujui wewe ni mwanacha ama mshabiki huku ukandambilini, ila pia hujui maana ya mashabiki, ungejua hata tu kuchagua viongozi wa klabu wanaipenda hawaruhusiwi itakuwa itakua kuamua. Ni lini mshabiki wa yanga amempangia cha kufanya manji.
 
Jangwami tunaandamana lini kupinga magazeti yanayomchafua mtukufu kiongozi wetu? He he hee! Pesa bwana, watu wanachanachana magazeti ya mangi kisa gabacholi kamwaga mpunga
 
Kwani klabu ya Simba na Yanga inamilikiwa na tajiri....?

Kwani haina wanachama...?

Wanachama wenyewe wako busy kushadadia ya mtani wake.... Ila yanayoendelea klabuni hawaya jui....
Nadhani ungesoma viziri mada ukishaielwa ndipo ukomenti, mshabiki kazi yake kushabikia tu, mshabiki anaweza shabikia mpa vilabu vitatu tofauti, mfano wapo mashabiki Man, U ambao ni watanzania na wananchi nchi jirani ambao wazishabikia simba na yanga. Nadhani utakua umenielewa, hapa tujadili iliyoletwa, inawezekana alieleta mada alitaka kumaanisha hicho ambacho mnacho moyoni mwenu, ila amekosea kuiwasilisha.
 
Back
Top Bottom