Marufuku kula chakula ulichopika

oba

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
310
65
Moja ya hoja madokta wanayoidai serikalini ni kuwa waruhusiwe kula msosi wanaopika kwasababu kwa utaratibu wa sasa wapo madokta ambao ni marufuku kufanya hivyo.
Eti kwa mshahara wa dokta hana sifa ya kupewa green card ya bima ya afya- NHIF ila anapewa brown card. Hii ina maana kuwa kuna huduma za afya kadhaa ambazo hawezi kuzipata kwa bima hiyo na pia zipo hospital kadhaa za hali ya juu ambazo hawezi kwenda kutibiwa kwa kutegemea bima hiyo. Hii ina maana kuwa pamoja na kuwa yeye anaruhusiwa kuwapa watu wengine kiwango cha juu cha huduma ya afya yeye hana sifa ya kupata huduma hiyo. Ni sawa na kwamba anaingia jikoni kupika lakini haruhusiwi kula.
Hili nalo eti linahitaji PhD ili mtu ujue kuwa hapa serikali ilifanya ujinga, hivi mimi nitoe huduma ambayo mwenyewe sina sifa ya kuipata ni haki hii? kwa nini mfanyakazi wa afya asipewe hiyo kadi ya green irrespective of the salary?no wonder wagonjwa wengine wa bima wanakosa huduma bora kwasababu wanatibiwa na wataalamu wenye frustrations.
Serikali iache ujinga itumie tu hata akili ya mbumbumbu, mtu ambaye hajaenda shule, mambo mengine hayahitaji mogomo!!!
 
Back
Top Bottom