Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,618
- 9,611
Rais Donald Trump wa Marekani ametangaza kuwa Marekani itajitoa kwenye makubaliano ya kimataifa kuhusu biashara ya silaha ATT uliosainiwa na serikali ya Obama.
Rais Trump ametoa taarifa hiyo wakati akihudhuria mkutano wa Chama cha wamiliki silaha cha Marekani NRA, na kusisitiza kuwa Marekani itajitoa kwenye makubaliano hayo yanayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.
Makubaliano hayo yanasimamia biashara ya kimataifa ya silaha ndogo ndogo na ndege. Uliidhinishwa na Umoja wa Mataifa na kusainiwa na serikali ya Obama, lakini baraza la seneti la Marekani bado halijaidhinisha mkataba huo.
Ikulu ya Marekani imesema makubaliano hayo yanazuia uwezo wa Marekani kuuza silaha kwa washirika na wadau wake.
Hata hivyo hatua hiyo mpya ya Rais Trump imekosolewa na baadhi ya mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu.