Marekani: Iran inafanya uchokozi wa hali ya juu

Marekani: Iran inafanya uchokozi wa hali ya juu

Kapepo

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2015
Posts
1,078
Reaction score
1,227
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson ameituhumu Iran kwa kufanya "uchokozi wa hali ya juu" unaoendelea ambao amesema unanuia kuvuruga uthabiti katika Mashariki ya Kati na kuhujumu juhudi za Marekani katika kanda hiyo.

"Iran isipochukuliwa hatua inaweza kwenda njia sawa na ya Korea Kaskazini na kuubeba ulimwengu wote katika safari hiyo," Bw Tillerson amesema.

Rais Donald Trump tayari ameagiza utathmini mpya ufanywe kuhusu mkataba uliotiwa saini kati ya nchi za Magharibi kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.

Hata hivyo, Marekani imekiri kwamba Tehran inatii makubaliano hayo ya mwaka 2015.

Marekani: Korea Kaskazini ilikusudia uchokoziKorea Kaskazini: Tutaishambulia Marekani kwa nyuklia

Iran kufikia sasa haijasema lolote kuhusu tamko hilo jipya kutoka kwa Marekani.

Iran imekanusha mara kwa mara tuhuma kutoka kwa nchi za Magharibi kwamba inajaribu kustawisha silaha za nyuklia.

Jumanne, Marekani iliituhumu Korea Kaskazini na kusema taifa hilo lilikuwa linajaribu kufanya "uchokozi kutokee jambo fulani", baada ya nchi hiyo kufanya jaribio la kombora ambalo lilifeli mwishoni mwa wiki.

Kuijibu Marekani, Korea Kaskazini ilisema inaweza kuwa ikifanya majaribio ya makombora kila wiki.

Aidha, ilionya kwamba itaikabili Marekani kwa vita vikali iwapo taifa hilo litathubutu kuishambulia kijeshi.

'Vitisho vingi'

Jumatano, Bw Tillerson alsiema utathmini huo mpya kuhusu Iran, ambao aliutangaza katika Bungela Congress siku moja awali, kando na kutathmini iwapo Tehran imetimiza makubaliano ya mkataba huo wa nyuklia pia utachunguza vitendo vya Iran Mashariki ya Kati.

Marekani yaionya vikali Korea Kaskazini

Bw Tillerson aliituhumu Iran kwa kuhujumu juhudi za Marekani nchini Lebanon, Iraq, Syria na Yemen.

"Mpango wa kina wa sera kuhusu Iran unatuhitaji tuangazie vitisho hivi vinavyoletwa na Iran, na ni wazi kwamba ni vingi (vitisho)," alisema

Bw Tillerson awali alikiri kwamba Iran ilikuwa imeheshimu makubaliano ya mkataba huo wa 2015, lakini aliibua wasiwasi kuhusu taifa hilo akisema limeendelea kuwa "mfadhili wa ugaidi".

Rais Trump kwa muda mrefu amekuwa akisema mkataba huo kuhusu Iran "ndio mbaya zaidi kuwahi kutiwa saini".

Manowari za Marekani hazikuelekea Korea Kaskazini

Hata hivyo, mtangulizi wake Barack Obama alisema mkataba huo, kati ya Iran na mataifa sita yenye ushawishi duniani zikiwemo China, urusi na Uingereza, ilikuwa ndiyo njia bora zaidi ya kuizuia Iran kustawisha silaha za nyuklia.
 
Kilichomfanya US kuogopa kushambulia Korea kaskazini ndio kinafanya Marekani kuogopa kushambulia Iran.

Iran na North Korea ndio sehemu ambazo zinaitaji maamuzi magumu ya nchi za Ulaya na America kuyafanya, na maamuzi hayo yatawaacha na hasara kubwa sana kuanzia kiuchumi, kibiashara ,Usalama na Kijamii

Maeneo makubwa sana na yanaoendesha uchumi wa Ulaya na America ni maeneo miwili tu
1Asia Pacific
ambapo kwa mwaka unazunguka uchumi wa 17.1566 Tillion usd

2 Middle East
middle east ni eneo muhimu sana kibiashara na uwekezaji mkubwa sana wa makapuni ya mafuta na Gas kutoka nchi za Ulaya na America pia tunatakiwa kujua 70%ya Energy ambayo inarun mitambo na vifaa inatoka middle east ambayo ni (mafuta na Gas).
Katika nchi zote 17 za Middle East kuna nchi ndugu na kipenzi cha wazungu(Israel) pia kuna nchi washirika wakubwa wa biashara na wazungu (Saudi arabia,kuwait,UAE) kama vile ilivyo kwa South Korea na Japan eneo la Asia Pacific pia Iran si mwarabu japo yupo sehemu ya waarabu ni kama Israel si mwarabu ni Mchanganyiko wa Waisrael pure na mizungu so Iran hato kuwa na huruma kwa waarabu vibaraka wa wazungu atatifua eneo lote la Middle East
 
Duh! Sasa Mbona Haeleweki Mara NK Mara Iran......Iran inachotakiwa kufanya nikuhakikisha inapata Nuclear war heads and Hydrogen Bomb otherwise US/NATO/Israel na SAUD ARABs wanahasira nae sana maana hawa waPersia ni wabishi balaa na mbaya zaidi wanakua Kiteknolojia jambo ambalo US hapendi....
 
USA ndiye "malaika mtoa roho" katika hii Dunia, maana pote yeye ni mleta vita na mauti.

Hafai kabisa.
 
Akimgusa Iran, wakina Urusi, Korea Kaskazini, China na Uturuki watanuna na hawatakubali hivyo watapiga Marekani, Israel na Saudi arabia
 
Back
Top Bottom