Marekani yamgeukia binti wa Osama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Marekani yamgeukia binti wa Osama

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ehud, May 8, 2011.

 1. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #1
  May 8, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  KUFUATIA Binti Osama bin Laden kushuhudia baba yake akiuawa, Serikali ya Marekani imemweka katika ulini mkali na kumchunga nyendo zake kutokana na kuwa kipenzi cha baba yake.Gazeti la Time la Marekani limeeleza kuwa Binti huyo aliyejulikana kwa jina la Safiyah aliyezaliwa muda mfupi baada ya shambulio la Septemba11, 2011 anaweza kuwa ni mrithi wa Osama siku zijazo asipochungwa vizuri.

  Binti huyo aliyezaliwa na mmoja wa wake wa Osama raia wa Yemen, Amal Al Sadah, amewahi kutajwa na baba yake kuwa nimwerevu, mkakamavu na anayemwamini.

  Nimekuwa baba wa binti huyu baada ya Septemba 11. Nimempa jina la Safiyah ambaye aliwahi kumuua jasusi wa Kiyahudi nyakati za mtume. Binti yangu huyu ataua kila aliye adui wa Uislamu,” alikaririwa Osama na Mwandishi wa CNN nchini Pakistan, Hamid Mir, katika moja ya mahojiano yake akiwa hai.

  Hata hivyo, mama wa binti huyo, Amal alisema hakuna mtoto anayechagua kuwa azaliwe katika familia gani, lakini kutokana na mapenzi ya mtoto huyo kwa baba yake, maswali mengi aliyokuwa akimuuliza kutokana na udadisi wake pamoja na kashuhudia baba yake akiuawa ni kitu ambacho hawezi kukielezea.

  Mama wa mtoto huyo aliolewa na bin Laden mwaka 2000, mwaka mmoja kabla ya shambulio la Septemba 11 akiwa na umri wa miaka 18, wakati mumewe huyo mpya akiwa na umri wa miaka 43.Aliyekuwa mwalimu wa mama huyo, Sheikh Rashed Mohammed Saeed Ismail ambaye ndiye aliyewezesha ndoa yake na Bil Laden, alimwelezea kuwa katika umri wake mdogo, alikuwa mfuasi mzuri wa dini na mwenye imani ya kutosha, pia aliamini katika mambo ambayo bin Laden alikuwa akihubiri.

  Mwaka mmoja baada ya kuolewa, Amal alipata mtoto wa kike akiwa Kandahar na kumpa jina hilo la Safiyah, ambaye ndiye anayetajwa kushuhudia baba yake akiuawa na makomandoo wa Marekani.Hata hivyo, wataalamu wa masuala ya saikolojia na malezi wametahadharisha kuwa binti huyo anaweza kuwa mtu hatari sana kutokana na kushuhudia kifo cha baba yake.

  Kwa habari zaidi soma hapa Marekani yamgeukia binti wa Osama
   
 2. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #2
  May 8, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  isije ikawa yale yale...unamwondoa mtu na vizazi vyake vyote!
   
 3. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #3
  May 8, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  They are creating their own monsters. Amerika inatakiwa ibadilishe mtazamo wake kwa nchi zingine na ifute kabisa aspirations za kuitawala dunia. Kama wataendelea na lengo kama hizo basi wajue kutakua na watu tayari kuwapinga kwa kutumia njia zote zikiwemo terrorism.
  Nikama kusema: tuue wa masikini wote ili kumaliza umasikini duniani. Noble goal, wrong approach.
  Huyo mtoto hawezi kua na roho nzuri na wa america, kama vile watoto wa walio kufa in the world trade center hawawezi kua na roho nzuri na Osama. spiral inaendelea, kama movie vile. Akifa actor huyu anakuja mngine.
   
 4. k

  kilombero yetu JF-Expert Member

  #4
  May 8, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 1,007
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  osama mrith si lazima atokane na familia ya osama wapo wafuas wake wengi tu watarith kiti
   
Loading...