Sinoni
JF-Expert Member
- May 16, 2011
- 6,187
- 10,664
picha! Roy Moore, Jaji wa Mahakama Kuu katika jimbo la Alabama nchini Marekani
Habari kutoka nchini Marekani zinasema kuwa, Roy Moore amesimamishwa kazi na kuna uwezekano pia akafutwa kazi kabisa. Shirika la Habari la Reuters limeripoti kwamba, Moore ambaye amekuwa akipinga wazi vitendo ya mahusiano ya ngono baina ya watu wa jinsia moja, ametuhumiwa na kamisheni ya uchunguzi kwa kile kinachodaiwa na kamisheni hiyo kuwa ni kukiuka sheria za maadili katika jimbo hilo la Alabama. Kwa mujibu wa tuhuma hizo, Roy Moore hata anaweza kuachishwa kazi kabisa. Ni vyema kuashiria kuwa, kwa miaka mingi sasa sheria ya ndoa za watu wa jinsia moja imekuwa ikijadiliwa nchini Marekani, ambapo mwezi Juni mwaka jana mahakama kuu ya nchi hiyo iliwapa watu wanaofanya vitendo hivyo vichafu, haki ya kufunga ndoa hizo. Hii ni kusema kuwa, hatua Roy Moore ya kutoa amri ya kupinga vitendo hivyo vya kiasherati ni sawa na kupingana na mahakama kuu ya Federali nchini Marekani.