INAWEZEKANA KUBADILIKA.?Baba wa Taifa alitupeleka huko baada ya uhuru. Uzuri wake hawa unaowaona wote tunawapigia makofi ya tuna imani walisomeshwa kwenye mfumo huu.
Hii haikuwa dhana ya waanzilishi wa ujamaa, mfumo wa ujamaa unazingatia kwenye collectiveness, mapato ya nchi yanakusanywa na kuboresha miundo mbinu pamoja na huduma nyingine kwa faida ya wananchi wote. Serikali ndiye mmiliki wa rasilimali zote za nchi.Sijaelewa lengo hasa la MADA.
Kuhusu matabaka mifuko yote ina matabaka labda lililo muhimu ni kutanabaisha matabaka yepi. Kwa mfano kwenye mfumo wa ujamaa kulikuwa na kungali na tabaka la watawala. Chini ya mfumo wa chama kimoja vigogo wa chama hugeuka kuwa tabaka la watawala na kufaidi "MEMA" ya nchi.
OK...MAANA NAONA MFUMO HUO NI KAMA WAKINYONYAJI SANA DAH.Ki vipi ndio kwanza tunabadilika taratibu sasa hivi, kuingia kwa mfumo wa vyama vingi ni moja ya mabadiliko hayo.
AZIDI KUKUELEWA MFUMO HAUKUWA NA NIA YA UNYONYAJI SIO...?Ni wale walioaminiwa kwenye madaraka ndiyo wanakuwa na chance nzuri ya kunyonya. Ni mfumo unaohitaji nidhamu ya hali ya juu.
Mfumo huu ulilenga kwenye usawa, hakuna bwana na mtwana, wote ni ndugu. Ndiyo maana huku kwetu neno Sir lilifutwa wote tulikua Ndugu, Ndugu Juma, Ndugu Peter....ect. Lakini cha ajabu hata waliouanzisha wameushindwa. Ni mfumo mgumu kuuteleza.N
AZIDI KUKUELEWA MFUMO HAUKUWA NA NIA YA UNYONYAJI SIO...?
Hii haikuwa dhana ya waanzilishi wa ujamaa, mfumo wa ujamaa unazingatia kwenye collectiveness, mapato ya nchi yanakusanywa na kuboresha miundo mbinu pamoja na huduma nyingine kwa faida ya wananchi wote. Serikali ndiye mmiliki wa rasilimali zote za nchi.
Kwenye ujamaa hakuna tabaka la watawala bali kuna viongozi wanaochaguliwa kidemokrasia kama wawakilishi wa wananchi.
Haya maandishi ni matamu sana...hawa watu walilenga kuleta usawa katika jamii, unfortunately equality is not an element of nature...napenda sana history, it seems that our future lie within out past.Marxism–Leninism ni mfumo wa siasa au uliojulikana duniani kama Marxism na Leninism, lengo lilikua kuanzisha serikali za kijamaa na kuziendeleza zaidi. Marxist–Leninists walihodhi mfumo huu na waliusambaza pembe zote za dunia kutokana na uelewa wa sehemu ile, lakini kipaumbele cha mfumo huu ilikua chama kimoja cha kisiasa kitakacho endesha serikali ambayo itasimami uchumi, maswala ya kimataifa, elimu, afya, jeshi, na maswala mengine yote. Hii ilikuwa tofauti na siasa za kibepari ambayo kuna tabaka la mabwana ambao walimiliki uchumi wa nchi. Siasa hii imebakia katika serikali za China, Cuba, Laos na Vietnam na huu ndio ulikua mfumo wa Communist Party of the Soviet Union (CPSU) na nchi nyingine za ulaya Mashariki (Eastern Block).
Marxism-Leninism kwanza walianza filosofa hii kwa mawazo yaliyofanana katika Muungano wa Kisoviet mnamo miaka ya 1920, wakati Joseph Stalin na wengine waliomuunga mkono kuchukua madaraka ya Chama Cha Kikomunist cha Urusi (bolsheviks). Kilikataa wazo hili la Umoja la Marxists wakati dunia ikiwa kwenye mapinduzi umuhimu wa siasa za ujamaa (siasa mkusanyo wa mapato) na baadae kuhama kutoka ubepari mpaka kufikia Taifa la kijamaa. Mwisho walikuja na mpango wa miaka mitano. Kimataifa pia mpango huu ulianza kutangazwa na kuanza kusaidia mapinduzi ya nchi nyingine ili ziunge mkono mfumo huu wa siasa.
Vladimir Lenin