Marekani yatuma wanajeshi 1000 Niger, ni baada ya mapinduzi ya kijeshi

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,000
17,909
Wiizara ya Ulinzi ya Marekani, Pentagon, imetangaza kuwa wanajeshi 1,000 wa nchi hiyo wametumwa tena nchini Niger.

Televisheni ya CNN imetangaza kuwa, afisa wa Pentagon ametangaza kuwa takriban wanajeshi 1,000 wa Marekani wamerudishwa katika kambi ya Agadiz nchini Niger baada ya kupinduliwa na kukamatwa Rais wa Niger, Mohamed Bazuom.

Jumatano iliyopita, kikosi cha Gadi ra Rais wa Niger kilimpindua kiongozi wa nchi hiyo, Mohamed Bazuom. Vikosi vya Ulinzi na Usalama vya nchi hiyo vilisema katika taarifa yao kwa vyombo vya habari kupitia televisheni ya taifa siku ya Jumatano, yaani saa chache baada za mapinduzi hayo, kuwa rais huyo anashikiliwa na maafisa wa kijeshi waliofanya mapinduzi.

Makamanda waliohusika na mapinduzi hayo wanamtuhumu Bazuom kuwa anahusika na hali mbaya ya usalama inayoshuhudiwa nchini Niger.

Niger ni nchi yenye hifadhi kubwa zaidi ya madini ya uranium duniani, lakini kwa upande mwingine, nchi hiyo inatambuliwa kuwa miongoni mwa "nchi maskini na zenye madeni makubwa" duniani. Uchumi wa nchi hiyo unategemea kilimo na mifugo na mauzo ya nje ya bidhaa ghafi.

Ni vyema kukumbusha pia kwamba nchi za Mali, Burkina Faso na Guinea Conakry zimeonya dhidi ya uingiliaji wowote wa kijeshi wa nchi za kiigeni dhidi ya Niger.

Taarifa ya pamoja iliyotolewa na nchi za Burkina Faso na Mali imesema kuwa hatua yoyote kama hiyo itakuwa sawa na tangazo la vita dhidi ya nchi hizo. "Uingiliaji wowote wa kijeshi nchini Niger utakuwa sawa na kutangaza vita dhidi yetu," imesema taarifa hiyo.

Taarifa ya serikali ya Guinea Conakry pia imesema kuwa, nchi hiyo haitatii vikwazo vya ECOWAS, ambavyo ni kinyume cha sheria. Baraza la utawala wa kijeshi wa Guinea Conakry limeonya kwamba "uingiliaji wa kijeshi nchini Niger utapelekea kusambaratika jumuiya ya ECOWAS."
 
Na Jana wakuu wa kijeshi wa nchi za ECOWAS wamekaa kikao kujadili njia za kijeshi huko Nigeria

Ngoja tuone mikwara ya wale vijana wenye mihemko kama itakuwa kweli,

Wiki Moja iliyotolewa na ECOWAS itamalizika keshokutwa tu,hapa ni patam kwa kweli!
 
Back
Top Bottom