Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 3,119
- 1,428
MASACHE KASAKA ACHUKUA FOMU INEC YA UBUNGE JIMBO LA LUPA
MGOMBEA wa Kiti cha Ubunge wa Jimbo la Lupa, Wilaya ya Chunya Kwa tiketi ya CCM Ndg. Masache Njelu Kasaka leo tarehe 25/8/2025 amechukua fomu za uteuzi wa Wagombea Kiti cha Ubunge Jimbo la Lupa, Wilaya ya Chunya kutoka Kwa Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi Jimbo la Lupa Ndg. Athuman Bamba Kwa Niaba ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC)
Ndugu Masache Kasaka amefika katika Ofisi za Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) na kuchukua fomu kwaajili ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Lupa Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Mwezi Oktoba 2025.
Itakumbukwa kuwa, Masache Kasaka ameliwakilisha Jimbo la Lupa katika Bunge la 12 (2020-2025) na sasa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imemteua tena kuwatumikia wananchi Jimboni katika Bunge la 13 (2025-2030)
Uteuzi huu ni sehemu ya majina ya wagombea walioteuliwa rasmi na CCM kupeperusha bendera ya chama hicho kuwania ubunge katika majimbo mbalimbali nchini yaliyotangazwa, tarehe 23 Agosti, 2025, jijini Dodoma.
Hongera sana Ndugu MASACHE KASAKA kwa kuteuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kugombea nafasi ya Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Jimbo la Lupa
Kila la heri katika kampeni za Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba, 2025.
#OktobaTunatiki✅
#KazinaUtuTunasongaMbele
#TunazimaZoteTunawashaKijani