Mkuu,
Inamaanisha kuwa Marekani wanasimamia interest zao tu!
Kama hakuna interest zao, kafilie mbali...lakini kama kuna kitu wanataka basi watakupaka mafuta na kukusifu na kukuspray perfume kidogo.
Wakipata chao bomba..
Siku hizi si unasikia pia hapa kwetu mara balozi wa marekani ametoa milioni 20, mara marekani wamechangia nini...unafikiri wanatupenda?
Wanatia grease kulainisha deals zao tu.... Uliona vita ya Iraq, walipoingia walifanya nini? Kwanza kulinda visima vya mafuta...na demokrasi unaiona huko Iraq hadi hii leo au vipi?
Kwa hiyo mkuu, Marekani ni kulinda interest zao tu, hapendwi mtu!!
Umesahau wikileaks documents? Ni move zao kusambaratisha nchi ambazo walikwishazi/target zamani na unauona moto wake...wameuwasha kweli...
Hata ya kwetu wametoa ya Hosea na ushughulikiaji wa ufisadi na rushwa...wamemtaja nani ni kikwazo? Kwa hiyo hata hii yetu wanataka vitu vyao...