Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Marekani itatuma vifaru na magari ya kivita pamoja na wanajeshi 3,000 nchini Poland kuanzia Alhamisi.
Wanajeshi hao watapelekezwa taifa hilo la Ulaya kama sehemu ya hatua za Rais Barack Obama kuwahakikishia washirika wake katika muungano wa kujihami wa nchi za Magharibi (Nato) kwamba imejitolea kukabiliana na tishio kutoka kwa Urusi.
Kuwasili kwa wanajeshi hao kunajiri siku chache kabla ya kuapishwa kwa Donald Trump kuwa rais mpya.
Bw Trump ameashiria kwamba anataka uhusiano kati ya Marekani na Urusi uimarike.
Operesheni ya sasa ndiyo kubwa zaidi kwa Marekani kupeleka wanajeshi Ulaya katika kipindi cha miongo kadha.
Tayari zaidi ya vifaru 80 na mamia ya magari ya kivita vimewasilishwa Ujerumani na sasa vinasafirishwa hadi mashariki mwa Ulaya kwa barabara na reli.
Wanajeshi wa Marekani watashiriki mazoezi ya kijeshi katika mataifa ya bahari ya Baltic.
Hii inatazamwa na wengi kama hatua ya Rais Obama kujibu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine na kuwahakikishia washirika wake Nato.
Mpango wa sasa ni wa kuwabadilisha wanajeshi watakaokuwa huko kila baada ya miezi tisa.
Kuchaguliwa kwa Donald Trump hata hivyo kumeibua maswali kuhusu iwapo mpango wa sasa wa jeshi la Marekani utaendelea.
Waziri wa ulinzi aliyependekezwa na Bw Trump, Jenerali James Mattis, huenda akaulizwa kuhusu mtazamo wa utawala wa Trump kwa urusi atakapokuwa anahojiwa na kamati ya ya bunge la Seneti baadaye Alhamisi.
Chanzo: BBC