Marekani yasitisha msaada kwa sekta ya afya Kenya

jayec

JF-Expert Member
Feb 1, 2017
599
477
9 Mei 2017

Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) ambao hutumiwa na Marekani kutoa misaada kwa nchi za nje, limesitisha ufadhili wake kwa miradi ya afya nchini Kenya.

Taarifa kutoka kwa shirika hilo imesema hatua ya kusitisha ufadhili kwa miradi yote ya Wizara ya Afya ya Kenya imetokana na hatua ya Kenya kutotimiza "masharti ambayo hayajaelezwa".

Maafisa wa USAID wameagizwa kutojishughulisha na "shughuli zozote za kibiashara" na taasisi za serikali ya Kenya pamoja na mashirika mengine yenye uhusiano na serikali.

Hatua hiyo ya Marekani inatarajiwa kuathiri miradi mbalimbali ya serikali ikiwemo mipango ya kukabiliana na malaria, kifua kikuu na Ukimwi pamoja na miradi ya uzazi wa mpango, huduma za afya kwa wajawazito na watoto.

Kwa miezi kadha sasa, wizara ya afya nchini Kenya imekubwa na tuhuma za ulaji rushwa.

Sekta ya afya Kenya pia ilitatizwa na mgomo wa taifa madaktari ambao ulidumu kwa siku 100 kuanzia Desemba.

Mwaka uliopita, mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali alisema jumla ya dola 50 milioni hazikubainika zilivyotumiwa katika wizara ya afya.

Maafisa wakuu katika wizara ya afya pamoja na jamaa za baadhi ya viongozi wakuu serikalini walidaiwa kuhusika katika kufujwa kwa pesa hizo.

Wizara ya afya hata hivyo ilijitetea na kusema madai hayo yalikuwa kwenye ripoti ambayo ilifichuliwa mapema kabla ya wahasibu wa wizara hiyo kujibu maswali yaliyokuwa yameibuliwa na mkaguzi huyo kuhusu matumizi ya pesa hizo.

Mwandishi wa BBC Abdinoor Aden anasema hatua ya sasa hivi ya serikali ya Marekani itaibua maswali zaidi kuhusu usimamizi wa fedha katika Wizara ya Afya Kenya licha ya hatua ya rais Kenyatta ya kumhamisha Katibu Mkuu wa wizara hiyo.

Hatua ya USAID inatarajiwa kuathiri sana miradi ya serikali pamoja na miradi ya mashirika mengine ya afya ambayo hutumiwa an USAID kutoa huduma maeneo mbalimbali Kenya.
 
Wasitishe na kuja Kenya ikiwezekana Afrika..wanafiki wakubwa sana hawa, hawa lengo lolote la kutusaidia, ni unafiki tu wa viongozi wetu unatuponza waafrika ifike mahali tujue kwamba tunatakiwa kuishi bila ya kutegemea hawa nguruwe weupe
 
Huwa nakuona ukirukaruka kama mtoto anaeanza kutembea ukisikia Tz imesitishiwa misaada.

ndiyo Tanzania imesitishiwa misaada mingi sana kwasababu ya serikali ya CCM kufanya figisu kwenye uchaguzi wa Zanzibar na kutunga sheria kandamizi za uhuru wa habari na sheria onevu za mitandao ya kijamii.
 
Poleni sana, mlisema hamtegemeagi Misaada??
hii ni statement ya Kiafrika kabisa....very stupid statement...this is foreign aid...it is not good at all...inatufanya waafrika tulale tukitegemea nchi kama Marekani...I think this is a good move...ni wakati wa kujitegemea...naona comments nyingi hapa ni za Kiafrika kwel kwel and its very sad...very sad because as Africans we dont want t work for our prosperity..we want to capitalize on other people's work...America and other developed nations were never made great because of foreign aid...Nilifurahishwa na Magufuli aliposema reli ya TZ itakuwa financed na serikali ya TZ...jambo la busara sana...ona sisi tulipewa loan kutoka Uchina, sasa hivi bei ya sukari na unga ni ya kutisha! bajeti ni kubwa mno na mara nne ya the previous govt..debt has risen tremendously...TZ thats the way to go! let us refuse foreign aid.
 
Kwa mara ya kwanza leo naungana na wewe! I hate this chronic disease of depending on foreign aid!

Ndo maana hata ndege sisi sa hz tunanunua kwa hela yetu wenyewe!
 
ukiona masharti hayaelezwi ujue yana mahusiano na vitendo vya kishoga.
Sababu ni haikutumika ipasavyo. Na huu ni mwanzo wa mpango wa budget cuts for international development baada ya uongozi mpya kuingia madarakani. Misaada kutoka USA itaendelea kupungua kama sio kufutwa kabisa. Ni matumaini yetu sote serikali zetu zitafanya kwa matendo zaidi ya maneno ya majukwaani.
 
Back
Top Bottom