Masela wa Mbagala wajiunga na maandamano ya Marekani

Masela wa Mbagala wajiunga na maandamano ya Marekani

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,745
Reaction score
25,677
Pale Mbagala Kizuiani, mkabala na kituo cha daladala, Mangi ameweka TV nje ya kiduka chake na masela wapiga debe huikodolea macho muda wote wanaposubiri daladala. Burudani yao ilikuwa ni enzi ya ligi ya Uingereza.

Tangu Corona iingie wanaona kama TV inarusha maluweluwe tu! Mara mojamoja ninapopita pale huwa wanaomba niwatafsirie taarifa za BBC na Aljazeera.

Wiki yote hii TV ya Mangi inaonyesha maandamano ya wazungu. Masela kila wakigeuka, wakipindua, wakirudi wanakuta maandamano yanaendelea! Tayari wameshaelewa sababu ya maandamano, kuna mtu alishawahadithia kuwa askari wa kizungu alimkaba mswahili kwa goti mpaka akamuua. Wenyewe wanaiita “Roba ya goti”

Nilipofika Rais Trump alikuwa anaongea, masela wakaniuliza anasemaje, nikawaambia Rais anasema anasikitika sana. Halafu akaoneshwa Jacob Frey anaongea na waandishi, msela mmoja akauliza

“Na huyo nani?” Nikawaambia . Nikafafanua zaidi, “yaani kama Makonda wa mkoa tukio lilikotokea”.

“Ehe anasemaje?”, msela mwingine mwenye shauku akauliza. Nikawaambia anasikitika na anaomba na kusihi huyu askari ashtakiwe! Nikaona masela wanatazamana halafu wanatingisha vichwa, mimi nikadhani wanasikitika kutokana na ule unyama.

Halafu ikaoneshwa picha ya wanajeshi wamepiga magoti mbele ya waandamanaji. Msela wa mwanzo akauliza,
“Siyo wajeda wale?”.

Nikamwambia, “Naam, wanajeshi wale!”
“Wanasali?”, akaongeza.

Nikamwambia hapana, walikuwa wanaomba msamaha kwa waandamanaji kwa kitendo alichofanya mwenzao. Mara nikaona Masela wanasimama mmoja baada ya mwingine na kuondoka. Nikawauliza,
“Vipi, mbona mnaondoka na taarifa haijaisha?”

Msela mmoja akanijibu huku akiondoka, “Acha fix! Tumekushtukia unatulisha matango pori!”

Credit: James Gayo "Kingo"
 
Masela waliona kama ndoto MaAskari kumuomba radhi Mwananchi ikabidi waondoke zao. Lkn huo ndio ukweli
 
Wamezoea ya Tz, waandamanaji wanaahidiwa vilema na rais wao, mkuu wa mkoa na makamanda
 
Tayari wameshaelewa sababu ya maandamano, kuna mtu alishawahadithia kuwa askari wa kizungu alimkaba mswahili kwa goti mpaka akamuua. Wenyewe wanaiita “Roba ya goti”“Ehe anasemaje?”, msela mwingine mwenye shauku akauliza. Nikawaambia anasikitika na anaomba na kusihi huyu askari ashtakiwe! Nikaona masela wanatazamana halafu wanatingisha vichwa, mimi nikadhani wanasikitika kutokana na ule unyama.Msela mmoja akanijibu huku akiondoka, “Acha fix! Tumekushtukia unatulisha matango pori!”
Ahahaaaaaaaaa! Ndio Tanzania yetu hiyo kumbe ndio maana watu bado wanang'ang'ania ccm kwa miaka 60 sasa huwa nilikuwa nashindwa kuelewa kabisa sasa naelewa. Kama hii inatokea kwa vijana wa Dar sijui itakuwaje kwa vijana wa mikoani halafu vijijini! Tz bado sana.
 
Kiuhalisia polisi wa marekani kypiga goti kuomba msamaha ni usanii tu,,kwani wanajua mziki wa protester kuuzima bila kujipendekeza hauwezekaniki,
Jana tu pilidi huko UK walitoja mbio baada ya kuelemewa na protester
 
😀😆😀
Naona wamewazaaa wakona mh haiwezekani polisi ampigie magoti muandamanaji badala ya kumpiga na kumchakaza wakaona unawaingiza chaka
 
Kiuhalisia polisi wa marekani kypiga goti kuomba msamaha ni usanii tu,,kwani wanajua mziki wa protester kuuzima bila kujipendekeza hauwezekaniki,
Jana tu pilidi huko UK walitoja mbio baada ya kuelemewa na protester

I watched one polisi wa farasi aliangushwa na farasi baada ya farasi kuruka ghafla kwa protesters, basi paramedics wakaja fasta kumhudumia, UK hali jana ilikuwa mbaya haa.. 👇




 
Dogo ulipoteaga wapi tangu hulete thread kujua gharama ya kununua private jet kipindi kile tunaomboleza kifo cha Mengi. Rudisha avatar Picha yako ya mwanzo
 
Dogo ulipoteaga wapi tangu hulete thread kujua gharama ya kununua private jet kipindi kile tunaomboleza kifo cha Mengi. Rudisha avatar Picha yako ya mwanzo
Dah! mkuu lile dili linakwenda vema kabisa.
COVID-19 ndiyo imenitibulia kabisa mipango yangu.
Nilipanga mwezi wa 5 mwishoni ndege iwasili pale JNIA.
Ila kuna kiwanja changu binafsi cha Ismail Kanungila Airport kipo mji wa Ifakara kinamaliziwa kutengenezwa
IMG_20200608_193916_257.JPG


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah! mkuu lile dili linakwenda vema kabisa.
COVID-19 ndiyo imenitibulia kabisa mipango yangu.
Nilipanga mwezi wa 5 mwishoni ndege iwasili pale JNIA.
Ila kuna kiwanja changu binafsi cha Ismail Kanungila Airport kipo mji wa Ifakara kinamaliziwa kutengenezwa
View attachment 1472250

Sent using Jamii Forums mobile app
Dah aiseee hivi viporo vya kande iliyochacha mnavyoparamia na kubughia
 
Mkuu kituo cha haki za binadam cha huko hakijaishutum serikali ya usa kukiuka haki za binadam kama wanavofanyaga huku tz?
 
Back
Top Bottom