Sera za ubinafsishaji za awamu ya tatu kwa kiasi kikubwa zilikuwa matokeo ya legacy aliyoacha Thatcher na influence yake kwa IMF na World Bank.
Kuna siku Rais wa awamu ya tatu aliulizwa Mwalimu akiona jinsi watanzania wanavyoishi sasa hivi kitu gani kitamshangaza? akajibu "tumetengeneza MATAJIRI wengi, jambo ambalo halikutegemewa". Thatcher pia alitengeneza matajiri, lakini kule it was at expense of people's jobs, a lot of jobs were lost.
Yahoo wamefanya poll kuangalia ni watu wangapi wanasikitishwa na kifo cha Thatcher, imeonekana asilimia 43 wanafurahishwa na kifo cha Thatcher. Wachangiaji wa mjadala kwenye ile thread ya Yahoo wanalalamika kwanini poll imetolewa mapema kwa sababu wanaamini ingeendelea kuwepo matokeo yangekuwa reversed.
Wanasiasa waliompinga Thatcher na sera zake, ndio wanaomtetea baada ya kifo chake. Wadau wameshtukia kuwa wanasiasa hawa wanapigania legacy ya chama chao cha Conservative na si ya Thatcher.
Kuna wanaoamini kuwa Thatcher ameboresha esteem ya mtoto wa kike kuwa anaweza kuwa kiongozi wa juu, Obama ni mmoja wa waliotoa kauli hiyo. Hata hivyo wadau wengine wanaona kuwa utawala wake umeharibu kabisa image ya kiongozi mwanamke!
My take: Margaret Thatcher policies and impact could be a very interesting PhD title...