Marekani kutoa kipigo zaidi kwa Iran

Marekani kutoa kipigo zaidi kwa Iran

Bikis

Member
Joined
Feb 23, 2019
Posts
52
Reaction score
74
Juhudi za kimataifa zinaanza huku Rais Donald Trump wa Marekani, ambaye binafsi aliagiza mauaji hayo ya Jenerali Soleimani, akiitishia Iran kwamba nchi yake itavishambulia vituo muhimu 52 kwa Iran endapo Jamhuri hiyo ya Kiislamu itaamuwa kulipiza kisasi.

Akitumia jukwaa lake maarufu la mtandao wa Twitter, Trump ameandika kwamba Marekani itajibu "kwa haraka na kwa nguvu sana", ikiwa Iran itachukuwa hatua za kulipiza kisasi.

Msururu huo wa twita za vitisho ulitanguliwa na Ikulu ya Marekani kuwasilisha rasmi mbele ya baraza la Congress ilani ya mashambulizi ya ndege isiyo rubani yaliyomuuwa Jenerali Soleimani.

Sheria za Marekani zinataka bunge lifahamishwe ndani ya kipindi cha saa 48 pale jeshi la Marekani linapotumwa kwenye mzozo unaohusisha silaha au hali inayoweza kupelekea vita.

Wachambuzi wengi wanasema kuwa kimsingi tayari Marekani imetangaza vita dhidi ya Iran, na iliyobakia ni juu ya Iran kama itaingia vitani au la.
 
.
255747488737_status_0045163a629241978478f4e813e043f2.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naam mtanange ndio hivyo umetangazwa na Marekani. Karibuni uwanjani Iran. Anzeni japo kwa kurusha kipande cha kokoto Tel Aviv muone moto ambao hamjawahi kuushuhudia na ambao hautasahaulika miongoni mwa vizazi vyenu milele.
 
They attacked us, & we hit back. If they attack again, which I would strongly advise them not to do, we will hit them harder than they have ever been hit before!
 
Naam mtanange ndio hivyo umetangazwa na Marekani. Karibuni uwanjani Iran. Anzeni japo kwa kurusha kipande cha kokoto Tel Aviv muone moto ambao hamjawahi kuushuhudia na ambao hautasahaulika miongoni mwa vizazi vyenu milele.

Hezbollah atabidhiwa ku deal na israel.
 
tayari website za marekani zimeanza kuhackiwa
 
Nina wahurumia Sana raia wa mataifa yenye vituo vya marekani maana Iran itayaharibu vibaya sana muda sio mrefu tutaanza kupokea wakimbizi kutoka Saudia, Dubai,Qtaar,kuwait,yaan matoto ya kiarabu yatasambaa hapo posta nakwambia unajichagulia inalo liona linafaa unalivutia ndani.
 
Back
Top Bottom