Masauni: Mpango kukijanisha nchi upo mbioni

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,743
Reaction score
2,601



Mwanza. Serikali ipo mbioni kuanzisha Mpango wa Mageuzi ya Kijani utakaolenga kukijanisha Tanzania na kusafisha Mazingira ambao programu zake zitasambaa nchi nzima ikiwa moja ya njia ya kuhifadhi na utunzaji wa Mazingira.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Hamad Yussuf Masauni ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza, Machi 13, 2026 ambapo amesisitiza kuwa kila mmoja anaowajibu wa kulinda mazingira na Serikali itawapongeza wale wanaozingatia sheria za Uhifadhi na Utunzaji wa Mazingira na pia kuwachukulia hatua kali wanaoharibu Mazingira.

Amesema Mpango huo umegusa takribani maeneo yote ili kuhakikisha Mazingira yanakuwa safi na salama hususani katika upandaji miti ili kuepuka majangwa na kuongeza bustani, usafishaji wa miji, ulinzi wa vyanzo vya maji, utakaochangia kwa kiasi kikubwa kupunguza maradhi.

Aidha, Waziri amewataka wawekezaji na watanzania wote kulinda Mazingira huku akisisitiza kuwa Serikali haitasita kuwachukulia hatua wale wote wanaosababisha uharibifu wa Mazingira kwa namna yoyote.

"Tunawajibu wa kulinda Mazingira Ili Mazingira yawe mazuri ni lazima sisi tuyalinde, na ili yawe mabaya ni lazima sisi tuyaharibu, Serikali inawajibu wa kuhakikisha watanzania wanaendelea kutunza Mazingira, na katika kuhakikisha hilo, Serikali haitasita kuwachulia hatua wale wote wanaoharibu Mazingira kwa namna Moja ama nyingine,” amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda amesema Ofisi yake inafanya juhudi kuhakikisha Mazingira yanalindwa na kutunzwa katika mkoa huo licha ya changamoto zinazoikabili Ofisi hiyo hasa katika udhibiti wa Kelele chafuzi za Maeneo ya kumbi za starehe.

Mhe. Mtanda ameiomba Ofisi ya Makamu wa Rais kuendelea na jitihada za kuondoa Gugumaji katika Ziwa Victoria ili kulinda samaki na ikolojia ya mazalia ya majini akielezea kuwa shughuli za uvuvi ni muhimili muhimu kwa wananchi wa Mkoa wa Mwanza.

Amesema asilimia 53 ya eneo la Mkoa wa Mwanza linazungukwa na maji hivyo linahitaji uangalizi wa kipekee katika uhifadhi wa mazingira hususan vyanzo vya maji na mwambao wa Ziwa Victoria ili kuhakikisha rasilimali za uvuvi zinaendelea kuwepo.

Katika hatua nyingine Mhe. Masauni pia aliweza kutembelea eneo lililoathirika na mafuriko hivi karibuni na kuharibu miundombinu mbalimbali ikiwemo barabara, nyumba na mali za wananchi.
 
Nataka kijiwe safi nikisajili, waje wavaa suti wapige moonshine, "vingereza viwe og from first sip" 🤣🤣
Mimi siku hizi napiga kwa machale sna nisije fia usingizini🤣
 
Mjomba nimecheka balaa karibu nipaliwe na msosi 🤣🤣

Unaogopa one way 🎫 🎟️ 🤣🤣
Nalewa kwa machale mno , na majukumu yamenikaba mkuu🤣 mda wa kuwa nduki mda wote naukosa
 
Nalewa kwa machale mno , na majukumu yamenikaba mkuu🤣 mda wa kuwa nduki mda wote naukosa
Kiasi mkuu...maana pombe ipo ila hela ikitoka mwenye baa harudishi 🤣🤣
Kama inabidi punguza kabisa uwe unakunywa kwa machale zaidi.

Maamuzi tu mbona utashinda hilo jaribu 🤣😊
 
Kiasi mkuu...maana pombe ipo ila hela ikitoka mwenye baa harudishi 🤣🤣
Kama inabidi punguza kabisa uwe unakunywa kwa machale zaidi.

Maamuzi tu mbona utashinda hilo jaribu 🤣😊
Mimi nanywea nyumbani tu bar ni ngumu kunikuta mkuu
 
Aah home tena kreti unalipapasa pembeni ya kochi ...unazipiga nyingi inaonekana.
Vita ngumu hiyo mzigo bill tayari 🤣
Pombe za kunywea ndani raha sana🤣 ulakula vitu huku samaki wako mkubwa anachemka
 
Pombe za kunywea ndani raha sana🤣 ulakula vitu huku samaki wako mkubwa anachemka
🤣🤣 Kwamba Jikoni mwenyewe, mhudumu mwenyewe na bill tayari...ikizidi unazima kwenye kochi saaafi no pressure utafikaje home 🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…