Boniphace Kichonge
JF-Expert Member
- Jul 31, 2017
- 1,605
- 1,958
Wadau wa JF
Serikali ya Marekani imeamua kusitisha misaada kwa Mamlaka ya Palestina.Uamuzi huo umefikiwa wiki mbili baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump kutishia kuacha kutoa msaada kwa Wapalestina. Maafisa wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani walisema jana kuwa nchi hiyo itatoa Dola milioni 60 kati ya Dola milioni 125 ambazo zilipangwa hapo kabla kwenda katika shirika hilo la UNRWA, lakini fedha zilizobakia zitazuiwa kwa sasa.
Hata hivyo, wizara hiyo imesisitiza kwamba uamuzi huo haujachukuliwa kwa lengo la kuwashinikiza viongozi wa Palestina, bali kwa sababu Marekani inataka nchi nyingine kusaidia katika malipo pamoja na kulifanyia mageuzi shirika hilo. Msemaji wa wizara hiyo, Heather Nauert amewaambia waandishi habari kwamba hatua hiyo haikusudii kumuadhibu mtu yeyote na kwamba kwa muda mrefu Marekani imekuwa mfadhili mkuu wa shirika hilo.
''Serikali ya Marekani na utawala wa Trump unaamini kwamba watu wanatakiwa kuchangia katika mzigo huu wa gharama. Tungependa nchi nyingine, hasa zile zinazoikosoa Marekani kwa kile zinachoamini kuhusu msimamo wetu dhidi ya Wapalestina, kujitokeza na kulisaidia shirika la UNRWA,'' alisema Nauert.
Chanzo: DW