kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 9,784
- 20,155
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani amepiga marufuku kufanyika karamu zozote zinazohusiana na mwezi mtukufu wa Ramadhani katika wizara hiyo mwaka huu.
Shirika la habari la IRNA limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, tangu mwaka 1999 hadi hivi sasa, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imekuwa ikialika watu kula futari katika siku za mwezi mtukufu wa Ramadhani au kushiriki katika sherehe za sikukuu ya Idul Fatr, ukitoa matukio machache tu.
Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Rex Tillerson mwaka huu amekataa ombi la idara ya kidini na masuala ya kimataifa ya wizara hiyo ya kualika watu kusherehekea sikukuu ya Idul Fitr kwenye wizara hiyo.
Tillerson amedai kuwa, wizara hiyo mwaka huu haina nia ya kuendesha ratiba maalumu kuhusiana na mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Kwa kawaida, waalikwa katika seherehe hizo za Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kuhusu mwezi mtukufu wa Ramadhani huwa ni wajumbe wa Baraza la Congress, viongozi wa jumuiya za Kiislamu, wanadiplomasia wa nchi za Kiislamu pamoja na viongozi wa ngazi za juu wa Marekani.
Tangu alipoingia madarakani Rais Donald Trump nchini Marekani, chuki dhidi ya Waislamu na matukufu yao zimeongezeka sana nchini humo.
Source;Parstoday
My take: Wapige na wasipige uislamu unakua kwa kasi zaidi duniani