mayowela
JF-Expert Member
- Nov 2, 2014
- 2,124
- 1,746
Natumai tuko salama, nimeona nigusie hili suala kwa kuwa mi napenda maendeleo ya hivi vituo na ninapenda ubunifu.mimi sio mzuri sana wala sina ujuzi kwenye masoko pia kwenye media masscom (mawasiliano ya umma) siyafahamu ila napenda kufuatilia hivo vitu.
Clouds fm ni kituo cha muda mrefu na nikituo kinachoaminiwa sana na makampuni, mashirika ya serikari hata binafsi kwa kuteka vijana, na imeaminika na ndivyo ilivo kuwa biashara yako ili isikike kwenye masikio ya watanzania wengi ni vizuri upeleke tangazo lako Clouds, hiyo ina maanisha idara ya masoko na mauzo iko vizuri na ina ubunifu wa kutosha ili kuuza brand yao.
Lakini Clouds imekuwa ikifanya matamasha na udhamini mbalili mbali ili kujitangaza na kujipanua yaani kufikia wasikilizaji wake moja kwa moja hiyo ni nzuri.
Kwa upande wa Efm haina muda mrefu sana ila imejichukulia umaarufu sana kupitia matamasha kama komaa concert, saka saka, shika ndinga, nk na misemo yao kama ni kwikwi, Idara yao ya masoko pia iko vizuri kwa kubuni maudhui yanayomteka msikilizaji wa kawaida japo ilikuwa sehemu mmoja ila kwa sasa inajitanua kwa kasi.
(Marketing strategy) mbinu za kimasoko ni kama zinafanana ila hazifanani hata kidogo E-fm amekuja na vitu vipya ambavyo Clouds alikuwa hajasanuka navyo na alihisi havihitajiki kwa mlaji wake (msikilizaji) kama Singeli.. Clouds aliona anaenda kupoteza wasikilizaji wa Dar es salaam na pwani yote akacopy na kuiba mtangazaji wa E-fm (kicheko) japo alipokuwa kule alikuwa bora sana kuliko alipo sasa hii yaweza sabababishwa na kipindi anachofanya na muda kilipo.
Lakini pia E-fm akaja na Mida ya Kubet, vipindi vya michezo kufanyika ne hasa maeneo ya bar zinazoonesha mpira, Clouds akaona naachwa sasa nayeye akaanza na Kijiwe soka japo sijui kimefia wapi.hiin yote nikutafuta milage
E-fm alianza na kurusha vipindi nje ya studio alipata wasikilizaji sana na ilipendeza sana ila Clouds ni kama aliproove failure ikabidi abuni kitu kingine.
E-fm amekuja na vitasa day amabayo hufanyika kama leo sabasaba hupigwa mziki kutwa nzima hii naona Clouds hajaona kama inahamasa kwake.
E-fm kaja na shika ndika, wese day ambapo hugawa mafuta kwa wasikilizaji wenye boda boda na bajaji, pia joging club ambayo kwa sasa iko kule Mwanza mkoa mpya kimatangazo
Huu ni ubunifu mzuri kwa redio zote na zimeleta chahcu ya umsikilize nani na uzime wapi pia hii huvuta makampuni kudhamini vipindi mbali mbali ili yaweze kuuza bidhaa zao. Ila pia redio zingine nazo zijitahidi naona zinazidi kupotea tu na ukongwe wao ubunifu zero.