Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 10,488
- 16,646
Kifo katika maisha ya dunia ni kitu cha lazima ambacho humpata kila kiumbe bila uchaguzi.Wako wanaokufa wachanga,wazee na wakongwe.
Vifo navyo hutofautiana kutokana kwa namna nyingi sana.Kilicho maarufu ni kuwa vifo vya watu waovu mara nyingi huambatana na kutapatapa sana muda unapokaribia na wakati wa kifo chenyewe.
Marekani si miongoni mwa tawala kongwe katika historia ya dunia lakini katika umri wake mfupi limeshiriki kwenye kutenda maovu mengi ndio maana muda wake wa kifo unavyokaribia imekuwa ikitapatapa mno.Matarajio ni kuwa hali yake hiyo ni mpango wa Allah kuwadhihirishia waja wake kuwa hakuna aliye mkuu na mwenye nguvu kuliko yeye.
Kwa sasa taifa hilo kila linapoelekea ni balaa kwake.Kutoka hawapendi wakaonekana ni wadogo na kubaki kwao ndani ya mizozo hiyo ndio kunawamaliza nguvu kwa kasi mno.
Kwa mujibu wa Jerusalem post Marekani kwa sasa inaweka kwenye mezani ni kilichobora kati ya kufunga kambi zake za kijeshi zilizosambaa duniani kuelekeza nguvu maneneo ya Asia karibu na China na Urusi.
Wameshaanza kuondoka kinamna mashariki ya kati lakini kuondoka moja kwa moja wanasema watawapa nguvu magaidi pamoja na Iran kuchukua madaraka.Kitendo hicho kitapelekea kufa kwa Israel ambayo wamekuwa wakiilinda kwa hali na mali.Kubaki kwake imekuwa ni gharama kubwa sana wakati uchumi umeyumba sana.
Kutapatapa kwa Marekani mashariki ya kati kumedhihiri kwa kulazimika kwake kufanya makubaliano mpaka na kikosi cha wanamgambo maskini wa Haouth ili kusitisha vita baina yao.Vile vile katika kulazimisha kusitishwa vita vya siku 12 vya Israel na Iran ambapo yenyewe ilikuwa ikiisaidia Israel.
Ili kuokoa pesa na kukuza uchumi wake raisi Trump ameingia vitani vya kibiashara na mataifa karibu yote ya dunia mpaka mataifa marafiki.Washauri wa kiuchumi wamegundua hatua hizo hazileti nafuu ila kuzidisha shinikizo la kiuchumi ndani ya nchi.
Tukija upande wa vita vya Ukraine na Urusi.Kiukweli Marekani imeishiwa na cha kuwasaidia waukraine washinde vita na Urusi.Kuondoka hawawezi wanaona wataaibika na kuonekana wao ni wadogo.Kubaki kwake ndio ni balaa zaidi kwani uchumi na silaha vimeisha.
Matendo yote ya Marekani kwa sasa ni kutapatapa katika kifo.Trump ambaye ndiye kiongozi kwa kipindi hiki amekuwa na hasira na ugomvi na kila mtu mpaka washauri wake wa ndani.