X-PASTER
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 11,604
- 1,857
Marekani Kutoa msaada wa Kijeshi Somalia
Afisa mmoja mwandamizi katika jeshi la Marekani, Generali William Ward, amesema Marekani itaisaidia serikali ya Somalia, kuthibiti mji mkuu wa Mogadishu.
Akiongea mjini Washington, Ward, ambaye ni kamanda mkuu wa jeshi la Marekani barani Afrika, amesema oparesheni ya kutwaa uthibiti wa mji huo kutoka kwa makundi ya wanamgambo wa kiislamu inaendelea, lakini hakusema ni msaada upi marekani inatoa.
Rais wa serikali ya Mpito ya Somalia, Sheikh Sharif Ahmed ameukaribisha msaada huo wa Marekani. Wiki iliyopita Gazeti la New York Times liliripoti kuwa kikosi maalum cha Marekani kitashiriki katika oparesheni ya kuwasaka wapiganaji wa kiislamu mjini Mogadishi wiki chache zijazo.