Masanduku ya kura yachomwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Masanduku ya kura yachomwa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ilumine, Nov 1, 2010.

 1. Ilumine

  Ilumine Senior Member

  #1
  Nov 1, 2010
  Joined: Dec 27, 2008
  Messages: 196
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shija Felician, Kahama (Gazeti la Mwananchi)

  WAKATI zoezi la kuhesabu kura za ubunge na urais likiendelea katika kata ya Bulige jimbo la Msalala Wilayani hapa,Wilayani Kahama, jumla ya Masanduku 18 na nyumba moja imechomwa moto.

  Sakata hilo lilikuja baada ya mvutano mkali wa kukusanya matokeo ya uchaguzi wa udiwani katika kata ya Bulige, ambapo Chama cha Mapinduzi (CCM) kilikuwa kikidai kuwa kimepata ushindi, huku Chadema wakidai hivyo.


  Hali hiyo ilisababisha kutokea kwa vitendo vya vurugu na uvunjifu wa amani katika eneo hilo.


  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Daudi Sias alisema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Novemba 1, 2010 baada ya Wananchi hao kuvamia sehemu yalipokuwa masanduku ya kupigia kura zilizohesabiwa.
   
 2. Avanti

  Avanti JF-Expert Member

  #2
  Nov 1, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 1,209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hiyo ni kweli kabisa. Mdogo wangu alikuwa msimamizi na alinipigia usiku wa saa 6 akiwa porini kwa kujaribu ya usalama. Ukitaka uhakika piga namba 0784860452 atakupa stori nzima
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Nov 1, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,395
  Likes Received: 414,707
  Trophy Points: 280


  Bila tume huru ya uchaguzi uhalali wa chaguzi zetu mashakani...........
   
Loading...