Mary Nagu atuambie

namtumbo

Member
Aug 30, 2011
78
102
Wiki hii kwenye mkutano wa wafanyabishara Mhe Mary Nagu katika kujibu swali la Mwenyekiti wa TPSF kuhusu mtazamo wa viongozi wa Serikali kuhusu ushiriki wa wazawa kwenye sekta ya gesi, aliwahakikishia wafanyabiashara kwamba mtazamo wa Badhi ya viongozi (akimlenga Prof.Muhongo) umebadilika kuhusu uwezo wa wazawa kushiriki kwenye biashara hiyo. Lengo langu sio kuongelea hoja hiyo leo hapa, bali nilipenda Mhe Nagu yeye kama Waziri mwenye dhamana ya uwezeshaji atueleze yafuatayo:

1) atutajie watanzania watatu waliowezeshwa chini ya Wizara yake. Watanzania hao ni akina nani? Wapo wapi? Wamepiga hatua gani? Atakapotuletea majibu haya atufahamishe pia vigezo vinavyotumika kuwezesha hao watanzania.

2) Zipi wapi fedha za mabilioni ya Kikwete? Baada ya disbursement ya kwanza, wangapi wamesharejesha fedha hizo, na baada ya kurejesha wangapi wamekopeshwa tena? Wangapi wameondoka kwenye umasikini baada kupata fedha hizo

3) Njia mojawapo ya kuwezesha wananchi ni kuweka mazingira ya kisera na kisheria yatakayopelekea wananchi kukopesheka katika taasisi za fedha na mabenki nchini. Ni hatua zipi Mhe Nagu amechukua kuhakikisha wananchi wanapata mikopo nafuu kwenye taasisi za fedha

4) Ukosefu wa fursa za mikopo kwa wananchi walio wengi kunapelekea wananchi kukimbilia kwenye mikopo ya muda mfupi kwa riba kubwa "Loan sharks". Watu wengi wamepata matatizo na mikopo hiyo ikiwa ni pamoja na kuuziwa nyumba zao, kunyanyasika, kutishiwa maisha na watoa mikopo ya aina hiyo. Je Mhe Nagu amechukua hatua gani za kuweka sheria za ku regulate hawa Loan Sharks waache kutoa mikopo ghali kuliko mikopo mingine yoyote duniani. Hivi sasa zipo baadhi ya Loan shark zinatoza riba ya ailimia 100 hadi 300 kwa mwezi. Je Mhe Nagu hiyo ni sawa?

Mhe Nagu unachotakiwa ni kuwa innovative na kufikiria nje ya boxi. Hivi unashindwaje kuweka sera mahususi ya kuamua kwamba kampuni yoyote inayoomba kazi ya ujenzi Serikalini, lazima iwe na ubia na kampuni ndogo ndogo za ujenzi....ili hizo kampuni ndogo zijingewe uwezo, ujuzi na kipato? Ethiopia wanafanya hivyo, vijana wanaomaliza engineering toka Chuo kikuu wanaambiwa wafungue firm zao......na kampuni yoyote kubwa ya ndani au nje inayoomba kazi ya Serikali lazima iwe na ubia na kampuni hizo ndogo ili ipate kazi. Vilevile vijana wanaomaliza shule ya Useremala kwenye VETA wanapewa mitaji kufungua kampuni, na kazi yoyote iliyo chini ya usd 100,000 sera na sheria zao zinalazimisha wapewe hao walioanzisha kampuni za useremala. mhe Nagu hili nalo linakushinda?

Mwisho natoa rai kwa mzee Mengi, TPSF inavyotetea maslahi ya sekta ya binafsi, isiangalie wafanyabiashara wakubwa peke yake, bali pia inagalie na kutetea maslahi ya wafanyabiashara wadogo pia ambao ni wengi na changamoto zao sio kubwa kama hizo za kuwekeza kwenye mafuta na gesi. Zile programu za mtangulizi wako Mama Esther Mkwizu za matching grants (ambapo wafanyabiashara wadogo na wa kati waliwezeshwa kwa kupatiwa mitaji kuanzia shilingi milioni moja hadi milioni 100
ni vema zikaendelezwa.



 
she is a con-woman... hata degree ya kufanyiwa kazi na wasaidizi, she is a very phony woman
 
Then hujui urembo ni nini:A S 13::A S 13:

Mheshimiwa Nagu, amekuja na ufumbuzi wa mvutano kati Mengi na Mhongo japo haikuwa official kwamba yy binafsi anaamin waliokuwa wanapinga sasa wamebadilika kimtazamo juu ya uwekezaji katika ges na mafuta. Mheshimiwa Mengi tangu mvutano ulipoaanza kila akipata dakika chache za TV, Lazima asemee hilo jambo. sasa Mengi Achana na hilo jambo kwani waziri kakuhakikihia kuwa selikal iko pamoja nanyi
 
Mheshimiwa Nagu, amekuja na ufumbuzi wa mvutano kati Mengi na Mhongo japo haikuwa official kwamba yy binafsi anaamin waliokuwa wanapinga sasa wamebadilika kimtazamo juu ya uwekezaji katika ges na mafuta. Mheshimiwa Mengi tangu mvutano ulipoaanza kila akipata dakika chache za TV, Lazima asemee hilo jambo. sasa Mengi Achana na hilo jambo kwani waziri kakuhakikihia kuwa selikal iko pamoja nanyi
aisee... umeamka na kaulanzi??

nasoma post yako na quote uliyofanya haviendani

au ndio mcharuko wa mawazo?
 
Huyu nagu anatafuta hela za uchaguzi kwa mengi mgonjwa kama mzee wake Lowasa hana jipya akili zake zenyewe kama za sugu tu.
 
Tumwache tu Nagu, amepewa tu kwa sbbu ya jenda hana anachoweza.
Huyu mama ni zaidi ya kibatali jenda zimesaidia wengi kazi kweli make akili yake kwa muhongo hata doti moja ya muhongo ni sawa akili za ukoo wao wote.
 
Huyu nagu anatafuta hela za uchaguzi kwa mengi mgonjwa kama mzee wake Lowasa hana jipya akili zake zenyewe kama za sugu tu.

umehama kambi ya lowassa? nyway huku Hana'ng huyo mary nagu kwisha habari yake jimbo mbunge wa cdm anasubiri kuapishwa
 
Back
Top Bottom