SULEIMAN ABEID
JF-Expert Member
- Feb 26, 2013
- 390
- 385
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini na Naibu waziri wa Nishati na madini nchini, Stephen Masele amevamiwa na kundi la vibaka wakati akienda kupatiwa matibabu katika Zahanati ya BAKWATA iliyopo majengo Shinyanga ambapo amefafanua kuwa suala hilo halihusiana na mambo ya kisiasa.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Shinyanga, Masele alisema alivamiwa na kundi la vibaka zaidi ya 30 juzi saa 4.00 usiku alipokuwa akiteremka kutoka ndani ya gari lake kwa lengo la kuingia katika zahanati hiyo kwa ajili ya kupatiwa matibabu kutokana na kusumbuliwa na tatizo la vidonda vya koo.
Hata hivyo mbunge huyo amekanusha uvumi uliozagaa mjini hapa ukidai alivamiwa na kundi la wananchi waliomkuta akiendelea kufanya kampeni usiku kwa ajili ya wagombea wa chama chake (CCM) wanaogombea uchaguzi wa serikali za mitaa huku akigawa fedha kwa watu jambo lililowakera na hivyo kuamua kumvamia kwa lengo la kumzuia asiendelee kugawa fedha hizo.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na waandishi wa habari mjini Shinyanga jana ikiwemo habari zilizoandikwa kupitia mitandao ya kijamii walidai mbunge huyo alivamiwa na wananchi waliomkuta akiendelea kuwafanyia kampeni wagombea wa CCM kinyume cha sheria huku akigawa fedha kwa baadhi ya watu.
Akifafanua Masele alisema baada ya kuteremka kutoka ndani ya gari alilokuwa nalo Toyota Landcruiser lenye namba za usajili STL 2448 akiwa ameongozana na vijana wake wawili ambapo mmoja alikuwa ni Green guard wa UVCCM ghafla alivamiwa na kundi la vijana wanaohisiwa kuwa ni vibaka karibu 30 waliomlazimisha awapatie fedha alizokuwa nazo.
Masele alisema baada ya kutakiwa kusimama alilazimika kutii amri hiyo kwa tahadhari kubwa huku akijihama wasiweze kumdhuru na kwamba mmoja wao papo hapo alimpokonya simu aliyokuwa nayo kiganjani huku wengine wakimpekua katika mifuko ya suruali yake kwa lengo la kutafuta fedha kabla hawajagundua kwamba alikuwa ni yeye.
Kwa kweli nimeshitushwa na tukio hili, sikutegemea kabisa kwamba litanitokea, maana jana (juzi) nilikuwa natokea katika hoteli ya Vig Mark ambako tulikuwa tumemsindikiza mgeni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai na baada ya kupata chakula niliamua kurejea nyumbani,
Hata hivyo sikuwa najisikia vizuri katika koo langu, nilihisi nina vidonda vya koo niliamua nipitie katika Zahanati ya BAKWATA pale Majengo ili nipate dawa, lakini nilipofika katika zahanati hiyo wakati nateremka ghafla nilivamiwa na kundi la vibaka zaidi ya 30, walinizingira na kunilazimisha niwapitie fedha, alieleza Masele.
Hata hivyo alisema katika purukushani hiyo hakuna hata kijana mmoja aliyejaribu kumpiga na kwamba walipobaini ni yeye walisema wanachohitaji kutoka kwake ni fedha tu ili waweze kuishi na hivyo waliweza kuchukua fedha za Afrika ya kusini randi 400 alizokuwa nazo mfukoni takribani shilingi 50,000 za kitanzania.
Alisema kutokana na vurugu zilizokuwa katika eneo hilo baadhi ya wananchi waliokuwa jirani walisogea kwa lengo la kutoa msaada ambapo mmoja wa makada wa CCM alifyatua risasi mbili hewani kwa kutumia bastola yake ili kuwatisha vibaka hao waweze kukimbia hata hivyo hawakutishika wala kuondoka.
Kutokana na vurugu hiyo baadhi ya wananchi walisogea eneo la tukio, na mmoja wa wanachama wa CCM anayeishi jirani alijaribu kufyatua hewani risasi mbili kwa kutumia bastola yake, lakini vibaka wale hawakuondoka, mpaka polisi waliokuwa doria walipofika katika eneo hilo na kupiga risasi kadhaa hewani ndipo wakatawanyika, alieleza Masele.
Masele alisema binafsi hana tatizo na watu waliomvamia kwa vile yeye yuko salama isipokuwa anachokiomba kutoka kwa vijana hao wamrejeshee vitu vyake vingine ikiwemo kadi zake za muhimu ikiwemo za benki fedha wasirudishe kwa vile huenda lengo lao ilikuwa ni kupata fedha kwa ajili ya sikukuu na kwamba halihusishi tukio hilo na masuala ya kisiasa, anawachia polisi wachunguze.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mpaka hiyo jana mchana hakuna mtu ye yote aliyekuwa amekamatwa na ofisi yake inaendelea na uchunguzi wa kina ili kuweza kuwabaini na kuwakamata wahusika ambapo ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa watuhumiwa.
Ni kweli mheshimiwa mbunge na Naibu waziri wa Nishati na madini, Stephen Masele jana (juzi) alivamiwa na kundi la watu zaidi ya 30 waliojaribu kumshambulia na kuweza kumpora simu moja ya mkononi aina ya Sumsung S4 iliyokuwa na njia mbili zenye namba 0767 286 000 na 0658 286 600 na pochi iliyokuwa na vitambulisho vya benki na randi 400 za Afrika ya Kusini, alieleza.:sad: