Marekani kuweka masharti mapya ya viza

Marekani kuweka masharti mapya ya viza

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2012
Posts
2,047
Reaction score
3,978
Wengi miongoni mwa watu watakaoomba viza za kuingia nchini Marekani wanaweza hivi karibuni kuanza kuombwa utambulisho wao katika mitandao ya kijamii, historia ya safari walizozifanya, namba zao za simu na anuani ya barua pepe.

Haya yanakwenda sambamba na mapendekezo ya Rais Donald Trump ya kuwachunguza kwa kina raia wa nchi za nje wanaoingia nchini humo. Kulingana na maelekezo ya wizara ya mambo ya nje, masharti hayo yatawahusu watu milioni 14.7 kila mwaka, ambao wataombwa taarifa zao za mawasiliano na safari katika muda wa miaka mitano kabla ya tarehe ya kuomba viza.

Waomba viza vile vile wataombwa kueleza ikiwa waliwahi kufukuzwa kutoka Marekani, au iwapo kuna mtu aliye na uhusiano nao ambaye aliwahi kuhusika katika vitendo vya kigaidi.

Nchi kama Ujerumani, Ufaransa na Uingereza, ambazo raia wake hawahitaji viza kuingia Marekani, hazitahusishwa katika utaratibu huo mpya, lakini China na India ni miongoni mwa nchi zinazolengwa.
 
Mkuu hakuna Nchi inayoingia USA bila visa hizo ulizotaja masharti ya kupata visa ni mepesi ukilinganisha na Nchi zingine ..ingekua hivyo Wabongo,wapopo au wasenegali wangeenda UK na kuchukua uraia hili waende bila Visa USA...
 
Umetisha kiongozi
 
Hivyo vigezo ni kwa wageni wote au ni kwa sisi wa shithole countries tu?
 
Mkuu hakuna Nchi inayoingia USA bila visa hizo ulizotaja masharti ya kupata visa ni mepesi ukilinganisha na Nchi zingine ..ingekua hivyo Wabongo,wapopo au wasenegali wangeenda UK na kuchukua uraia hili waende bila Visa USA...

nilisikia mjerumani anaingia nchi zaidi ya mia moja bila viza... kama mtanzania akienda kenya au uganda. haitaji kwenda kujieleza ubalozini kuomba visa
 
Mkuu hakuna Nchi inayoingia USA bila visa hizo ulizotaja masharti ya kupata visa ni mepesi ukilinganisha na Nchi zingine ..ingekua hivyo Wabongo,wapopo au wasenegali wangeenda UK na kuchukua uraia hili waende bila Visa USA...
Ni kweli ukiwa na passport za hizo nchi hauhiultaji visa kuingia US na unavyosema sijui wapopo na wabongo wangechukua uraia wa Sijui U.K au France wewe unafikiri ni mchezo kupata huo uraia kwa hizo nchi wachilia mbali uraia viza tu. na ata ukipata huwezi kuhitaji tena kwenda US maana maisha ni mazuri kuliko ata hiyo US
 
Street life maana ya Visa ni kigezo anachopata mgeni kuingia Nchi husika sasa zipo aina Mbili za Visa kuna visa anapata mgeni anapoingia iwe border au airport na aina ingine ya visa ni kuiomba kabla haujasafiri ukiwa katika Nchi yako kwa ubalozi wa Nchi unayotaka kwenda kwa maana hiyo hizo Nchi zilizotajwa hawapewi hizo visa zote na wanaingia? Nchi ambazo hawatumii visa ni leseni ya udereva au kitambulisho cha kazi ni Scandinavian country ni muda wanafanya hivyo kwa kuzuia ugaidi Nchi karibu zote USA lazima wapate VISA...
 
Inaonekana unajuwa kuliko mtoa mada.....................
mimi ninachokifahamu ukiwa una VISA ya inchi mojawapo za ulaya ambayo VISA yao inaitwa
Schengen VISA , inauwezo wa kwenda inchi zote za bala la Ulaya na sio marekani ....
 
Mkuu hakuna Nchi inayoingia USA bila visa hizo ulizotaja masharti ya kupata visa ni mepesi ukilinganisha na Nchi zingine ..ingekua hivyo Wabongo,wapopo au wasenegali wangeenda UK na kuchukua uraia hili waende bila Visa USA...
Mbona kupata visa ya UK ni ngumu kupata kuliko US?
 
Wengi miongoni mwa watu watakaoomba viza za kuingia nchini Marekani wanaweza hivi karibuni kuanza kuombwa utambulisho wao katika mitandao ya kijamii, historia ya safari walizozifanya, namba zao za simu na anuani ya barua pepe.

Haya yanakwenda sambamba na mapendekezo ya Rais Donald Trump ya kuwachunguza kwa kina raia wa nchi za nje wanaoingia nchini humo. Kulingana na maelekezo ya wizara ya mambo ya nje, masharti hayo yatawahusu watu milioni 14.7 kila mwaka, ambao wataombwa taarifa zao za mawasiliano na safari katika muda wa miaka mitano kabla ya tarehe ya kuomba viza.

Waomba viza vile vile wataombwa kueleza ikiwa waliwahi kufukuzwa kutoka Marekani, au iwapo kuna mtu aliye na uhusiano nao ambaye aliwahi kuhusika katika vitendo vya kigaidi.

Nchi kama Ujerumani, Ufaransa na Uingereza, ambazo raia wake hawahitaji viza kuingia Marekani, hazitahusishwa katika utaratibu huo mpya, lakini China na India ni miongoni mwa nchi zinazolengwa.
Mpango kwa sasa ni canada wazee..achaneni na hii Nchi inayojiona pepo. Nendeni mkapigwe baridi ya Canada na chance ya kubakia huko ni rahisi sana. I recommend Canada/Australia than USA
 
Mbona kupata visa ya UK ni ngumu kupata kuliko US?
Kwa kuanza life zote ni ngumu kwa kweli Mimi nilipokua naanza mambo ya safari sijawahi kufikiri kwenda katika balozi zao nilizipita tuu ila nilipotoka Nje ya Nchi ilikua rahisi kwenda na kupata Visa zao hao wote bila usumbufu...Sasa hivi ni bora kuanzia life Australia, Asia huko USA wanadundisha sana vijana
 
Street life maana ya Visa ni kigezo anachopata mgeni kuingia Nchi husika sasa zipo aina Mbili za Visa kuna visa anapata mgeni anapoingia iwe border au airport na aina ingine ya visa ni kuiomba kabla haujasafiri ukiwa katika Nchi yako kwa ubalozi wa Nchi unayotaka kwenda kwa maana hiyo hizo Nchi zilizotajwa hawapewi hizo visa zote na wanaingia? Nchi ambazo hawatumii visa ni leseni ya udereva au kitambulisho cha kazi ni Scandinavian country ni muda wanafanya hivyo kwa kuzuia ugaidi Nchi karibu zote USA lazima wapate VISA...
Visa on arrival.
 
Trump anashindwa kusoma alama za nyakati.magaidi skuizi wanatumia raia Wa ndani ya nchi husika.a.k.a homegrown terrorists.hizi sheria anazoweka tutakao umia ni sie walalahoi.
 
Back
Top Bottom