Mashabiki wa chadema na mapinduzi ya kisasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mashabiki wa chadema na mapinduzi ya kisasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Profesa, Jul 17, 2012.

 1. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Mashabikiwa CHADEMA, kama mnakusudia kuchukua nchi hii 2015, basi muanze kuonyesha busara na hekina ya jinsi mnavyoweza kuwazidi wapinzani wenu wakuu kwa hoja na uafahamu wa mambo na mbinu za kisiasa. Bado hilo mnapaswa kulifanyia kazi kwa sababu wengi wanaongozwa na ushabiki na pale wanapoguswa pabaya huwa mnatumia hasira na matusi kama walivyo baadhi ya wajinga wa CCM.

  Kuweni mfano unajua kwanini? Msipojenga utamaduni wa kuelewa hoja za mpinzani wenu na kuzipangua, basi mtakuwa nawakati mgumu kuiendehsa nchi maana utamaduni huohuo ndio mtakaoutumia kundeshana wenyewe kwa wenyewe maana wakati huo nyinyi ndio labda mtakuwa viongozi.

  Viongozi wa CHADEMA, mna wajibu wa kuanzisha utamaduni utakaorithiwa na washabiki wenu ili watakaposhangilia ushindi wenu 2015, basi muwe na nafasi ya kushirikiana nao kutimiza ndoto zao na matumaini ya mabadiliko mnaypyakusudia. Msiwe kama baadhi ya viongozi wa CCM kuahidi kuwafanyia watu na kuwajengea matumaini hewa ambayo hamuwezi kuyatimiza. hamuiwezi kuyatimiza makubwa zaidi kwasababu changamoto za nchi hii hazitofautiani na nchi yeyote ile inayoendelea duniani. Na msisahau mtawaongoza wafuasi wa CHADEMA nna wafuasi wa CCM ambao wako vizuri ki-system.

  MSINASE KWENYE MBINU ZILIZO ZEEKA ZA KUWAAHIDI WATU MTWAFANYIA! WAAHIDINI WATU MTAWAONGOZA KUFANYA NCHI YAO IBADILIKE NA KUWA BORA KWA KUWA-FACILITATE NA KUWAWEKEA MAZINGIRA YATAKAYO "PUNGUZA" CHANGAMOTO ZAO KWA KIASI KIKUBWA (kwa kuwa hakuna nchi duniani iliyoko peponi). Mkiwaahidi watu mtawafanyia kama mnavyonasa kwenye siasa za kijinga zinazoendelea, hamtakuwa tofauti na wanasiasa walafi wenye kujipendelea wao, na kufanya short-cut ili tu wapate madaraka. Ukweli ni kuwa ni watu tu wao wenyewe ndio watakao leta mabadiliko wakisimamiwa na uongozi na uatawala bora (So utawala peke yake).

  Masikio yangu na macho yangu yananiambia kwamba CHADEMA wanakusudia kkulipiza kisasi kwa viongozi wa CCM iwapo watachukua madaraka, na hili liko kwenye mawazo ya wengi wa viongozi wa CCM, mmejipanga vipi kuwafanya wafuasi wenu waamini kuwa CCM nao ni raia wa nchi hii na wana haki saqwa na wafuasi wa CHADEMA? Maana shida kubwa ni kuwa siasa mnazoziendesha zinawapa umaarufu na wafuasi wengi ila je, hazitawarudi?

  Nimefurahishwa na hotuba ya Wizara ya Mambo ya Ndani ni mwanzo mzuri, wekeni jambo hili kwenye kampeni zenu maana mnahitaji support ya vyombo hivi vya usalama, na ninaona vyombo vya usalama ni kama vimepata mahala pa kusemea, nbaujua mfumo wetu ulivyo mgumu ndani ya majeshi hata kama mabo hayaendi sawa ni ngumu kuinuka.

  Ninawaambia haya kwakuwa nyinyi pia ni wa-Tanzania wenzangu, tutatofautiana kiitikadi humu ndani ila mwisho wa siku tukivuka mpaka, ni wamoja tunaongea lugha moja na utaifa wetu na msimamo wetu ni mmoja.

  KUWENI MFANO MZURI na SI MBAYA!

  MUNGU IBARIKI TANZANIA (Tanganyika na Zanzibar).
   
 2. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Profesa, wanaostahili hasa kupewa ujumbe huu ni wale walioko madarakani...kwamba wawatendee haki Watanzania kwa ujumla wao ili na wao waweze kutendewa haki siku watakapoyaachia hayo madaraka...hakuna mwenye hatimiliki ya kuitawala Tanzania milele. Lakini naelewa woga unaojaribu kuuelezea hapa, yanayowatafuna ni madhambi yenu mlioko madarakani na wasi wasi mlio nao kama chama kingine kitashinda uchaguzi wa mwaka 2015...the guilty are always afraid.
   
 3. mwitaz

  mwitaz JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2012
  Joined: Feb 19, 2012
  Messages: 314
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
 4. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,693
  Likes Received: 12,742
  Trophy Points: 280
  Asante kwa ushauri uliotoa!
   
 5. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Mag3 there is nothing wrong ku-confess the truth, ni kweli kwamba i am so guilty of my party and it is only because it has been trusted, but some of the crooks have spoiled it thinking that they can rule forever. Ila nakumbuka siku Mh. Jk alipokuwa anaingia madarakani, honi mabarabarani vifijo shangwe na nderemo... nbiliwahi kuliambia kundi moja la vijana shangwe hizi nazitilia mashaka, matumaini yako juu mno kulko ukweli wa mambo ndio ishara yake. na hawa wanaomshangilia matazamio yao yasipotimizwa watashabikia kundoka kwake kwa staili hii hiii.

  Leo hii sihitaji kutia neno... unayajua... ila basi, bado CHADEMA haiko salama na staili hii ya raia, matumaini yao yako juu mno kwa kukatishwa tamaa na kutokutimizwa kwa ahadi na matarajio yaliyotangazwa na CCM, sasa kama CHADEMA wasipokuwa makini, umaarufu wao unaweza kushuka kwa kasi ileile. Mimi nataka kujua kati yenu wooote mnaotoa hoja humu ndani, nani amesoma katiba na ilani ya CCM? Nani amesoma na Katiba na ilani ya CHADEMA kiundani, hili ninahofia linaweza kuwa tatizo, natoa changamoto msome kiundani, ili mkitoa hoja na kukosoa basi muwe na uelewa mzuri wa makundi haya makubwa zaidi kisiasa. Ninazo katiba za karibu vyama vyote na ilani za vyama vinavyoongoza kisasa. Nimesoma zote ili kuhakikisha siropoki, na najua vyama vingi tu vina mawazo mazuri tu.
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Jul 17, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Profesa,
  Tatizo la katiba na ilani ya CCM ni kwamba vimeshazikwa. Baadhi yetu tuliyasoma yote tukiwa middle school na secondary school. Rushwa ni mwiko, bado nakumbuka kabisa maneno hayo. Nitasema ukweli daima. Lakini ni nani ndani ya CCM kuanzia mwenyekiti hadi katibu kata anayefuata na kuzingatia hayo hivi leo? Ni kama vile CCM ina katiba mpya. Nitatumia nafasi yangu ya kazi kujitajirisha. Kila mwanya nitakaopata nitakwapua...hii ndiyo inaonekana kuwa ilani na katiba ya CCM hivi leo.
   
 7. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #7
  Jul 17, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Profesa,nakubaliana kabisa na wewe. Siasa za maji taka zina nia ya kuwaingiza watu kwenye matatizo. Bila kutumia akili, watakwama katikati ya njia. Fujo na ukosefu wa amani hautaiwezesha Chadema kukubalika katika jamii. Jamii inaweza kuwachukia tena sana tu maana hakuna anayetaka kuona ndugu au rafiki yake anaingia matatani sababu ya siasa
   
 8. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #8
  Jul 17, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Profesa, sifa kuu la chama chochote cha siasa ni namna itakavyosimamia mambo makuu mawili, la kwanza usalama wa mwananchi na la pili maendeleo yake. Chama chochote kinachofikia hatua ya kuonekana inazembea au kutelekeza mojawapo ya majukumu haya hakifai na kinapoteza kabisa sifa zote za kuwa chama tawala...dawa pekee ni kupumzishwa kwa kuondolewa madarakani. Kwa bahati mbaya toka tupate uhuru hali kama hii hatujawahi kuishuhudia, na hii imetoa nafasi ya dhana potofu kujengeka miongoni mwa baadhi ya jamii, hofu ya Tanzania bila CCM. Wako watu bila kutafakari kwa kina wamefika mbali na kudai eti afadhali zimwi likujualo wakiwa na maana kwamba heri CCM tunayoifahamu kuliko, kwa mfano, Chadema!

  Profesa, ukweli ni kwamba hali kama hii inatisha na bila kumung'unya maneno inasababishwa na ama ujinga au woga ambao kiini chake ni uroho wa kukosa. Kama isingekuwa hivyo hakuna namna Jakaya Kikwete angeweza kuchaguliwa tena kuwa Raisi mwaka 2010 baada ya kuonesha katika awamu yake ya kwanza uwezo finyu kama tulivyoshuhudia. Ni juhudi kubwa za Viongozi wa Chadema ambazo kidogo kidogo zimeanza kuwapa matumaini wananchi walio wengi huku ikiwapa mafisadi hofu ya mkate wao kutiwa mchanga. Matokeo ya hofu iliyowaingia watawala ni kutelekezwa kwa majukumu yao kwa wananchi na hivyo kuamua kuzinajisi hadi taasisi ambazo hazikutakiwa kutumika kisiasa kama polisi, Usalama wa Taifa na sasa mahakama.

  Profesa, ilipofika CCM hakuna, narudia hakuna namna yoyote itakayoweza kuitumia kujitakasa bali kuamua kukaa kando na kuruhusu watu wapya wenye mawazo mapya wakamate usukani. Ni kwa njia hii tutaweza kujenga ule utamaduni wa kuwajibika au kuwajibishwa...kwamba kama wananchi wanakupa ridhaa ya kuwaongoza, usipotimiza kama ulivyoahidi watakuondoa wamweke mwingine. Hivi sasa kiburi cha watawala kinatokana na hii dhana kuwa mtaji wao bado ni ule uleee!...hata wakivurunda namna gani wananchi bado wanaamini katika ujinga wa zimwi likujualo. Ndio maana kijana kama William Malecela, kwa mfano, anaweza kupata ujasiri wa kutoa kufuru kama dai la CCM kutawala kwa miaka hamsini!

  Profesa, Tanzania ingekuwa imejikwamua zamani sana ila tunako haka katabia ka mbuni ka kufikiri sisi tuko tofauti na binadamu wengine...kwamba yanayotokea kwingineko hayawezekani Tanzania. Kwa wafuasi wengi wa CCM, kila baada ya miaka mitano wanaridhika kuwasindikiza walafi hao hao kwa vifijo na nderemo hadi meza kuu halafu wao wanarudi kwenye umasikini wao na njaa yao kusubiri tena miaka mingine mitano. Ajabu ni kuwa pamoja na yote hayo wanaendelea kuikumbatia CCM hadi njaa inapokuwa haivumiliki...hapo utasikia lawama kwa wanaodaiwa eti wanakiharibu chama (Eti some crooks have spoiled it!) Wakitupiwa makombo kidogo haooo! wameshasahau wanaanza kuwanyooshea vidole Chadema and the cycle continues!
   
Loading...