MASAHIHISHO: Report ya mchanga ina maswali mengi ya kujibu

Ujue madini mengine yanaoitwa Gold by product hayapo kwenye mkataba na hatuna cha kuwadai hapo labda hiyo Gold yenyewe na Copper.
Duu, hebu naomba unielimieshe kidogo, kama hayapo kwenye mkataba hiyo ni implication kuwa wanachukua bure? Na je hiyo quantity ya Gold na Copper waliyoripoti ndio hiyo hiyo imekutwa na kamati?
 
Kweli kbs,mi naona watu wanakurupuka tu, sina maslahi na accacia lkn pia bado naona kamati km haikuwa wazi kivile ili hata mama zetu kule vijijini waelewe.
Nilitegemea pia kuona kamati inasema nn khs mikataba. Na je according to mikataba, tumeibiwa kiasi gani? Then ndio zingekuja hizo hesabu za madini mengine waliyoyaona.

Na sikuona mapendekezo ya kamati kwenye mikataba,ina maana mikataba iko sawa? Je kusimamisha watu kazi bila marekebisho ya mikataba tutakuwa tumetatua tatizo?

Kwakweli naumia na mashimo tunayoachiwa ila pia niko na maswali kibao hapa hata natamani sijui aje Nani anifafanulie labda ntaelewa.


Kuna kamati/tume nyingine itakuwa na uchunguzi wao, na wataleta haya yote unayoyasema. kumbuka Raisi aliunda tume mbili, moja imeleta ripoti na nyingine bado inafanya kazi, na italeta ripoti yake. kwahiyo tuvute subira. hata hivyo Sisi ndiyo wenye mali, kwahiyo tunapaswa kutetea mali yetu; ACACIA naye atakuja na utetezi wake. lakini katika hili la madini nampa pongezi raisi hata kwa ile tu kuthubutu kugusa; kwasababu ilionekana ni untouchable na mikataba haiko wazi.
 
Kwani mruma alikuwa peke yake kwenye kamati?


Mkuu umesoma comment kwa umakini au na wewe umekurupuka kama kamati na rais wako???
Masahihisho yanatakiwa mengi tu kwenye ile report. Makontena 277 yawe na tani 7 za dhahabu...maana yake kila container lina kilo 25 za dhahabu...plus hayo madini mengine. Kilo 25 mi kama ounces 803....kwahiyo kwa makontena yote 277 kuna ounces 225,000. Huu ni uongo mtakatifu. Maana yake kama hii ni 30% tu ya production ya Buzwagi na Buly basi monthly production yao itakuwa around 750,000 ounces. Hatuna gold deposit za kiwango hicho kwenye mgodi wowote ule duniani.
Tulawaka ilidumu kwa miaka 9 chini ya Barick na wao hawakuwa na makinikia...dhahabu ilikuwa inakuwa extracted hapohapo mgodini....miaka 9 uote zilipatikana ounce kama milioni 1. Leo useme eti makontena yale ambao ni mzigo wa mwezi mmoja...tena 30% tu ya zalishaji yawe na karibu robo ya kilichopatikana Tulawaka kwa miaka 9? Tulawaka ndio mgodi pekee uliokuwa na grade ya juu kabisa ya dhahabu kuwahi kutokea katika migodi yote ya kanda ya ziwa.
Wekeni ripoti yote wazi....tuisome.




Mruma na wenzake ni majanga kwa fani zao...njaa ikishaingia kwenye ubongo huwa ni tabu sana.
 
Hakuna kitu kigumu kama kuongoza watu ambao wanaamini wako njema kielimu, kumbe wamesoma, wana vyeti, lakini hawakuelimika. Hatutaacha kuwa maskini mpaka tubadilidike na kuamua kuelimika kwanza baadae ndio vyeti
 
Kuna tume itakayokuja na taarifa kuhusu economic impact. Hiyo ndiyo itayoelezea vinzuri kiwango cha pesa zilizopotea. Hii ya jana kazi yake ilikuwa ni kufanya laboratory analysis ya kiwango cha madini kilichomo kwenye mchanga na kutafuta value yake. Tume inayofuata ndiyo itaangalia maslahi kwa mujibu wa mikataba iliyopo. Ndio maana hiyo tume wamejazwa wachumi. Wachumi hao ndio watakaoweza kuona hata impact ya kujenga smelter itasaidia kiasi gani katika uchumi wetu.



Suburini wachumi wawaambie mjenge smelter badala ya kuwatafuta watu wakiobobea kwenye hzo fani kama hamkuja jicheka wenyewe siku moja.


Eti wachumi???uchumi na minerals processing Wapi na Wapi....endeleeni kukurupuka kama mkivokurupuka kuingia mikataba ya kimangungo.na Barrick halafu moto wake mtauona siku si nyingi.
 
Wewe ni mtu usie makini... unaambiwa hao jamaa walikua hawatulipi chochote kwenye madini kama Uranium, barium, beryllium, sulphate, polonium, nickel, iron. Yani huo ni wizi mkubwa sana.

Tupo pa1 na rais... wewe mleta mada ni dalali ya hao vibaka.
Hayo madini mengine hayako kwenye mkataba.
 
Mimi nimesema hivyo. Kama una takwimu tofauti, sema ya kwako!
Kama hujui omba msaada. Katika masuala yenye rejea kama sheria hakuna cha 'mimi nina hiki na wewe sema cha kwako....' Sheria (Mining Act 2010) ni moja na pekee inayoratibu pamoja na mabo mengine, suala ya mirabaha. Katika sheria hiyo hakuna mrabaha wa 3%.
 
Tusubiri Tume ya wanasheria na wataalamu wengine ndipo tupate la kujadili kwa ni kujadili nusunusu hatuindei haki wala mwenye tume.
 
Mfumo wa uongozi aliouweka Mkuu wetu wa awamu hii ndio utakaoliingiza taifa hili pabaya. Mkuu amejitahid na amefanikiwa kuweka mfumo wa watu kuwaona wote wanao-challenge mawazo yake ni wezi, wapiga deal, mafisadi, wala rushwa au wamepewa chochote kile wamkosoe. Huu utaratibu ni mbaya na naona taratibu unaanza kulitafuna taifa.

Sasa hivi ukiongea tofauti na mawazo ya Rais au Serikali yako basi wewe utaonekana ni moja ya watu hao niliowataja hapo juu. Kuna vitu vingi tu sasa hivi Mh. Mkuu anachemka lkn watu (wataalam) wanapiga kimya kwa kuogopa kuonekana hawaitakii mema nchi hii au wamepewa hela (wamehongwa). Hii ni mbaya sana kwa taifa. Ku-challenge (kuhoji) maamuz au mawazo ya Rais (au Serikali) sio usaliti kwa nchi, ni njia nzuri ya kufanikisha mambo yaende, hatuwezi kufanana mawazo au mitazamo n aukiona mnafanana kwny kila jambo basi ujue anguko lenu limekaribia.

Kwenye taarifa ya jana kuna vitu vimepotoshwa/vimekuzwa lkn watu hawawezi kuviongelea kwa kuogopa km nilivyosema hapo juu. Mkulu anaposema kwa makontena yale 277 serikali ilkuwa inapoteza mapato kati ya Bil na Trilion ya dhahabu sio sahihi.

Hizi ni true value (thamani halisi) ya dhahabu iliyopo kwny makontena ambayo ikiuzwa, serikali kupitia TRA itachukua kodi/tozo/mrahaba wa 3% kwa sheria ya sasa hivi. Kwahiyo hiyo hela yote sio ya kwetu, sisi tuna % tu ya hela hiyo iliyotajwa. Tatizo lililopo ni kuwa kulingana na taarifa ya tume, thamani halisi ya dhahabu ni ndogo kuliko iliyotajwa hapo mwanzoni. Sasa hili tumelikuza na kuwaaminisha watanzania tumeibiwa kati ya Bil na Trilion wakati si kweli, chetu pale ni 3% ya true value (Bil ..... to Tril .....).

Ni kama kwenye biashara zingine tu za uzalishaji, utazalisha soda utauza zile soda, baada ya mauzo halisi ya soda zile kwa thamani sahihi ya soda, ile hela iliyopatikana (gross revenue) itapigwa % kadhaa kama kodi/tozo na mzalishaji atabaki na chake baada ya kodi/tozo (net revenue).

Sasa jana tumeaminishwa ile gross revenue baada ya kuuza zile dhahabu ni yetu yoteee. Hili tulikosea jana na kuleta tahaaruki kubwa ya kuonesha kuwa tunaibiwa sana. Ni kweli tunaibiwa lkn tuepuke kukuza mambo.
MAELEZO YAKO NI BAYANA KABISA. UKIFUATILIA TAARIFA YA KAMATI, UTABAINI KUWA MRABAHA WA WASTANI TULIOSTAHILI KULIPWA NI TZS BILIONI 33.788 NA MRABAHA AMBAO ULIKUWA DECLARED (PROVISIONAL) NA ACACIA NI TZS BILIONI 4.484. HIVYO TOFAUTI KWA KUINGIZA MADINI YOTE YALIYOTAJWA NA KAMATI NI TZS BILIONI 29.304. HII NI IWAPO UCHAMBUZI WA KIMAABARA WALIOUFANYA KAMATI NI SAHIHI (MAANA WANAWEZA KUWA WANAPOTOSHA PIA). UKITUMIA HESABU YA SIKU ZOTE KWA MADINI PAYABLE AMBAYO NI DHAHABU, FEDHA NA SHABA, MRABAHA STAHIKI KWA MUJIBU WA TAARIFA YA KAMATI NI TZS BILIONI 27.84. HIVYO TOFAUTI INAKUWA TZS BILIONI 23.356. KWA MWENDO HUU KAMA SIJAKOSEA HESABU, TUKUBALIANE KUWA TUMEKUWA TUKIPIGWA ILA SIO KWA KIWANGO KILE CHA TRILLIONS KWA KONTENA 277 KAMA WALIVYODAI KAMATI. TUWE MAKINI TUSIJE KUJENGA MATUMAINI MAKUBWA SANA KUWA KUMBE TUNAWEZA KUWA DONOR COUNTRY KWA ZAO HILO LA MADINI. NAUNGA MKONO JUHUDI ZA MHE. JPM NA NINADHANI ASIISHIE KWENYE MAKINIKIA PEKEE, TUDHIBITI TANZANITE NA ALMASI PIA. MWADUI WAMECHIMBA KWA MIAKA MINGI HATUPATI LOLOTE LA MAANA. MWAMKO HUU NI MZURI ILA TUSIJENGE MATUMAINI YA KUPITILIZA KAMA KAMATI WALIVYOPOSHA JANA KUWA TUNAIBIWA TRILLIONS.
 
Nampongeza Raisi wetu.Ila ile report aikusema chochote kuhusu mkataba hapo ndio nina wasiwasi kwani ilikuwa yuko busy na wateule wake kuwaadhibu wakati sio wao walio ingia nao mikataba.Mikataba hiyo ipo since 1998 na serekali hiyohiyo ya magufuli.Kitu amabacho nilitaka kusikia ni kuwa after that report,ACCACIA will pay tax amounting XX amount based on this findings.Au nisikie kuanzia sasa tunasimamisha uchimbaji wa madini kutokana na kipengele hichi kukiukwa.Kinyume na hivyo bado ni siasa tu za kupigiana makofi
 
Je, ripoti ilipitia mkataba kuona unasemaje kuhusu jambo hili na kumshauri Raisi namna bora za kujinasua kwenye hili au Raisi aliwapa kazi wanasheria wake ili waweze kumshauri namna bora ya kudeal na jambo hili ili mbeleni tusijepata madhara.
You are right mr.right!Hakuna ushauri wowote wa nini kifanyike kulingana na mkataba.
 
You have to be utterly stupid to agree to receiving 3% of the "profit" from people who can cook the books and declare no profit.

Kuna watu humu wananikumbusha uuzaji wa nchi kwa Wajerumani kwa kulipwa chumvi tu. Mkataba usiokuwa wa haki sio mkataba halali.
 
Swali langu ni very basic: Wakati akina Tundu Lissu wanaomba Mikataba ya madini iletwe kujadiliwa Bungeni wakati ule (Miaka ya 1998) nyie mlisemaje? Siyo nyie mliowaita wachochezi, na kwamba wanataka kuleta vita??? Sasa mmetoka kuzimu na kuwa wazalendo?? I DON'T TRUST YOU nor believe what you say.
 
  • Thanks
Reactions: Mdf
Back
Top Bottom