Marekani Rasmi kuiangusha Iran?

Marekani Rasmi kuiangusha Iran?

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,302
Reaction score
93,339
Na, Robert Heriel.

Ili uwe Kiranja wa dunia sharti utawala nchi zingine iwe kwa makubaliano maalumu au kwa mabavu. Hakuna nchi iliyowahi kuwa Super Power wa huu ulimwengu bila kuvamia nchi zingine. Ili nchi iweze kujitawala basi lazima itawale nchi zingine hata kama sio zote. Kutotawala nchi nyingine ni kushindwa kujitawala.

Marekani yupo katika Mihangaiko ya kuitawala dunia. Mpaka sasa amefikia hatua nzuri kukamilisha mpango wake wa kuiongoza dunia kikamilifu. Katika kutimiza mipango yake wapo watakaoumia na wapo watakaonufaika. Watakaoumia ni zile nchi anazozifuata ili kuziangusha. Watakaonufaika ni washirika wake wa nchi za Magharibi. Bila kumsahau Taifa la Urusi ambalo limewekwa kama adui Bandia kwa malengo ya kibiashara baina yake na Marekani.

Iran anayohaki ya kujitetea na wajibu wa kulinda maslahi yake. Pia Marekani anayohaki ya kupigania ukubwa wake ikiwa ataona umuhimu wa kufanya hivyo.

Iran ataangushwa kwa wakati wake. Marekani anajua namna ya kufanya biashara hasa ya kivita. Hawezi kuiangusha Iran kwa siku moja. Hapa atapata Hasara tofauti na atakavyomkawiza. Kupitia kumkawiza atauza silaha zake kwenye makundi yake yaliyopo mashariki ya kati. Hapo napo Iran yapo makundi anayoyasapoti hivyo hiyo itakuwa ni biashara katika vita. Unauza silaha unapata pesa. Baada ya Vita atakayeshinda anafaidika na mali za eneo husika. Iwe ni mafuta au mali yoyote ile. Hapa ni baada ya kuweka vibaraka watakaosimamia maslahi ya taifa lililosaidia ushindi.

Iran hana chaguo muhimu kushinda katika vita na Marekani zaidi ya kutumia kwa kificho (Indirect occurance) vikundi vya waasi au kigaidi kulipiza kisasi cha QASSIM SOLEIMAN aliyeuawa mnamo siku ya ijumaa katika nchi ya Iraq.

Hii ndio mbinu kidogo ambayo angalau Iran anaweza kuitumia katika kulipa kisasi chake. Lakini sio kwa kujiingiza moja kwa moja kwenye vita.

Iran lazima aelewe kuwa Marekani inamsubiri kwa hamu zote kuanzisha vita ili waangamize taifa lao. Bila shaka Iran hili wanalifahamu. Iran pia inafahamu kuwa haina uwezo wa kupambana na Marekani ikashinda. Iran lazima ijue kuwa kujiingiza kwenye vita na Marekani mapema ni kuwaisha kuanguka kwa taifa lao.

Iran inatakiwa itumie viikundi vya kibiashara za kivita kwa kigaidi au Waasi kulipa kisasi chao. Huu ndio utakuwa uamuzi sahihi. Kuliko kujiingiza kichwa kichwa katika vita ambavyo ni wazi Marekani ndio wanavihitaji kwa udi na uvumba.

Iran haitoweza Kushinda kamwe ikijiingiza kwenye Vita na Marekani kutokana na Sababu za msingi katika uwanja wa vita. Sababu hizo ni pamoja na;

1. Dhana za kivita na Teknolojia
Iran ni nchi inayoendelea tofauti na Marekani ambayo imeendelea katika nyanja karibia zote za maisha. Marekani inasilaha nyingi za kisasa na hatari ukilinganisha na Iran. Silaha ambazo bajeti yake ni kubwa. Pia Teknolojia ya Marekani ipo mbali ukilinganisha na Iran. Hii inapelekea Marekani kushinda endapo vita ikianza. Hili Iran wanalijua fika.

2. Uchumi
Uchumi unachangia kwa kiasi kikubwa ubora wa jeshi. Marekani inauchumi mkubwa hali ambayo inauwezo wa kununua, kutengeneza, kulipa wanajeshi au kutoa hongo kwa ajili ya kununua taarifa za msingi kutoka kwa mahasimu wao. Hii ni tofauti na Iran, uchumi wa Iran sio mkubwa sana. Bado ni nchi inayohitaji muda ili kusimama. Hata kama itanunua silaha hazitakuwa nyingi kukidhi mahitaji ya vita. Pia kama vita vikipigwa ni wazi uchumi wa taifa la Iran utaporomoka kwa kiasi kikubwa tofuati na Marekani.

3. Washirika
Moja ya mambo USA anajivunia ni kuwa na Washirika wenye nguvu. Nchi za magharibi ni nchi Washirika wa Marekani. Nchi hizi zimekuwa zikishirikiana katika misheni mbalimbali za kuvamia nchi zingine. Hii ni tofauti na Iran ambaye hana Washirika wa kueleweka. Hata huyo China ambaye kidogo ndiye mwenye unafuu bado hafurukuti linapokuja suala la kukabiliana na Marekani. Iran anatofauti nyingi za kimtazamo na Washirika wake. Kwa mfano, Iran wanafikra za dini ya kiislam wakati China hana fikra hizo. Na hiyo tumeiona juzi juzi ambapo Waislam waliopo China waliingizwa kwenye kambi maalumu ya kubadilishwa mtazamo yao ya kidini.

Wapo watu hufikiri Taifa la Urusi litaisapoti Iran jambo ambalo sio kweli hata kidogo. Nimekwisha sema, Urusi ni adui bandia wa Marekani kwa lengo la biashara hasa ya silaha. Haya mataifa hayana ugomvi wa ukweli bali wanachokifanya ni danganya toto. Bahati nzuri Iran analijua hili.

4. Intellejensia
Moja ya mambo ambayo yatamfanya Iran ashindwe endapo itatokea vita ni ishu ya intelejensia. Vyombo vya kukusanya taarifa ziwe za hatari au kawaida baina ya Iran na Marekani ni tofauti sana. Shirika la Kijasusi la Marekani - CIA ndilo shirika bora dunia kwa ufanisi katika kukusanya data na kuzifanyia kazi. Mbali na hivyo shirika hilo pia hushirikiana na mashirika ya mataifa mengine ambayo ni mashirika bora, mathalani shirika la kijasusi la Israel Mosad. Pia CIA kwa kificho hushirikiana na shirika la kijasui la Urusi katika kufanikisha mishine zao. Hii ni tofauti na Iran ambaye intelejensia yake bado haijkomaa ukilinganisha na Marekani. Sisemi kwamba intelejensia ya Iran ni ndogo bali nasema haiwezi kufurukuta kwa Marekani.

5. Kambi za Kijeshi (Military Base)
Marekani anakambi za kijeshi karibu dunia nzima tofauti na Iran. Mbaya zaidi Marekani anakambi mpaka karibu na nchi ya Iran. Kwa upande wa Magharibi mwa nchi ya Iran ipo nchi ya Iraq hapo Marekani anakambi zake za kijeshi. Kwa upande wa Mashariki Iran imepakana na nchi ya Afghanistan huko napo kuna kambi za kijeshi za Marekani. Saudi Arabia, United States of Arabs, Qatar, Oman, n.k. Nchi zote hizo zipo mdomoni mwa Iran. Hii ni kusema kama vita anza basi Iran atakuwa amezungukwa pande zote.

Iran haitaweza ingia kwenye vita kwa kujitakia ikiwa inafahamu fika kuwa hilo ndilo anguka lake. Kitakachofanyika ni kutumia makundi ya kigaidi kulipa kisasi chake. Kwa kutumia vikundi vya kigaidi itakuwa imejiondoa katika lawama za moja kwa moja kutoka kwa Marekani. Hivyo Marekani atakosa uhalali wa kuvamia taifa hilo.

Vita kama itaanza itakuwa ni vita yenye manufaa kwa Marekani. Lakini itakuwa ni hasara kwa Iran. Pia italeta mtikisiko wa Kiuchumi katika dunia kwa habari ya uchumi wa mafuta. Ni wazi mafuta yatapanda bei. Hivyo gharama za maisha nazo zitakuwa juu.

Vita hii ni muhimu kwa Marekani na sehemu ya taifa hilo kujiimairisha na kuongeza maeneo ya kiutawala. Marekani inapaswa ione kuwa kipi ni bora kati ya Maslahi yake au maslahi ya dunia kwa ujumla.

Ninachojua ni kuwa Marekani anatamani vita hii itokee. Hata Washirika wake wanatamani jambo hilo. Hasa hasa Saudi Arabia ambaye miaka ya hivi karibuni anaiona Iran kama taifa linalomzidi ushawishi Mashariki ya Kati.

Hatuombei Vita, lakini hatutajidanganya kuwa vita ni moja ya biashara zenye utajiri mkubwa katika mataifa makubwa. Vita ni pesa kwa aliyeiratibu. Vita ni sehemu ya sababu ya kutawala eneo fulani. Lakini vita ni sehemu ya kutetea nchi yako.

Vita vitaisha duniani endapo atatokea adui nje ya dunia yetu. Mfano kutoka sayari zingine. Lakini kama tutakuwa sisi kwa sisi vita havitaishi leo hata milele.

Kila la Kheri Iran katika kujitetea mbele ya Kaka Mkubwa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
 
Makundi yenyewe ya kigaidi ambayo unashauri iran wayatumie ndio hawa alshabab?

Alishabab anatunisha msuli kwa raia ambao hawana silaha yani kiufupi ni kundi la uviziaji ni kama panya road tu sema wao wame develop kwa silaha nzito kidogo

Alqaeda kidogo ilikua inatishio lakini nao tangu bosi wao afe saizi kila mmoja anaogopa kutanguliza mguu mbele
 
And this is a point, waajemi watanzania na walitambue

Bila kumsahau Taifa la Urusi ambalo limewekwa kama adui Bandia kwa malengo ya kibiashara baina yake na Marekani.
 
Hivi Kama Marekani anataka kuitawala Iran na anajua ni dhaifu anasubiri nini?,kawaida huvamia tu bila UN resolution kama alivyofanya kwa Irak.

Hata yeye anajua madhara ya vita kiuchumi na kijamii ndio maana hakurupuki,
Huu mchezo si wa kuufanyia propaganda.

Marekani ameshindwa vita vingi tu duniani,Vietnam alichemka,pia Syria,

Siku waarab waikjiitambua ndio utakua mwisho hili taifa la magaidi hapa duniani,acha waendelee kuuza siraha huku wakimwaga damu isio na hatia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
thetallest,

Iran sio dhaifu. Marekani anapata ukakasi kuivamia Iran sio kwa sababu Iran ina nguvu ya kuogopwa hasha!
Bali ni kutokana na sababu kuwa Urusi inaushirika wa kibiashara na Iran. Urusi imewekeza Iran. Hata China imewekeza Iran. Kuvamia Iran na kuipiga ni kugusa Maslahi ya Urusi na Uchina. Hapo kitakachofanyika ni lazimayawepo mazungumzo baina ya Marekani, Urusi na Uchina kabla vita haijaanza. Bila mazungumzo basi haitakuwa vita vya Marekani na Iran pekee bali Urusi atahusika(ila hategemewi) Uchina atahusika(huyu anategemewa japo sio sana).

Waajemi wajiandae kwa kweli
 
bado ni tishio, affiliates wake wametapakaa Burkina Faso, Mali, Cameroon, Niger, Nigeria, Chad na wana 'hit' ile mbaya
sijui unazungumzia 'tishio' kwa namna gani labda
 
bado ni tishio, affiliates wake wametapakaa Burkina Faso, Mali, Cameroon, Niger, Nigeria, Chad na wana 'hit' ile mbaya
sijui unazungumzia 'tishio' kwa namna gani labda
Alqaeda ni tishio kwa nchi kama hizo ulizotaja sio US na wao hilo wanalijua ndo maana wamenyuti kama hawajui kinachoendelea

It's Scars
 
huangalii/husikilizi habari wewe, eti wamenyuti

Nchi zote izo tayari wame respond kama walivyo respond Al-Shabab ndani ya izi siku 5 ( isipokua Chad na Niger) ambao wako mbioni
Hao alqaeda wanavimba wakiwa huku kwenye mataifa madogo halafu hata mashambulizi yao yakuvizia hawapigani face to face

Tanzania imesumbuliwa na jombi kwa miaka kadhaa huko nyuma lakini hiyo ilikua haimaanishi kua jombi anaweza kupambana vita uso kwa uso na wanajeshi wa tz, kwasababu anafanya uhalifu kwa kujificha

Hao alqaeda alshabab wote wamejifichia mistuni kwanini wanaogopa kuweka makambi yao hapa city center kama kweli hawaogopi?

Nani asiyeweza kumvizia mike tyson akiwa amelala kisha kumshushia ngumi nzito ya uso?

Ukiambiwa ukampige ngumi ya uso akiwa yupo macho utakubali?

Nakwambia hivi alqaeda, boko haram sijui alishababu na wapuuzi wengine hao ni wahuni wakitaa tu kwenye nchi kama zetu hizi lakini sio kuzihesabia kua zitaleta impact yeyote zikitumwa kuishambulia US



It's Scars
 
Back
Top Bottom