Marufuku kuokota embe hapa!!

Joined
May 8, 2012
Posts
29
Reaction score
4
Mtoto mmoja alikuwa akiokota embe kwenye shamba la miembe la Mzee-Kijana. Mara yule Mzee-Kijana naye ghafla akaja kuliangalia shamba lake na kumkuta yule Mtoto akiokota embe kwenye shamba lake. Mzee-Kijana akamwambia yule Mtoto; leo iwe mwanzo na mwisho wa kuokota embe kwenye shamba langu. Yule Mtoto akajibu; sawa Mzee nimekuelewa. Baada ya siku 3 yule Mtoto akaenda tena kwenye shamba la miembe la yule Mzee-Kijana ili kula embe; lakini safari hii yule Mtoto aliamua kupanda juu kwenye mwembe ili akale embe akiwa juu. Mara na Mzee-Kijana akaja kwenye shamba lake kama kawaida na akamkuta yule Mtoto aliyemkataza asiokote embe kwenye shamba lake; tena safari hii akiwa juu ya mwembe. Akamwuliza; we Mtoto, hivi unakumbuka kwamba nilikuambia iwe mwanzo na mwisho kuokota embe kwenye shamba langu? Mtoto akajibu, ni kweli Mzee; lakini kumbuka kwamba ulinikataza KUOKOTA EMBE na sio KUCHUMA EMBE; sasa mimi leo SIOKOTI ila NACHUMA na ndio maana nikaamua kupanda juu ili NISIOKOTE EMBE zako ila NICHUME tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…