Marekani yaua magaidi wa ISIS zaidi ya 80

ze kokuyo

JF-Expert Member
Jan 24, 2014
7,417
9,603
Jeshi la marekani limefanya mashambulizi ya anga huko nchini Libya,ambapo yalilenga kambi za mafunzo za Isis.
Ndege mbili za marekani za mashambulizi mazito ikiwemo ya nyuklia aina ya B-2 stealth ziliruka umbali wa karibu kilometa 9400(5700miles) kutoka Missouri nchini Marekani mpaka Libya kufanya mashambulizi kwenye kambi za mafunzo ya IS karibu na mji wa Sirte.
B2 ilishambulia kambi hizo kwa mabomu zaidi ya mia moja aina ya PGM(Precision Guidance Munitions) na kuua zaidi ya wapiganaji 85 wa IS na wale waliokua wanajaribu kukimbia wakati shambulio hilo likitekelezwa walishambuliwa na makombora aina ya Hellfire yaliyorushwa toka kwenye ndege isiyo na rubani aina ya MQ-9 Reaper.
Shambulio hilo liliidhinishwa na Rais Barrack Obama ikiwa zimebaki siku mbili kuondoka uongozini na kumpisha Rais mteule Donald Trump ambaye aliapishwa January 20 kuwa Rais wa 45 wa marekani.
 

Attachments

  • maxresdefault.jpg
    maxresdefault.jpg
    53.3 KB · Views: 327
  • article-1368337-0B451E1200000578-851_964x300.jpg
    article-1368337-0B451E1200000578-851_964x300.jpg
    36.5 KB · Views: 37
Ghaddafi

Pumzika kwa amani

Saizi libya imekuwa centre ya Isis

Ndege zinamimina mabomu angani tu

Tank za mafuta yanasafirishwa ughaibuni

Maisha bora,elimu bure hakuna tena

Siku ya kifo chako walikudhalilisha

Ila Leo wanadhalilishwa na drones,missiles kutoka kwenye ndege zisizo na rubani

Kila siku wanakufa Mediterranean sea

Curse of Ghaddafi
Pumzika kwa amani
 
UISLAM SIO UGAIDI. SOMENI NA KUELEWA UFAFANUZI HAPO CHINI. ALIEULIZA NI MWISLAM NA AMEJIBIWA NA MUISLAM.

JE NINI HUKUMU YA MWENYE KUJIUNGA NA DA‘ISH=ISIS


Nini hukumu ya kujiunga au ‎kuunga ‎mkono, kwa njia yoyote ile, makundi yenye siasa kali, kama Daish, ‎kwa kingereeza: ISIS, na ‎mengi mengine, yenye kudai kuwa yanapigana ‎Jihadi ili kurudisha Ukhalifa wa ‎umma wote duiani? Na nini hukumu ya ‎mwenye kujiunga nao?‎ Shukran.”‎

JIBU

BISMILLAH

Hakuna khilafu, baina ya wanazuoni wote wenye kuaminika na kuheshimika ‎kwamba Da‘ish, yenye ubembuzi wa ‎دولة ألإسلامية فى العراق والشام ‏‎ , au ISIS kwa ‎kiingerez (Islamic State of Iraq and Syria, au Lavand), kama walivyo liita ‎kundi hilo wale waliolianzisha, ni kundi la KIGAIDI, ujambazi, uharamia, ‎ujangili, mauaji, na uaporaji wa mali na nchi, wanaotumia jina la Uwislamu ‎kwa lengo la siyo tu kusambaratisha mataifa ya Iraq na Syria, bali mataifa ya ‎Kiislamu, kwa upande mmoja, na kjuonesha kuwa Uwislamu ni dini ya ‎kigaidi, na ugaidi ndiyo Uwislamu. ‎

Ndiyo maana, wahanga wao wengi, zaidi, ni Waislamu, na nchi, zaidi, ‎wanazo fanya ufisadi wao, ni nchi za Kiislamu, na kuzidisha baadhi ya ‎vitibmbivyao vya kuripua na kujiripua, ni nchi chache zisizokuwa za ‎Kiislamu, ili kuonesha kuwa Uislamu ni ugaidi, na magaidi ni Waislamu. ‎
Vitendo yvo vyote, ni kusambaza vitisho, mauaji, ubakaji wa wanawake na ‎watoto, na kufanya uharibufu wa mali na miundo mbinu, kwa kujiripua ‎katika nchi mbali mbali, hata zisizokuwa za Kiislamu, ili kuonesha kuwa ‎Uwislamu na ugaidi ni kitu kimoja. ‎

Ni kundi lilioanzishwa na magenge ya “Upelelezi” bali ni Asasi za Uchochezi ‎wa baadhi ya Mataifa, yenye malengo yao ya kisiasa na kiuchumi, katika ‎enzi yetu wenyewe, hii, Asasasi ambazo, baadhi yake, zimeungama hadharani ‎kuwa wao, na waungaji mkono wenziwao, ndio waanzilishi na “wakunga” ‎wa “mtoto” huyo wa haramu. Na hivyo, ni wazi kuwa “mwanaharamu huyo” ‎anapewa kila aina ya msaada kutimiza malengo yao, na hata kuliwekea ‎kingozi wa kiyahudi, ambaye SI Mwislamu, aongoze kundi hilo na ‎kuwaandikisha vijana wa Kiislamu kutoka nchi mbali mbali, kwenda ‎kujiunga na magaidi hao, na kuungwa mkono na baadhi ya wanaojiita ‎Mashekhe wa Kiislamu, kwamba wapiganaji hao ni Mujahidiin na hivyo ni ‎budi kuwaunga mkono kwa hali na mali, na kujiunga nao kwa vitendo. Ila ‎mashekhe hao wanawazuwia watoto wao wenyewe, kujiunga na kundi hilo. ‎Yaani ni Mashekhe wanafiki, ambao wanahamasisha watoto wa wengine ‎kwenda machinjoni na kuua au wauliwe, lakini wao wenyewe au watoto wao ‎hawataki kuwapeleka. Wanafiki, madalali wa walioanzisha Da‘isha na ‎makundi mengine ya aina hiyo hiyo, duniani. Ni washangiliaji na wacheza ‎ngoma ya Ibilisi, Shaytani, adui wa Waislamu na Waumini. ‎

Uwislamu haujapata kuhubiri ugaidi, au uharamia na mauaji. Uwislamu ni ‎dini ya Amani, Utulivu, Ustahamilivu, Usamehevu, Umoja,, Upole, ‎Unyamavu, Unyoofu, Upendo na Huruma. Uwislamu ni kuamini kuwa ‎Hakuna Mola wa kuabudiwa, kwa haki isipokuwa Allah, na Muhammad ni ‎Mjumbe Wake.‎

Na Uwislamu haupiganiwi kwa mauaji, wala dhuluma, bali unahubiriwa ‎kwa njia za amani, utulivu, hekima na mawadha mema.‎

Mwenyezi Mungu amesema:‎
‎ادْعُ إِلَى سَبِيلِ رَبِّكَ بِالْحِكْمَةِ وَالْمَوْعِظَةِ الْحَسَنَةِ (النحل: 125 )‏
‎“Lingania Dini ya Mola wako kwa hekima na mawaidha mema.” An-Nahl: ‎‎125)‎

Uwislamu umepiga marufuku, kwa kauli na vitendo, ‎التطرف والتفريط‎ ‎UVUKAJI MIPAKA katika jambo lolote lile na Ukiukaji wa maadili, Uvunjai ‎wa Amani na Utuivu, na Mauaji hata kumuua mtu mmoja, asiye na makosa. ‎

Kumuua mtu mmoja asiye na makosa ni sawa na dhambi za kuua wanaadamu ‎wote. Na kuokoa maisha ya mtu mmoja ni sawa na kuokoa maisha ya ‎wanaadamu wote.‎

‎‏مَن قَتَلَ نَفْساً بِغَيْرِ نَفْسٍ أَوْ فَسَادٍ فِي الأَرْضِ فَكَأَنَّمَا قَتَلَ النَّاسَ جَمِيعاً وَمَنْ أَحْيَاهَا فَكَأَنَّمَا أَحْيَا النَّاسَ ‏جَمِيعاً ‏( المائدة:32 ‏
‎“…Mwenye kuua mtu bila ya yeye kuua, au kufanya ufisadi (uharibifu, ‎uovu) katika nchi, basi ni kama amewaua watu wote. Na mwenye kuokoa ‎mtu na mauti ni kama aliyewaokoa watu wote.” (Al-Ma’ida:32)‎

Iweje uhusishwe Uwislamu na kuua watu ovyo ovyo, kupora wake wa watu ‎na kuwanajisi, kupora watoto wao wa kike, na kuwafanya watumwa! ‎Kuteketeza mali, majumba, miundo mbinu na kadhalika, wakati sote tunajuwa ‎maagizo ya Mtume ‎ﷺ‎ kwa majeshi ya Waislamu waliokuwa wanaenda ‎kuhami na kujitetea: ‎

‎‏(انْطَلِقُوا بِاسْمِ اللَّهِ وَبِاللَّهِ وَعَلَى مِلَّةِ رَسُولِ اللَّهِ، وَلَا تَقْتُلُوا شَيْخًا فَانِيًا وَلَا طِفْلًا وَلَا صَغِيرًا وَلَا امْرَأَةً، وَلَا ‏تَغُلُّوا، وَضُمُّوا ‏غَنَائِمَكُمْ، وَأَصْلِحُوا وَأَحْسِنُوا إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ) سنن أبي داود
‎“Nendeni kwa Jina la Mwenyezi Mungu, na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ‎na kwa mujibu wa Dini\mafunzo ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! ‎Msimuue mtu mzima, mkongwe, wala mtoto mchanga, wala mtoto mdogo, ‎wala mwanamke! Na MSIVUKE MIPAKA (MSIPINDUKIE MIPAKA ‎MLIYO WEKEWA KATIKA SHARIA). Na kusanyeni pamoja ghanima ‎zenu (siyo kila mtu ajichukulie apatacho). Na fanyeni suluhu, na wema. ‎Kwani Mwenyezi Mungu anawapenda wenye kutenada mema.” Amiopokea ‎Abu Daud.‎

Uko wapi Mwongozo wa Uwislamu, huo, ulitolewa na Mtume ‎ﷺ‎ wakati wa ‎mapigano, na mwongozo wa vitendo vya Da‘ish\ISIS na washirika wao, au ‎magenge mengine kama wao –yenye majina mbali mbali-, katika kauli zao, ‎vitendo vyao, misimamo yao, na malengo yao!!!? Wako mbali kabisa na ‎Mwongozo wa Uwislamu katika kujihami, umbali wa mashariki na ‎magharibi ya kuchomoza Jua na kuchwa Jua. Umbali wa mbingu na ardhi.‎

Msikilize Khalifa wa Mtume ‎ﷺ‎, Sayyidina Abu Bakr ‎رضي الله عنه‎ anawaambia ‎nini wanajeshi wa Kiislamu, pale alipowatuma kwenda nje ya Madina kutetea ‎na kujihami, dhidi ya vitisho na vitendo vya waliokuwa wakitishia usalma ‎wao. ‎

Sayyidina Abu Bakr ‎رضي الله عنه‎ alikuwa akiwausia wapiganaji wa Jihadi kwa ‎wasia huo huo wa Mtume ‎ﷺ‎ . ‎

Alimuusia Yazid bin Abi Sufyan ‎رضي الله عنهما‎ [huyi ni Swahaba wa Mtume ‎ﷺ‎, si Yazid, mtoto wa Mu‘awiya bin Abi Sufyan, ambaye SI swahaba] ‎alipompa uwongozi wa “platuni” =kikosi kidogo cha jeshi moja la Waislamu, ‎waliokuwa wanaelekea Shaam, kwa kumwabia: ‎

‎‏...إنك ستجد قوما زعموا أنهم حبسوا أنفسهم لله فذرهم وما زعموا أنهم حبسوا أنفسهم له وستجد قوما ‏فحصوا عن أوساط رءوسهم من الشعر فاضرب ما فحصوا عنه بالسيف وإني موصيك بعشر لا تقتلن ‏امرأة ولا صبيا ولا كبيرا هرما ولا تقطعن شجرا مثمرا ولا تخربن عامرا ولا تعقرن شاة ولا بعيرا إلا ‏لمأكلة ولا تحرقن نحلا ولا تغرقنه ولا تغلل ولا تجبن (رواه مالك فى الموطأ)‏
‎“…Utakutana na watu wanao dai kuwa ni wachamungu waliojitolea nafsi zao ‎kumuabudu Mwenyezi Mungu (yaani Makasisi na Marabai). Ukikutana nao ‎waache na madi yao hayo!(ie usiwadhuru wala kuwabughudhi!) Na ‎utakutana na watu waliopasua nywele zao utosini, hao wakate nywele zao ‎kwa upanga (wapagani wa Shaam). Na nakuusia mambo kumi: 1. Kamwe ‎msiue mwanamke, 2. Wala mtoto mdogo, 3. Wala mzee kikongwe, 4. Wala ‎msikate mti wa matunda, 5. Wala msiangamize jengo, 6. Wala msiue ovyo ‎mbuzi au ngamia, isipokuwa kuchinja kwa ajili ya chakula chenu, tu, 7. Wala ‎msichome moto sega la nyuki, 8. Wala msilivunje, 9. Wala msiibe kutokana ‎kwenye ngawira, 10 na wala msiwe waoga!” Ameipokea Malik katika ‎Muwatta’.‎

Na huo ndio uliokuwa wasia wa Sayyidina Umar ‎رضي الله عنه‎ kwa wapiganaji ‎wa Jihadi katika Uwislamu, kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Bali ndio ‎muongozo halisi wa Uwislamu katika hali ya vita.‎

Hivyo, iweje wapiganaji wa Da‘ish, au wanaofuata nyayo zao na vitendo ‎vyao, chini ya majina mbali mbali ya uhadaifu na udanganhifu, wawe ni ‎wapiganaji wa Jihadi katika Uwislamu!!!!?? ‎

Iweje, Da‘ish na makundi mengine yanayofuata nyayo zao na vitendo vyao, ‎wawe Waislamu, vile lengo lau kubwa na furaha yao kubwa ni kuua, ‎kuadhibu na kuchoma moto Waislamu, kuharibu mali za Waislamu, ‎kupigania na kutetea magenge yenye malengo mbali mbali, tokea ya kisiasa, ‎kijamii, kiuchumi hadi chuki na uadui dhidi ya makundi mengine!? ‎

Makundi yote haya, yenye kufanya vitendo hivyo, yanaingia katika Hadithi ‎ya Mtume ‎ﷺ‎ ifuatayo, na nyingi nyengine kama hadithi hiyo:‎

‎عن أبي هريرة عن النبي صلى الله عليه وسلم أنه قال من خرج من الطاعة وفارق الجماعة فمات مات ‏ميتة جاهلية ومن قاتل تحت راية عمية يغضب لعصبة أو يدعو إلى عصبة أو ينصر عصبة فقتل فقتلة ‏جاهلية ومن خرج على أمتي يضرب برها وفاجرها ولا يتحاشى من مؤمنها ولا يفي لذي عهد عهده ‏فليس مني ولست منه (رواه مسلم)‏
Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayra ‎رضي الله عنه‎ akisema: Amesema Mtume ‎ﷺ‎ “Atayejitoa kwenye utiifu akajitenga na Umma na akafa, basi amekufa ‎kifo cha Ujahiliyya (si Mwislamu). Na atayepigana chini ya uwongozi pofu, ‎anakasirika kwa ajili ya genge fulani, au ana hubiri kujiunga na genge fulani, ‎au anatetea genge fulani, akauliwa basi ameuliwa katika kifo cha Ujahiliyya. ‎Na yeyote ataye toka kuwashambulia watu wa Umma wangu, akiua ovyo ‎ovyo: mja mwema na mja muovu; pasi na kumchelea hata Muumini wao, ‎wala kutkeleza dhimma ya waliopewa hifadhi katika Uwislamu (Yaani anaua ‎ovyo ovyo, Waislamu wema na wasiokuwa wema, bali hata Ahl al-Kitaab), ‎basi mtu huyo hahusiani name na wala mimi sihusiani naye (si Mwislamu)”. ‎Ameipokea Muslim. ‎

Yaani kwa ufupi, mwenyue kujiunga na kundi potofu, pofu, akiua ovyo ‎ovyo, Waislamu na wasiokuwa Waislamu, Waislamu wema na waislamu ‎waovu; hachelei asemayo, wala atendayo, wala hachelei dhambi za vitendo ‎vyake hivyo, basi huyo si Mwislamu, hata kidogo.‎

Hivyo, kujiunga na kundi lolote lenye muelekeo kama huo wa ISIS, ambao ni ‎wafuasi na wajukuu au vitukuu vya Uwahabi, jambo ambalo hata wao ‎wenyewe ISIS na makundi mengine wanakiri hilo na wala hawafichi ufuasi ‎wao huo, ni haramu; sawa sawa iwe kuungana nao kwa vitendo, au kwa ‎kuwasaidia kwa mali, au kwa kuwatetea kwa kauli, au hata kufurahia viendo ‎vyao hivyo, ni ugaidi ni uharamia, ni kujitoa katika Uwislamu. Hata ‎kufurahia na kushangilia uovu huo ni kujitoa katika Uwislamu.‎

Mwenye kuungana nao, kwa kauli, au vitendo, au mali, au imani, au itikadi, ‎atakuwa amemuasi Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na amejitoa kwenye ‎Njia ya Haki, na amepotoka upotofu ulio wazi kabisa:‎

‎يقول الله تعالى: (وَمَنْ يَعْصِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُبِينًا) الأحزاب/ 36‏
Da‘ish na ndugu zao wengine, wote, ni genge la kigaidi, na kujiunga nao, ‎kwa njia yoyote ile, ni kujiunga na ugaidi, na hivyo ni kujitoa katika ‎Uwislamu, na hatima yake, kwa asiyetubu, ni kufia kifo cha Ujahiliyya, ‎والعياذ ‏بالله‎ .‎

Na yeyote atayejiunga nao, au akapigana chini ya bendera yao, au chini ya ‎uwongozi wao, basi ni gaidi, mwenye kiu cha kuua watu wasio na makosa, ‎kupora mali za watu, kunajisi wanawake na watoto, na mmojawapo wa ‎mafisadi wakubwa, walio kasirikiwa na Mwenyezi Mungu na kulaaniwa ‎Naaye, ambao Moto mkali ndio adhabu yao, na ndio makaazi yao milele.. ‎Mwenyezi Mungu amesema, katika Qur’ani:‎
‎‏(وَمَنْ يَقْتُلْ مُؤْمِنًا مُتَعَمِّدًا فَجَزَاؤُهُ جَهَنَّمُ خَالِدًا فِيهَا وَغَضِبَ اللَّهُ عَلَيْهِ وَلَعَنَهُ وَأَعَدَّ لَهُ عَذَابًا عَظِيمًا) ‏النساء/ 93‏
‎“Na mwenye kumuua Mu’mini, kwa makusudi, basi malipo yake ni ‎Jahannamu, humo atadumu, na Mwenyezi Mugu amemkasirikia, na ‎amemlaani, na amemuandalia adhabu kubwa na kali.” (An-Nisa’: 93)‎

Hawa na wafuasi wao, iwe kwa vitendo, au kwa kauli, au kwa mali, au kwa ‎kuhamasisha watu waungane nao, au kwa kuchangisha michango ya ‎kuwasaidia, iwe kwa dhahiri au kwa siri, ni ugaidi, ni ufisadi, ni uharamia, ni ‎wizi, na hivyo Uwislamu hauhusiani nao, na wala wao hawahusiani na ‎Uwislamu, hata kama watadai vipi na vipi kuwa wao wanafanya hivyo kwa ‎ajili ya Uwislamu. Maana Uwislmu haukai chungu kimoja na Mauaji, Ufisadi, ‎Uporji wa mali, Vitosho, Uvunjaji wa Amani na Utulifu, Uvunjaji wa ‎Usalama, Upandikizaji wa Chuki na Uhasama miongoni mwa Waislamu na ‎wasiokuwa Waislamu, bali hata miongoni mwa Waislamu weneywe kwa ‎wenyewe. ‎

Hivyo, ni juu ya Waislamu kwa ujumla wao, na Viongozi wa Kiislamu, ‎katika nyanja zao mbali mbali, na wazee wa watoto vile vile, kuwanasihi ‎watoto wao, na hasa vijana wa Kiislamu, kutohadaika na mahubiri ya baadhi ‎ya mashekhe wapotofu, wanao waambia kuwa wakijiunga na makundi ‎hayo, kupigania jihadi, au wakijiripua au wakiuliwa basi watakwenda Peponi ‎moja kwa moja, na kuozeshwa mahuru al-ayn, 70 kila mmoja! Kama hayo ‎ndiyo malipo, kwanini mashekhe hao hawaendi wenyewe, wakawa mstari wa ‎mbele kujiunga na makundi hayo, ili waingie Peponi kwa haraka zaidi, na ‎wakaozeshwe wanawake hao mahuru-al ayn!!! Ni wapotofu, na ‎wapotoshaji! Msikubali kuingizwa katika mitego hiyo ya upotofu, au ‎kuvutiwa na miito ya kuvutia na kaulimbiu hadaifu na danganyifu, za ‎kuwatoa mhanga wa matakwa yao au chuki zao binafsi. Wasikubali ‎kufanywa kama kondooo au mbuzi wanao ongozwa machinjoni, na ‎mashekhe wababaifu, wapotofu, wenye kutafuta masilahi yao binafsi, au ‎kutetea masilhaii masilahi ya mabwana zao. Maana Mtume ‎ﷺ‎ amesema:‎

‎‏ (الدِّينُ النَّصِيحَةُ، قُلْنَا: لِمَنْ؟ قَالَ: لِلَّهِ وَلِرَسُولِهِ وَلِأَئِمَّةِ المُسْلِمِينَ وَعَامَّتِهِمْ) صحيح ‏مسلم
‎“Dini na kupeana nasaha! Watu wakamuuliza: “Kwa ajili ya nani\nini?”, ‎akawajibu kwa kusema: “Kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mjumbe Wake, na ‎kwa ajili ya Viongozi wa Waislamu na kwa ajili ya Waislamu wote!” ‎Ameipokea Muslim.‎

Uwislamu ni Dini. Na Dini SI uchochezi! Dini SI uchonganishaji! Dini Si ‎mauaji! Dini SI kuchoma watu moto! Dini SI uporaji wa mali. Dini SI ‎ubakaji! Dini Si ufisadi! Dini Si uharamia! Dini Si uharibifu wa mali! Dini SI ‎uangamizji wa miundo mbinu! Dini Si kujiripua, wala kuripua wengine!‎

Dini ni kupeana nasaha! Dini ni Uwislamu, na Uwislamu ni Amani, Utulivu, ‎Ustahamilivu, Usamehevu, Umoja,, ‎Upole, Unyamavu, Unyoofu, Upendo na ‎Huruma. ‎Ni kumuabudu Mola wako, kwa dhati, na wakati huo huo ‎kuwasalimisha wengine na shari ya mkono wako au ulimi wako.‎

‎عن عبد الله بن عمرو ـ رضي الله عنهما ـ عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: المسلم من سلم ‏المسلمون من لسانه ويده، والمهاجر من هجر ما نهى الله عنه (متفق عليه)‏‎.‎
Imepokewa kutoka kwa ‘Abdullah bin ‘Amr ‎رضي الله عنهما‎ akisema: Amesema ‎Mtume ‎ﷺ‎ : “Mwilsmau ni yule ambaye wamesalimika Waislamu wenziwe na ‎ulimi wake na mkonowake. Na muhajir (mhamaji) ni uyule aliyehama yale ‎aliyo yakataza Mwenyezi Mungu kutendwa.” Muttafaq ‘Alayhi.‎
 
Hivi hayo maandishi ya ajabu ni lugha ya kiislam au kiarabu?? Huwa nashangaa mpaka mswali kwa kiarabu ndiyo huyo mungu wenu anawasikia???
 
Ghaddafi

Pumzika kwa amani

Saizi libya imekuwa centre ya Isis

Ndege zinamimina mabomu angani tu

Tank za mafuta yanasafirishwa ughaibuni

Maisha bora,elimu bure hakuna tena

Siku ya kifo chako walikudhalilisha

Ila Leo wanadhalilishwa na drones,missiles kutoka kwenye ndege zisizo na rubani

Kila siku wanakufa Mediterranean sea

Curse of Ghaddafi
Pumzika kwa amani

Yamenigusa mno maneno haya
 
Back
Top Bottom