Mghoshingwa
JF-Expert Member
- Jul 9, 2011
- 305
- 74
Wana Jf, poleni kwa majukumu! Najitokeza kwa mara ya kwanza kuomba ushauri!
Nina mpenzi kwa miaka 4 hivi na tuna pendana sana. Kwa muda wote huu tulikuwa boy friend na girl friend. Mwez uliopita (september) bint alipata Ujauzito. Kimsing tulifurah sana. Niliamua kutuma wazaz wangu wapeleke posa. Jambo la kushangaza POSA ILIKATALIWA KWA KUWA MIMI NA HUYU BINT TUNASALI MADHEHEBU TOFAUTI. Yeye ni [colour=blue]MABATO[/colour] NA MIMI NI MLUTHERI. Wazazi wake hawataki kusikia lolote kuhusu ndoa japo wanajua binti yao ni MJAMZITO. Bint ananipenda na mimi nampenda pia. NAOMBENI USHAURI WADAU.
sasa unabishana nae au unamshauri,wazazi wa binti ndio wameshikilia hicho kigezo.mabato au sabato? dhehebu si kegezo bana ,watu wanaoana dini tofauti we unaongelea dhehebu
Kama unampenda na yeye anakupenda ongeza mtoto mwingine wakuleee!
Endelea kumpiga mimba nyingi kadiri uwezavyo, wenyewe watalegeza uzi
mimi ni msabato nacho jua mara nyingi wasabato huwa wanamtenga mwanao juu ya lile alilolifanya kiimani lakini ushauri mkubwa huwa ni kwamba yeye arudi kwenye darasa la ubatizo ajifunze upya na kubatizwa na mara ingine kama biti ataruhusiwa kuolewa na mwanaume mwenye dini tofauti ushauri mkubwa huwa ni kwamba mshauri mume wakawe msabato mfunge ndoa na akikataa basi alazimishwa
hapo kwenye blue ndio dini gani vile.
Maisha yawaumize kichwa, Dini nazo ziwatese......sishauri kubadili dini kwani wote ni wakristo wametofautiana siku za kuabudu na misingi ya kanisa....vema wakae na wazazi wawaruhusu, wakikataza basi kama kutengwa na watengwe, binadamu akikuchukia Mungu si upamoja naye
(Joshua1:9)[SUP]9 [/SUP]Have not I commanded you? Be strong, vigorous, and very courageous. Be not afraid, neither be dismayed, for the Lord your God is with you wherever you go
Kosa ulilolifanya ni kumpa mimba kabla ya kuoana, maana sasa unalazimika kutaka kumwoa hata kama hujajipanga sawasawa!!!
Siku zote kumbuka kuwa ndoa ni suala la MAPENZI, IMANI, JAMII, SHERIA na UCHUMI. Huwezi kukwepa kitu na ukijaribu tu kukwepa tegemea kupambana na matatizo mbele ya safari.
Tatizo hapo kwako ni JAMII(Wazazi na ndugu) na wala sio IMANI, nakushauri kufanya haya;
1/Jitahidi kuwashawishi zaidi wazazi ili wakuelewe(Tumia hata wazee wenye busara wenye ukaribu na wazazi
wake)
2/Angalia uwezekano wa kubadilisha dhehebu(Kama unahisi wazazi wako watapenda na wewe kama unapenda!!)
3/Tulia mpaka mchumba ajifungue halafu uanze mchakato upya(Huenda wazazi watakuja kukubali)
*Yote hayo yakishindikana basi na LIWALO NA LIWE, ama kumwoa au kutokumwoa kabisa, hilo unaamua mwenyewe pasipo kujali mtu!!!