Masele akanusha uvumi wa kushambuliwa na wananchi! Asema yuko salama

SULEIMAN ABEID

JF-Expert Member
Feb 26, 2013
390
385


KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini na Naibu waziri wa Nishati na madini nchini, Stephen Masele amevamiwa na kundi la vibaka wakati akienda kupatiwa matibabu katika Zahanati ya BAKWATA iliyopo majengo Shinyanga ambapo amefafanua kuwa suala hilo halihusiana na mambo ya kisiasa.


Akizungumza na waandishi wa habari mjini Shinyanga, Masele alisema alivamiwa na kundi la vibaka zaidi ya 30 juzi saa 4.00 usiku alipokuwa akiteremka kutoka ndani ya gari lake kwa lengo la kuingia katika zahanati hiyo kwa ajili ya kupatiwa matibabu kutokana na kusumbuliwa na tatizo la vidonda vya koo.


Hata hivyo mbunge huyo amekanusha uvumi uliozagaa mjini hapa ukidai alivamiwa na kundi la wananchi waliomkuta akiendelea kufanya kampeni usiku kwa ajili ya wagombea wa chama chake (CCM) wanaogombea uchaguzi wa serikali za mitaa huku akigawa fedha kwa watu jambo lililowakera na hivyo kuamua kumvamia kwa lengo la kumzuia asiendelee kugawa fedha hizo.


Baadhi ya wananchi waliozungumza na waandishi wa habari mjini Shinyanga jana ikiwemo habari zilizoandikwa kupitia mitandao ya kijamii walidai mbunge huyo alivamiwa na wananchi waliomkuta akiendelea kuwafanyia kampeni wagombea wa CCM kinyume cha sheria huku akigawa fedha kwa baadhi ya watu.


Akifafanua Masele alisema baada ya kuteremka kutoka ndani ya gari alilokuwa nalo Toyota Landcruiser lenye namba za usajili STL 2448 akiwa ameongozana na vijana wake wawili ambapo mmoja alikuwa ni Green guard wa UVCCM ghafla alivamiwa na kundi la vijana wanaohisiwa kuwa ni vibaka karibu 30 waliomlazimisha awapatie fedha alizokuwa nazo.

Masele alisema baada ya kutakiwa kusimama alilazimika kutii amri hiyo kwa tahadhari kubwa huku akijihama wasiweze kumdhuru na kwamba mmoja wao papo hapo alimpokonya simu aliyokuwa nayo kiganjani huku wengine wakimpekua katika mifuko ya suruali yake kwa lengo la kutafuta fedha kabla hawajagundua kwamba alikuwa ni yeye.


“Kwa kweli nimeshitushwa na tukio hili, sikutegemea kabisa kwamba litanitokea, maana jana (juzi) nilikuwa natokea katika hoteli ya Vig Mark ambako tulikuwa tumemsindikiza mgeni Naibu Katibu Mkuu wa CCM – Zanzibar, Vuai Ali Vuai na baada ya kupata chakula niliamua kurejea nyumbani,”

“Hata hivyo sikuwa najisikia vizuri katika koo langu, nilihisi nina vidonda vya koo niliamua nipitie katika Zahanati ya BAKWATA pale Majengo ili nipate dawa, lakini nilipofika katika zahanati hiyo wakati nateremka ghafla nilivamiwa na kundi la vibaka zaidi ya 30, walinizingira na kunilazimisha niwapitie fedha,” alieleza Masele.

Hata hivyo alisema katika purukushani hiyo hakuna hata kijana mmoja aliyejaribu kumpiga na kwamba walipobaini ni yeye walisema wanachohitaji kutoka kwake ni fedha tu ili waweze kuishi na hivyo waliweza kuchukua fedha za Afrika ya kusini randi 400 alizokuwa nazo mfukoni takribani shilingi 50,000 za kitanzania.

Alisema kutokana na vurugu zilizokuwa katika eneo hilo baadhi ya wananchi waliokuwa jirani walisogea kwa lengo la kutoa msaada ambapo mmoja wa makada wa CCM alifyatua risasi mbili hewani kwa kutumia bastola yake ili kuwatisha vibaka hao waweze kukimbia hata hivyo hawakutishika wala kuondoka.

“Kutokana na vurugu hiyo baadhi ya wananchi walisogea eneo la tukio, na mmoja wa wanachama wa CCM anayeishi jirani alijaribu kufyatua hewani risasi mbili kwa kutumia bastola yake, lakini vibaka wale hawakuondoka, mpaka polisi waliokuwa doria walipofika katika eneo hilo na kupiga risasi kadhaa hewani ndipo wakatawanyika,” alieleza Masele.

Masele alisema binafsi hana tatizo na watu waliomvamia kwa vile yeye yuko salama isipokuwa anachokiomba kutoka kwa vijana hao wamrejeshee vitu vyake vingine ikiwemo kadi zake za muhimu ikiwemo za benki fedha wasirudishe kwa vile huenda lengo lao ilikuwa ni kupata fedha kwa ajili ya sikukuu na kwamba halihusishi tukio hilo na masuala ya kisiasa, anawachia polisi wachunguze.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mpaka hiyo jana mchana hakuna mtu ye yote aliyekuwa amekamatwa na ofisi yake inaendelea na uchunguzi wa kina ili kuweza kuwabaini na kuwakamata wahusika ambapo ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa watuhumiwa.


“Ni kweli mheshimiwa mbunge na Naibu waziri wa Nishati na madini, Stephen Masele jana (juzi) alivamiwa na kundi la watu zaidi ya 30 waliojaribu kumshambulia na kuweza kumpora simu moja ya mkononi aina ya Sumsung S4 iliyokuwa na njia mbili zenye namba 0767 286 000 na 0658 286 600 na pochi iliyokuwa na vitambulisho vya benki na randi 400 za Afrika ya Kusini,” alieleza.:sad:




 

Attachments

  • DSC07982.JPG
    DSC07982.JPG
    43.4 KB · Views: 740
  • DSC07984.JPG
    DSC07984.JPG
    44.8 KB · Views: 682
1418564181826.jpg
Kwa hiyo hizi nyaraka sio zake, maana ametangaza rand 400 tu.?
 
Masele bana: acha uongo dogo.... vibaka kweli wapigiwe risasi 2 juu wasikimbie na wawe na confidence ya kusubiri mpaka polisi wafike..... kwi kwi kwiiiii.... uwongo wa magamba bana.... kajipange tena dogo uje na uzi mwingine huu hapana....
 
This is very bad

Hahaha Masele bana... Si useme ukweli tu Muheshimiwa???? WanaShinyanga tunajua.. Fuata sheria na taratibu za nchi... Na we unamamlaka gani kutembelea gari ya serikali, tena STL na zaid muda wa usiku... Bora ingekuwa gari ya Waziri..

Muheshimiwa usiwahadae watanzania wenzake na wanaShinyanga kwa ujumla.. Fanya maendeleo kwa vitendo utapendwa tu na utalindwa kwa nguvu zote.. Sio blaah blaah na ahadi za uongo.. Ndio maana vijana wa Shinyanga hawakupendi kabisa..
Mwakani kagombee Kigoma.
 
nimeamini nikweli kabisa huyu jamaa alishikwa akigawa rushwa. ukisoma maelezo yake yanajikang'anya. hayako consistence hata kidogo.
 
Ukiwa mwongo usiwe msahaulifu. Eti vibaka zaidi ya 30? labda atuhakikishie kuwa huko Shinyanga siku hizi kuna panya road a.k.a mbwa mwitu
 
Suleiman Abeid, acha hizo, kuna clip ya tukio lote, halafu unaandika hapa kutetea gamba, nakujua vizuri wewe, ni mwandishi unaendekeza njaa, haisaidiii kitu kukanusha tukio la kweli, Escrow we
 
Suleiman Abeid, acha hizo, kuna clip ya tukio lote, halafu unaandika hapa kutetea gamba, nakujua vizuri wewe, ni mwandishi unaendekeza njaa, haisaidiii kitu kukanusha tukio la kweli, Escrow we

Unaona sasa Mimi niliwaambia wangemvunjavunja ndo angeshika adabu! Sasa wananwacha mzima mpaka anapata nguvu ya kukanusha? Hovyo kabisa!! Shinyanga hatujafikia hapo pa kuwa na kundi la vibaka 30 wanaotembea kundi moja!! Eti mpaka majirani wanakuja vibaka hawajakimbia tu!? Uongoooooo!!
 
Tangu Tibaijuka kunyesha udhaifu katika kujitetea, siamini kama huyu dogo alikuwa hata na sababu ya kumlipa mleta mada aje ababwje humu JF. Hilo imehapita watuwalimsamehe tu wangemjeruhi tuone kama angesema ni vibaka! Hata elimu waliyonayo wanashindwa kuitumia kujieleza
 
Ningeshangaa zaidi kama angekaa kimya. Lakini kama ni kweli ajue anajidhalilisha
 
Naamin kwa maoni yako ya kijinga hata rpc pia ni mtu mwenye kuendekeza mishiko!!!! Wewe ni mpuuzi tu usiye elewa hata kilichoandikwa, hapa tumeandika maelezo ya pande zote mbili, kilichozungumzwa na wananchi, lakini pia maelezo ya masele!!! Yakiungwa mkono na rpc!!! Acha hizo za kudharau watu, ----- wewe!!!
 
Alipata wapi muda wa kuhesabu idadi ya hao anaowaita vibaka....??
 
Naamin kwa maoni yako ya kijinga hata rpc pia ni mtu mwenye kuendekeza mishiko!!!! Wewe ni mpuuzi tu usiye elewa hata kilichoandikwa, hapa tumeandika maelezo ya pande zote mbili, kilichozungumzwa na wananchi, lakini pia maelezo ya masele!!! Yakiungwa mkono na rpc!!! Acha hizo za kudharau watu, ----- wewe!!!

Uliyoyaandika na unaendelea kuyatetea basi wewe ni famba - jichunguze vizuri hata kama umetumwa kuja kudisimiss unazoziona ni allegation basi wewe na Masele uelewa wenu nautilia mashaka, ukipitia vizuri ulichokiandika inaonyesha waziwazi IQ yako itakuwa below 30! jichunguze
 
Back
Top Bottom