Marekani yadai imekalia visima vya Syria vya mafuta kisheria

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,045
18,014
Madai ya kijuba ya Marekani kuwa eti inakalia visima vya mafuta vya Syria kisheria

Nov 24, 2019 07:53 UTC

Tokea mwaka 2014, Marekani iliingia nchini Syria kinyume cha sheria kwa kisingizio cha kupambana na kundi la ISIS (Daesh). Kinyume na madai ya Rais Donald Trump wa Marekani kuwa ataondoa askari wa Marekani walioko Syria, hivi sasa wanajeshi hao wameongeza muda wa kuwepo kwao katika nchi hiyo ya Kiarabu kwa kisingizio kingine.

Trump amepanua majukumu ya wanajeshi wa Marekani huko Syria kwa kuwapa kazi ya eti kulinda visima vya mafuta mashariki mwa nchi hiyo. Uamuzi huo wa Marekani umekosolewa vikali katika duru mbali mbali.

Katika kujibu ukosoaji huo, James Jeffrey, mwakilishi maalumu wa serikali ya Marekani katika masuala ya Syria amedai kuwa, uwepo wa majeshi ya Marekani katika visima vya mafuta nchini Syria ni wa kisheria.

Jeffrey amedai kuwa: "Uwepo wetu katika visima vya mafuta nchini Syria ni wa kisheria. Naamini kuwa, hatua hii haikinzani na sheria za kimataifa. Sisi hatujafanya lolote kinyume cha sheria."

Katika kutetea uwepo wa majeshi ya Marekani mashariki mwa Syria, ameendelea kudai kuwa, wanamgambo wa Kikurdi wa Syria wanaojiita 'Vikosi vya Kidemokrasia vya Syria (SDF)' ndio wanaodhibiti visima hivyo na kile ambacho Marekani imefanya ni kuwarahisishia kazi yao.

Mwanzoni mwa Novemba 2019, pamoja na kuwa Trump alikuwa ameahidi kuondoa wanajeshi wa nchi yake huko Syria, alisema wanajeshi hao wataendelea kubakia katika nchi hiyo ya Kiarabu ili kulinda visima vya mafuta. Eneo ambalo wanajeshi wa Marekani waliko lina asilimia 90 ya akiba yote ya mafuta ghafi ya petroli ya Syria.

Lindsey Graham, seneta mwenye misimamo ya kufurutu ada wa chama cha Warepublican katika ujumbe kupitia ukurasa wake wa Twitter alitaka fedha zitakazopatikana katika uuzaji mafuta katika visima hivyo zitummike kwa ajili ya gharama za majeshi ya Marekani nchini Syria.

Baada ya Trump kutangaza kuondoa wanajeshi wa Marekani Syria, inaelekea kuwa, Graham na jenerali mstaafu wa Jeshi la Marekani, "Jack" Keane ambaye ni kati ya wachambuzi wa televisheni ya kihafidhina ya Fox News walimlazimisha abakishe baadhi ya askari hao katika maeneo yenye visima vya mafuta katika nchi hiyo ya Kiarabu.

Pamoja na hayo, Syria imekuwa ikisisitiza kuwa, majeshi ya Marekani yako nchini humo kinyume cha sheria kwani serikali ya Damascus haijawapa idhini. Kwa hivyo, hatua ya majeshi ya Marekani kuendelea kukalia kwa mabavu eneo la kaskazini mwa Syria inafanyika kwa lengo la kupora utajiri wa nchi hiyo hasa mafuta ya petroli. Bashar Ja'afari, Balozi wa Syria katika Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa, Marekani imekalia kwa mabavu visima vya mafuta vya Syria na wizi huo wa utajiri wa nchi yake unaendelea kutokana na kimya cha Baraza la Usalama.

Kinyume na ahadi za mara kwa mara za Trump kuwa wanajeshi wa nchi yake wataondoka Syria, lakini inonekana kuwa vyombo vya dola nchini Marekani vinapingana na wazo la rais huyo na kwa msingi huo, kufuatia mashinikizo ya Bunge la Kongresi, Trump ametangaza kutuma makomando 500 wa Marekani mashariki mwa Syria kwa kisingizio cha kulinda visima vya mafuta eneo hilo ili eti visishambuliwe na magaidi wa ISIS.

Kilichowazi ni kuwa Marekani inatafuta kisingizio cha kuendelea kuikalia kwa mabavu Syria. Kama alivyosema Sergei Lavrov, Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia: "Kulinda visima vya mafuta Syria ili visishambuliwe na magaidi ni kisingizio tu ili wanajeshi wa Marekani waendelee kuwepo Syria.

Utawala wa Trump sasa unataka kutumia unavyotaka utajiri wa mafuta ya Syria jambo ambalo ni ukiukwaji wa sheria za kimataifa ambazo zinapiga marufuku utumizi wa maliasili ya nchi huru bila idhini ya nchi hiyo.

Hivi sasa Marekani imeongeza idadi ya wanajeshi wake katika maeneo yenye visima vya mafuta katika mkoa wa Deir ez Zoor ambapo inajenga kituo kipya cha kijeshi eneo hilo. Wakati huo huo katika fremu ya mipango ya Marekani ya kuzigawa vipande vipande nchi za eneo la Asia Magharibi, serikali ya Trump inalenga kuibua utawala wa Kikurdi katika eneo la mashariki mwa Mto Furati ambapo gharama za kuunda utawala huo zitatokana na uuzaji wa mafuta katika visima hivyo vya Syria.

Kwa msingi huo si tu kuwa Marekani inaandaa mpango wa kuigawa Syria vipande vipande, bali pia inataka kuhakikisha kuwa mapigano ya ndani yanaendelea katika nchi hiyo ya Kiarabu. Hivyo lengo jingine ambalo Marekani inalifuatilia ni kuidhoofisha Syria ambayo ni mojawapo ya mihimili mikuu ya mrengo wa muqawama katika eneo.

Hili ndilo lengo ambalo utawala wa Kizayuni nao pia umekuwa ukilifuatilia.


4bsm81b57805141ioyj_800C450.jpeg


Chanzo: ParsToday
 
Ungananeni Russia,Iran na Syria mkamtoe huyo Mmarekani.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi wa Kiislamu amebainisha tofauti za kawaida za majeshi ya madola ya kiistikbari na jeshi la Jamhuri ya Kiislamu na kueleza kuwa: Jukumu kuu la majeshi ya madola ya ubeberu ni kufanya uvamizi, kughusubu na kutoa pigo kwa nchi nyingine lakini falsafa na mantiki ya vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kwamba, licha ya kuwa vimejiimarisha vilivyo kiulinzi, lakini uvamizi dhidi ya nchi nyingine kamwe hauna nafasi sera zake.
Matamshi ya Kiongozi Muadh
 
Back
Top Bottom