Marekani yatoa Shilingi bilioni 97 kwa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Marekani yatoa Shilingi bilioni 97 kwa Tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Sep 15, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 15, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Balozi wa Marekani hapa nchini, Alfonso Lenhardt.


  p { margin-bottom: 0.08in; }
  Marekani imesaini mkataba na Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya umeme na usambazaji wake katika mikoa sita hapa nchini mradi ambao utagharimu Dola milioni 65 (sawa na Sh. bilioni 97.5).
  Msaada huo umetolewa na Marekani kupitia Millenium Challenge Accont Tanzania MCA Tanzania MCA-T
  Mkataba huo ulitiwa saini jana jijini Dar es Salaam kati ya viongozi kutoka makampuni mawili yatakayofanya kazi kutoka nchi Marekani ambapo Tanzania iliwakilishwa na Mtendaji Mkuu wa MCA-T, Bernald Mchomvu.
  Kazi hiyo itafanywa na kampuni ya Symbion's Power LLC inayoongozwa na Paul Hinks na Pike Electric inayoongozwa na Eric Pike ambapo watajenga njia za umeme zenye urefu wa kilimota 1600 katika mikoa ya Mwanza, Tanga, Dodoma Mbeya, Morogoro na Iringa.
  Utiaji saini wa mktaba huo ulishuhudiwa na Balozi wa Marekani hapa nchini, Alfonso Lenhardt.
  Akizungumza jana jijini Dar es Salaam katika hafla ya utiaji saini, Balozi Lenhardt alisema makampuni hayo yalipatikana baada ya kutangazwa tenda ya wazi ambapo watu mbalimbali walioomba lakini bahati nzuri waliopata wanatoka nchini mwake.
  Aliyataka kukamilisha kazi hiyo katika muda uliopangwa na kwamba ana imani nao katika utendaji wao wa kazi hivyo walimuangushe.
  Kwa upande wake, Mchomvu alisema wilaya 25 katika mikoa hiyo zitafaidika pamoja na Zanzibar.
  Alisema kazi hiyo inatarajia kukamilima mwaka 2013 na kuyataka makampuni hayo kufanya kazi yao huku yakizingatia muda waliopangiwa.
  Alisema hivi sasa asilimia 15 ya watu ndio wanaopata umeme na kwamba baada ya kazi hiyo kukamilika wanatarajia kuongeza kiwango hicho hadi kufikia asilimia 17.
  Maeneo yatakayofaidika na msaada huo ni pamoja na vijijini ambapo alisema shule, hospitali, viwanda vidogo kilimo cha umwagiliaji ni miongoni mwa taasisi zitakazofaidika.
  Kwa upande wao wakandarasi hao waliahidi kukamilisha kazi hiyo kulingana na muda waliopewa.  CHANZO: NIPASHE

  Tutategemea misaada toka kwa Wafadhili mpaka lini? Hii Nchi imechoka kweli tunakwenda kama gari lililokuwa Bovu pasipokuwa na kulifanyia matengenezo halitokwenda kazi kweli. kweli
   
Loading...