Masahihisho kuhusu Uganga na Uchawi

Masahihisho kuhusu Uganga na Uchawi

FUSO

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2010
Posts
36,474
Reaction score
45,048
Hoja kwamba Mganga anakupa dawa ya utajiri - yeye mwenyewe ni maskini wa kutupwa!! Kwa nini asijipe utajiri huo yeye mwenyewe, mkewe ama nduguze?

Jibu: Uganga ni wito wa kimizimu; Uganga unatumia mizimu na ile sadaka ya damu na hela unayotoa ni lazima iidhinishwe na mizimu ambayo ndiyo inayokutumia wewe kuganga watu.

Kama mganga ataenda kinyume na maagizo ya mizimu chamoto atakipata; anaweza kuona nyumba yake kituo cha police.

Uchawi na uganga una masharti yake ambayo mganga ama mchawi akiyakiuka tu anakwenda na maji.

Kuna watu huchoka kuroga ama kuagua lakini wanashindwa kuacha sababu ya kuogopa adhabu.

Haya mambo huwa ni maagano ya roho ambazo mababu na mababu wa ukoo husika wali sign - kwenda kimyume na maagano haya wengi hutumbukia kwenye laana; Kumbukeni mababu zetu hawakuwa na makanisa bali waliabudu Mizimu kama Miungu yao, maana Mizimu inapenda kuabudiwa ili ifurahi then iachie baraka kwako ama kwa ukoo wenu.

Kwa kumalizia tu ni kwamba UCHAWI upo; na uganga UPO utake usitake.

Ila kumbuka pia kuna makanjanja wameingilia fani kuibia watu, wanaharibu fani yetu ya utatibu wa kiasili.
 
Tukimaliza korosho tunaanza kuwatafuta nyie waganga na kuwapa kichapo,nyie sio mashoga hivyo nchi za ulaya na world bank hawata watetea.
Taarifa hizi wape na wenzio.
 
Haya mambo yawezekana yakawa ya kweli kwani mwaka 2007 kuna jamaa mmoja namfahamu tulikuwa nae mtaani aliteseka sana kwa kuumwa hadi akawa kichaa ambapo wazazi wake walikuwa wakienda shambani wanamfunga kamba kwenye mti ili asitoroke, siku moja akaja atoweka ghafla kutoka kaskazin hadi akaenda ziwa nyasa ambapo alirudi na kapu lililojaaa zana za kinyuklia isiyokuwa na sayansi kwa macho yetu, baada ya hapo aliaanza kupiga kazi na watu wengi inasadikika wamepata mikwanja ya kutosha kabisa kupitia kwake.....usiniulize maana mm sijawai kwenda kuaguliwa kwake lkn namfaham na huwa nikienda home tunapiga story kama mshkaji tu.....si unajua nabii hakubalike kwao....
 
Mkuu hicho ndicho nilitaka kukifikisha kwa jamii;

Kama mizimu ikikuamulia jambo na ukagoma lazima ikupe adhabu kali tena ya mwendelezo hadi utakapoitii.

Kuna baadhi ya koo wanapewa adhabu ya Nuksi wanakuwa hawafanikiwi katika mambo wanayoyafanya kwa mikono yao.

Na kuna baadhi ya waganga wengine wamekuwa forced kuifanya hiyo kazi. Wengine hawaitaki kabisa, ni kero ila hawana namna.

Kwa mfano, unaweza mponyesha tajiri lakini mizimu ikakuzuia kabisa kuchukua hela yake ikakwambia uchukue elfu tano tu. Sasa yule tajiri kapona anataka kukupa nyumba nzuri na gari haya pokea uone cha moto.

Hii ndiyo siri ya uganga, kila kitu unapangiwa.

Ukiona mganga anapokea chochote na mwenye tamaa ya kujitajirisha basi ujue uganga wake ni ule wa kununua si wa asili ya ukoo na huo huwa una expiry date...
 
Waganga pamoja na wachawi hawa wote ni washirikina hawatufai ktk jamii zetu
Kaka amini nakwambia njoo tufanye chimbuko la ukoo wako; sitatumia chochote kile cha dumba nop; mimi nitapiga ngoma tu na kuimba kuita mizimu ya kwenu then uone mizimu yako itakachokwambia; waweza kuja na mkeo au hata wanao washuhudie utakachoambiwa na mababu zako. Unaweza vheza ngoma balaa kama mizimu yako itafurahi ama kukunyoosha kama unajifanya jeuri.

Kila mtu ana shina lake; utake usitake as long as umezaliwa hapa duniani basi una mizimu ya kwenu.
 
Hata mimi mganga wangu alinipa masharti ya kutosafiri nje ya mipaka ya Afrika kwa kuwa mizimu imeona nitazuiwa niwekwe bond au watanidungua juu kwa ju
Mganga hakupi sharti; ila ni mizimu yako tu ndiyo hutoa amri - mganga yeye ni translator tu.

Kwa mfano inaweza kukuzuia wewe kusafiri then ukasikia chombo hicho kimepata ajali nk.
 
Mkuu hicho ndicho nilitaka kukifikisha kwa jamii;

Kama mizimu ikikuamulia jambo na ukagoma lazima ikupe adhabu kali tena ya mwendelezo hadi utakapoitii.

Kuna baadhi ya koo wanapewa adhabu ya Nuksi wanakuwa hawafanikiwi katika mambo wanayoyafanya kwa mikono yao.

Na kuna baadhi ya waganga wengine wamekuwa forced kuifanya hiyo kazi. Wengine hawaitaki kabisa, ni kero ila hawana namna.

Kwa mfano, unaweza mponyesha tajiri lakini mizimu ikakuzuia kabisa kuchukua hela yake ikakwambia uchukue elfu tano tu. Sasa yule tajiri kapona anataka kukupa nyumba nzuri na gari haya pokea uone cha moto.

Hii ndiyo siri ya uganga, kila kitu unapangiwa.

Ukiona mganga anapokea chochote na mwenye tamaa ya kujitajirisha basi ujue uganga wake ni ule wa kununua si wa asili ya ukoo na huo huwa una expire date...
Hayo mambo yapo " na watu wengi mnoo wanashiriki katika kuyafanya " lakini sasa mbele za macho ya watu wao ndio huwa wakwanza kujifanya kuyapinga kwaajili ya kulinda status zao ... lakini wanacho kisema ni tofauti na uhalisia ya kile wanacho kifanya " huwa wanakwenda sana kwa hao waganga ili waweze kurahisisha mambo yao ya utafutaji .. ila wakija katika jamii huwa wanajifanya kuwa hawajui lolote kuhusu hayo ..wengi Wanaogopa kusema ukweli kwa sababu wanaishi katika jamii ya watu wanaoabudu hizi dini zilizoletwa na meli pamoja na majahazi
 
Kaka amini nakwambia njoo tufanye chimbuko la ukoo wako; sitatumia chochote kile cha dumba nop; mimi nitapiga ngoma tu na kuimba kuita mizimu ya kwenu then uone mizimu yako itakachokwambia; waweza kuja na mkeo au hata wanao washuhudie utakachoambiwa na mababu zako. Unaweza vheza ngoma balaa kama mizimu yako itafurahi ama kukunyoosha kama unajifanya jeuri.

Kila mtu ana shina lake; utake usitake as long as umezaliwa hapa duniani basi una mizimu ya kwenu.
Nipe Mimi iyo ofa bro, nataka nijuwe mengi kuhusu ukoo wangu na mila zetu... Ivi kuna tofauti gani kati ya Mizimu na Majini?
 
Mkuu hicho ndicho nilitaka kukifikisha kwa jamii;

Kama mizimu ikikuamulia jambo na ukagoma lazima ikupe adhabu kali tena ya mwendelezo hadi utakapoitii.

Kuna baadhi ya koo wanapewa adhabu ya Nuksi wanakuwa hawafanikiwi katika mambo wanayoyafanya kwa mikono yao.

Na kuna baadhi ya waganga wengine wamekuwa forced kuifanya hiyo kazi. Wengine hawaitaki kabisa, ni kero ila hawana namna.

Kwa mfano, unaweza mponyesha tajiri lakini mizimu ikakuzuia kabisa kuchukua hela yake ikakwambia uchukue elfu tano tu. Sasa yule tajiri kapona anataka kukupa nyumba nzuri na gari haya pokea uone cha moto.

Hii ndiyo siri ya uganga, kila kitu unapangiwa.

Ukiona mganga anapokea chochote na mwenye tamaa ya kujitajirisha basi ujue uganga wake ni ule wa kununua si wa asili ya ukoo na huo huwa una expire date...
mkuu FUSO nakubaliana na ww, sisemi sana ila ukiona hujawahi pata shida yeyote ya kwenda kwa mganga basi ujue kwenye kizazi chenu kilibarikiwa tangia huko mwanzo lakin kama ni vizazi vya mababu zetu ambao walikuwa wanabudi mizimu na miungu mbalimbali lazima tu uwatafute wanga na unaweza kuzunguka kwenye makanisa yote ya maombezi bila kupata mafanikio hivyo muhimu hapa ni kujua historia ya vizazi vyenu then ndo mnaamua kuikataa hiyo mizimu au kuiendeleza.....amina....CC mtani wangu Mshana Jr....
 
Haya Mambo yapo kabisa na yanatesa sana watu au jamiii,na kama hajakupata au kukusumbuwa au hujawai kwenda kwa mganga basi shukuru mungu tu,

Ila kamwe na kato abadani usije ukamkebehi mtu anayekwenda kwa mganga au anayesumbuliwa na mambo hayo ,la umuhimu kumuombea mungu tu ,maana hujui kesho yako ikoje au nyuma yako kimejificha nini,

mimi nishashuhudia watu wengi wapinga haya mambo baadae walikuja angukia kwenye haya mambo na wakawa washirika wakubwa , kikubwa tujifunze kuweka akiba ya maneno maana kesho yetu hatuijui,

maana unaweza hangaika wewe ukamaliza dua zote au maombi kanisani na bado ikawa hujafanikiwa na ukaja kuta kuna mambo yamekukaba tu ya asili ,

Hii dunia kuna mengi yamejificha na ni mengi kuliko yaliyokuwa wazi na wengi tunaowaona nje wa safi ndani wachafu na wengi tunaowaona nje wa chafu ndani wasafi,

na ndomana mchawi huwezi mjua wala m'baya wako huwezi mjuwa
 
Haya mambo yawezekana yakawa ya kweli kwani mwaka 2007 kuna jamaa mmoja namfahamu tulikuwa nae mtaani aliteseka sana kwa kuumwa hadi akawa kichaa ambapo wazazi wake walikuwa wakienda shambani wanamfunga kamba kwenye mti ili asitoroke, siku moja akaja atoweka ghafla kutoka kaskazin hadi akaenda ziwa nyasa ambapo alirudi na kapu lililojaaa zana za kinyuklia isiyokuwa na sayansi kwa macho yetu, baada ya hapo aliaanza kupiga kazi na watu wengi inasadikika wamepata mikwanja ya kutosha kabisa kupitia kwake.....usiniulize maana mm sijawai kwenda kuaguliwa kwake lkn namfaham na huwa nikienda home tunapiga story kama mshkaji tu.....si unajua nabii hakubalike kwao....
Mkuu namuhitaji mkuu
 
Nipe Mimi iyo ofa bro, nataka nijuwe mengi kuhusu ukoo wangu na mila zetu... Ivi kuna tofauti gani kati ya Mizimu na Majini?
Mizimu ni roho za ukoo wenu; Roho za mababu hizi hubeba laana ama baraka kutokana na matendo ya hao mababu wa ukoo wako. Kuna muda zinaweza kukusaidia ama kukudidimiza!! Ndiyo maana usifikiri wote wanaoanguka anguka makanisani ama misikitini ukafikiri wote ni majini hapana; hizi roho huwa zinatapatapa kama zikikosa uangalizi (kusujudiwa). Shida kubwa hutokea kama mababu wako waliingia maagano ambayo then kwa usomi wako ukaona hakuna umuhimu wa kuyafuatilia.

Majini hayo yaliumbwa pia na Mwenyezi Mungu ila yalilaaniwa na kutupwa hapa duniani, yanajifanua kuwa na nguvu za uungu ndani yake na kutaka kuabudiwa pia.
 
Mizimu ina nguvu sana; watu wengi wanapata adhabu bila wao kujua kwa nini; kumbe babu zao waliabudu hiyo mizimu toka enzi na enzi; sasa kizazi kipya kinaacha na kuona ni mambo ya kale hapo ndipo matatizo yanapoanza; ukoo unakuwa wa kufa hovyo hovyo kwa kuugua ama kwa ajali ama ukoo hawaolewi wala kuoa wanaishi kihunihuni tu ama ukoo wa mashoga na wasagaji hayo yote yanatokana na laana kutoyajali maagano ambayo mababu yali sign.
 
Je Mchawi anaweza kuwa mganga ?
Swali zuri sana; je dereva anaweza kuwa fundi? Jibu: utasema dereva mzuri ni yule anayejua kutengeza gari pia.

Waganga wengi wanajua namna uchawi unavyofanya kazi lakini kama nilivyosema mwanzo mizimu ya mganga haiwezi kukubali kuroga... Mizimu ya Uganga huwa inajitolea tu kuponyesha watu haiwezi ikarudi kuwadburu tena.

Mganga anajua kila kitu kubusu uchawi lakini hawezi kufanya - kiapo cha kimizimu hawezi kukiepuka kamwe.
 
Back
Top Bottom