MAREKANI: Mwanamume Auawa Kimakosa Na Polisi

MAREKANI: Mwanamume Auawa Kimakosa Na Polisi

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Posts
5,500
Reaction score
8,067
Mwanamume aliyeuawa kimakosa jimboni Alabama, Marekani aliuawa kwa kupigwa risasi mara tatu kutoka nyuma, uchunguzi wa maiti yake umebaini.

1543922981594.png


Emantic Bradford Jr, anayefahamika kama EJ, alipigwa risasi kichwani, shingoni, na kwenye mfupa wa nyonga akiwa katika jumba la kibiashara la Riverchase Galleria mjini Hoover, Alabama.

Polisi walikuwa wamedhania yeye ndiye mshambuliaji aliyewaua watu wawili kwa kuwapiga risasi - mwanamume mmoja wa miaka 18 na msichana wa miaka 12 mwezi jana.

Lakini baadaye polisi walikisi kwamba walikuwa wamekosea, na sasa wamemkamata mwanamume mwingine wanayesema ndiye mshukiwa halisi. Mwanamume huyo anayezuiliwa kwa sasa, Erron Brown, 20, alijisalimisha mwenyewe kwa polisi.

Uchunguzi wa maiti yake, ulioombwa na familia ya Bradford, umebainisha kwmaba afisa wa polisi alimpiga risasi EJ mwenye miaka 21 mara tatu kutoka nyuma.

Benjamin Crump, wakili anayeiwakilisha familia ya Bradford, anadaiwa kuwaambia waandishi wa habari katika kikao kimoja kwamba kwa mujibu wa upasuaji huo wa maiti, "afisa huyu wa polisi anafaa kushtakiwa".

"Hakuna chochote kinachoweza kumpa sababu yoyote ya kumpiga EJ kwani anamuondokea."

Afisa huyo ametumwa likizo ya lazima, na uchunguzi unaendelea.

Hata hivyo, kufikia sasa maafisa wa serikali wametoa maelezo finyu sana kuhusu kisa hicho, na pia bado hawajatoa kanda ya video ya kamera aliyokuwa nayo afisa huyo wa polisi.

Kupitia taarifa ya pamoja iliyopeperushwa na kituo cha habari cha ABC News, meya wa Hoover Bw Frank Brocato na mkuu wa polisi Nicklaus Derzis walisema kwamba kutoa maelezo kama hayo kunaweza kuathiri uchunguzi. Bradford alikuwa amebeba silaha wakati akipigwa risasi, lakini alikuwa na leseni.

1543923184761.png

(Pichani: Waandamanaji wakitaka haki itendeke kuhusu Emantic Fitzgerald Bradford Jr)

Polisi wanasema kwamba alizidisha hisia za kuwa tishio eneo hilo baada yake kuchomoa bunduki yake milio ya risasi iliposikika ndani ya jumba hilo la kibiashara.

Chini ya sheria za Alabama, inaruhusiwa kubeba bunduki maeneo ya umma, lakini wamiliki wa jumba la kibiashara la Riverchase Galleria hawawaruhusu watu kuingia na risasi humo.

Chanzo: BBC
 
inasikitisha sana zee la usa bby lipo wapi?
 
Back
Top Bottom