Ulukolokwitanga
JF-Expert Member
- Sep 18, 2010
- 8,396
- 7,968
kwangu nimewataarishia mapokezi mazuriBaada ya kusubiri kwa miaka kumi hatimaye imebakia masaa 48 tu kuhesabiwa ili serikali ipate takwimu inazohitaji. Nikiwa kama raia mwema wa Tanzania nimejiandaa vya kutosha kuhesabiwa na ninao wajibu wa kuwahamasisha watanzania wenzangu wahesabiwe. Ewe mwana JF mwenzangu, ewe Mtanzania mwenzangu huu ni wakati muafaka kuhesabiwa. Its a once in ten years opportunity. Kwangu nimeandaa soda na keki kwa ajili ya karani na kiongozi wa mtaa kujiburudisha huku wananiuliza maswali mkuu wa kaya.
SENSA KWA MAENDELEO YA TAIFA...
Kama wewe ni mvuvi hoja yako ina mantiki maana wawindaji wa kabila la Hadzabe watapatiwa chakula bure na watapatia nyama za porini. Sensa kwa maendeleo ya taifaSihesabiwi mpaka nipewe pweza mie
Kutokutii mamlaka ni dhambi kwa mujibu wa Sheikh mkuu wa mkoa wa Dar. Tii mamlaka inayotawala. Muislam safi Alhaji Jakaya Mrisho Kikwete Khalfan atakuwa wa kwanza kuhesabiwa.Kwangu watakuta bango mlangoni (mimi muislam sihesabiwi)chezea waislam wewe!
Tii mamlaka, tii sheria za nchi kujenga Tanzania moja yenye amani. Kama hata ukitoa hela kwenye ATM unazihesabu kuona kama ziko kamili, kwa nini serikali isihesabu watu wake kujua idadi yao??amabo mko tayari kuhesabiwa hamasishaneni, tuliogoma nasi tuna hamasishana tuendelee na msimamo wetu.
All the best kwa pande zote.
Mwambie ndio imesababisha serikali kujenga shule za kata baada ya takwimu kuonesha kuwa idadi kubwa ya vijana walio shule za msingi watakaohitaji kuanza sekondari. Pia ujenzi wa zahanati katika kata au vijiji hutegemea idadi ya watu, Isije tokea eneo mlilogomea sensa mkaonekana idadi yenu haitoshelezi kupatiwa dispensari au kituo cha afya halafu muanze kusingizia mfumo islamu au mfumo kristokuna kijana kaniuliza swali la kusikitisha sana.
Je sensa iliyopita imesaidia vipi ustawi wa jamii yetu?
Hata chama chako unacho support kitahitaji kujua idadi ya watu ili kijua maeneo gani ya kutoa kipaumbele wakati wa kampeni2002 tuliesabiwa lakini sijui kama serikali ilitumia takwimu kupanga maana matatizo bado pale pale.Tukimaliza sensa basi serikali ijikite kuamasisha swala rushwa kupita kila kaya na baada ya hapo turudi kwenye mapambano dhidi ya ufisadi kaya moja baada ya nyingine.
Sensa kwa maendeleo ya nchi,mi niko njiani narudi kutoka mkoani ili nihesabiwe kijijini kwangu Likurufusi bila kukosa ,sensa kwangu ni tukio muhimu kama vile kupiga kura,mii naandaa kabisa supu ya kuku wa kienyeji na togwa kwa ajili ya karani wa sensa atakaye kuja nihesabu kwenye kaya yanguBaada ya kusubiri kwa miaka kumi hatimaye imebakia masaa 48 tu kuhesabiwa ili serikali ipate takwimu inazohitaji. Nikiwa kama raia mwema wa Tanzania nimejiandaa vya kutosha kuhesabiwa na ninao wajibu wa kuwahamasisha watanzania wenzangu wahesabiwe. Ewe mwana JF mwenzangu, ewe Mtanzania mwenzangu huu ni wakati muafaka kuhesabiwa. Its a once in ten years opportunity. Kwangu nimeandaa soda na keki kwa ajili ya karani na kiongozi wa mtaa kujiburudisha huku wananiuliza maswali mkuu wa kaya.
SENSA KWA MAENDELEO YA TAIFA...