Marekani Ina agenda ya siri na CCM 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Marekani Ina agenda ya siri na CCM 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JOHN MADIBA, Jun 24, 2011.

 1. JOHN MADIBA

  JOHN MADIBA JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2011
  Joined: Jan 30, 2011
  Messages: 251
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tuanza na hili, Richmond(rushwa)-----Dowan(rushwa)-----Symbolic power( AGENDA 2015)= Marekani kutukuza rushwa kwa kukubali mitambo hiyo inunuliwe na kampuni kutoka nchini mwao. Na kubariki ununuzi huo na waziri wao wa mambo ya nje H.Clinton kutembelea mitambo hiyo.turudi nyuma kidogo mitamboo hiyo ilisababisha waziri mkuu wa tanzania akajiuzulu na alipojiuzulu haikupita muda mrefu rais wa marekani G.bush aliitembelea Tanzania na kusifu hatua kubwa iliyofanywa na serikali ya Tanzania katika kupiga vita Rushwa.
  Wamarekani wana agenda ya siri na CHAMA CHA MAFISADI,

  1.Ndio wakatafuta kampuni inunue mitambo hiyo na waziri wao H.Clinton akaitembelea
  2. Wakavinyamazisha wanasiasa wote waache kuiongelea mitambo hio. Hata wale waliokinara wakiisema ichukuliwe na serkali wako kimya kama maji kwenye mtungi.
  3.Wakaipigia Tanzania kampeni (debe) ndani ya umoja wa mataifa ili ipewe tunzo ya huduma bora katika sekta ya umma, Huu ni uwendawazimu, Walimu hawalipwi pesa zao polisi wanalalamika wanaishi kwenye mbavu za mbwa, Manesi madaktari nao wanamadai yao hawajatimiziwa lakini bado Marekani ikashawishi Tanzania ipewe tunzo hiyo wakati Republic of South africa kwa Zuma walikua wanasifa zakutuzidi kupew tunzo hiyo.
  4. Na kuna taarifa zisizo rasmi Obama ataitembelea Tanzania kabla 2015. anatafuta nini Clinton alikuja, Bush alikuja, OBAMA???? naye kuna nini Tanzania, kama ni misaada pia huko somalia, ethiopia wanashida kupita hizi tulizonazo.
  5. Tujiulize KWANINI TANZANI wanataka nini hapa, Agenda yao ni 2015.
  JE UNAFAHAMU NINI WANACHOTAKA????,,,,,,, KWANINI 2015??????
   
 2. sblandes

  sblandes JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2011
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,457
  Likes Received: 788
  Trophy Points: 280
  Mkuu mjenga nchi ni mwananchi,na mvunja nchi ni mwananchi,kama serikali ikiwa makini katika maamuzi yake na maslahi yake kwa wananchi wake haitakiwi kuogopa kushirikiana na nchi nyingine ikiwemo Marekani.Hakuna sababu ya kumwogopa USA kinachotakiwa ni umakini wa ushirikiano katika nyanja mbali mbali zenye maslahi ya Taifa letu kwa watu wetu.
   
 3. Tutafika

  Tutafika JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2011
  Joined: Nov 4, 2009
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 160
  uranium, tanzanite, petrol (ipo usibishe!), new kigamboni city, dar free trade area kama ilivyo dubai!,

  kwani hujui symbion inaongozwa na majasusi?, umeme watazalisha ila ni kwa ajili ya miiradi yao hiyo! tushauzwa zamaniiii.
   
 4. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #4
  Jun 24, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Hofu yangu ni hapo kwenye red.
   
 5. Avatar

  Avatar JF Gold Member

  #5
  Jun 24, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 676
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 35
  Sidhani kama tunahitaji kutafakari sana juu ya hili, United Republic of Tanzania tulikua na uhusiano mzuri na United States since kipindi cha J. K. Nyerere & j. F. Kennedy kuliko hao ulio wataja.
  Hii tabia ya kuconnect kila tukio na 2015 mimi yananishangaza sana... Nnauhakika United States watakua na agenda yao juu yetu kama ambavyo nasi tuna agenda juu yao. Alafu, sijalijua lengo lako, unataka US wasitupe misaada au??
   
 6. MGAWARIZIKI

  MGAWARIZIKI JF-Expert Member

  #6
  Jun 24, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 306
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni kweli lakini si viongozi wa serikali yetu ni waoga sana na wanapenda kunyenyekea na kutukuza nchi tajiri eti kisa watanyimwa misaada
   
 7. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #7
  Jun 24, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,437
  Likes Received: 19,789
  Trophy Points: 280
  [​IMG][​IMG]
   
 8. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #8
  Jun 24, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  nambie ajenda yetu juu yao
   
 9. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #9
  Jun 24, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Sio uongo Obama atatinga Tanzania muda si mrefu kwa sababu ya kwenda kutambika kwao japo kwa masaa. Sio kwamba hii serikali ni makini bali wamepata Fisadi papa JK ambaye anaangalia tumbo lake tu.
   
 10. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #10
  Jun 24, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Marekani ni rafiki wa Watanzania toka miaka hiyo ya Mwalimu [Keneddy na Jimmy Carter],urafki wa miaka hiyo ulikua full heshima,japo TANZANIA enzi hizo TAIFA changa ukilinganisha na Marekani.Watanzania kwenye urafiki wa zama hizo uliegemea zaidi kwa wamerekani kutambua zaidi uwezo wa wabongo [Watanzania] katika ubongo wao. Yani nikimaanisha uelewa wa falasafa nzima ya maisha ya Mwafrika katika bara la Afrika.Tuliongoza mapambano ya ukombozi wa bara la Afrika na kusaidia mataifa yale yaliyokua hayana sauti kusikika.Tanzania na udogo wake huo ilipigania China zama hizo kwenye balaza la usalama la umoja wa mataifa.


  Mwalimu anasema Mtanzania kama akitokea kuwakilisha nchi kwenye vikao vya kimataifa na ukafika wakti wa yeye kuzungumza basi hata mtu wa Taifa jingine aliyekua akifikilia kutoka kwenda kuvuta sigara,alikua anasitisha utokaji wake huo ili apate kusikiliza mtanzania huyo anatasema nini.Yaaani kwa Lugha ya DOTCOM GENERATION tunasema watanzania wa enzi hizo walikuwa wanawakilisha.[yaaani wanabamba].

  Kwa Picha hiyo marekani walikuwa na mapokeo tofauti sana dhidi ya TAIFA hili na hasa msimamo wa kiongozi wake hayati Mwalimu Julius K Nyerere akiwakilisha TAIFA kama kioo cha TAIFA changa la Watanzania, lenye msimamo wake usioegemea upande wowote na usiochaguliwa marafiki na kusimamia bila kuyumba msimamo wao wanaoamini ni faida kwa watanzania na haki kwa binadamu yoyote chini ya uso wa dunia hii.

  Wamarekani ni wadadisi sana na watundu wenye uwezo wa kucheza na akili za binadamu wenzao kwa umakini mkubwa na wenye kuitaji ujuzi na ufahamu mkubwa sana.

  Kupitia Mwalimu TAIFA lilikua na uwezo wa kujibu na kusimamia mbinu na maarifa yote ya TAIFA hilo kubwa dunia na hivyo basi kulifikisha mahari TAIFA hilo kubwa kupata kigugumizi cha kulitumia na hivyo TAIFA hilo kuwa na msimamo wa kuligeuza TAIFA hili enzi hizo TIAFA changa kuwa TAIFA rafiki wake.[Chini ya ule msimamo wao maarufu wa IF YOU CANT DEFEAT THEM JOIN THEM].

  Kujoin huko kumezaa mbinu, maarifa ambayo leo hii,tunasema ni kilio.Tumesahau misimamo, mbinu,maarifa na ubunifu wa kupambana na changamoto za kutoka kwenye TAIFA hilo kubwa.Hatuna waumiza vichwa wa kuoji maaamuzi ya TAIFA hilo kubwa ukizingatia sera ya daima ya TIAFA hilo kua HALINA MAADUI WALA MARAFIKI WA DAIMA ILA LINA LINA MARAFIKI WA INTEREST ZAKE.

  Sipingi sera za marekani kwa kuwa ni TAIFA huru lenye maamuzi yake,napingana na viongozi wetu wenye kumeza kila jambo wakasahu mbinu na maarifa aliyotumia mwalimu kuishi na TAIFA HILI kubwa duniani.Hatuwezi tukapingana kutokushirikiana na TAIFA hili lakini tuludi kwenye zama za Mwalimu aliwezaje kuishi na watu hawa na bado akaheshimika kwao pasipo kuwapa kitu,si madini wala mali ya asili au chochote.

  Please TAIFA hilo lipo nchini na lina investment zake hapa lakini viongozi wetu mnaitaji ubongo wenye kuchemka kuludisha heshima ya TANZANIA.Nawapenda wamerekani kwa utamaduni wao wa uwazi uliopitiliza tena wenye kutukuka.Wakati mwingine najiuliza mwalimu na udogo wa TAIFA lake lakini nae bado alichagua kuambatana na hawa jamaa,nilichojifunza ni kuwa Mwalimu nae pia alitumia kujifunza mambo mengi sana kupitia TAIFA hili. Na kwa kuwa lilikua na TAIFA linaloheshimika pamoja na udogo wetu tuliambatana kama watu tunaolingana.

  Wamarekani wana misemo yao kama ile ya USE AND ABUSE,hivyo michezo yao ya kisiasa wanaicheza mpaka kwa viongozi wao wa ndani billa shaka hivyo siwezi kuwaita ni waonevu pale wanapowachezea viongozi wetu.Wamarekani wanataka daima watu wenye fikra mpya za kuleta maono ya dunia mpya kila wakati na kila siku.Ndio maana wanatafuta taarifa nyingi sana kila siku dunia kote. Vitendo vya viongozi wetu kutumika wakifikilia marekani atakua mtetezi wao HILO WASAHAU KAMWE HALIPO.

  Marekani watakupa deal kupima uwezo wako ukilipokea na kushindwa kutadhimini na kuchuja walichokupa wakiwa wamekupa vigezo vyote vya wewe kusimamia kile unachoona amini na ni faida kwako ama kwa nchi yako nawe ukaingiza personal interest mwisho wa yote ,watakutunzia siri kwa muda mchache [ten to fifteen years] wanakumwaga mbele ya hadhara ili jamii yako ione madudu uliyoyafanya na watambue ukweli.

  Kupitia USE AND ABUSE Marekani imeendelea kuwa strong National na TAIFA lenye kusaidia demokrasia haswa mataifa yenye viongozi wabovu na wenye upeo mdogo wa kupokea na kutambua mambo yanayohusu falasafa nzima ya maana ya MAISHA ya wanachi wao na ustawi wa MATAIFA yao.

  Ni kipi bora kwa kiongozi kufa na kuacha alama ya kumbukumbu bora ya vizazi kwa vizazi vikilitaja jina lako kama alama ya uzalendo kwa TAIFA na mtu uliyetoa mchango wa maisha bora kwa binadamu wenzio hapa duniani kama [Mwalimu Nyerere au Kite Masile aliye bado hai] au kukumbukwa kama kiongozi uliyetumia mali za umma kuangamiza maisha ya raia wa TAIFA lako kwa starehe kama Mobutu na watawala madikiteta wengine.

  Tunaitaji turudi kwa Mwalimu alipotuacha,Marekani si tatizo tatizo ni viongozi wetu,manake uwezi kuitaji uongozi kwa nia ya kumilki mali na watu.Wamarekani uongozi ni unataka kuifanyia nini marekani na watu wake.

  Nikitizama watu kama Tindu Lissu, Zito Kabwe na hata Simbachawene,hawa ni wa chache kati ya mamilioni ya vijana wa kitanzania,ambao kama tungepata makundi kwa makundi yakasomeshwa kadi mabalimbali marekani mika mitano ni mingi sana Tanzania kuwa nyuma ya Mataifa ya Tiger Countries
   
 11. JOHN MADIBA

  JOHN MADIBA JF-Expert Member

  #11
  Jun 25, 2011
  Joined: Jan 30, 2011
  Messages: 251
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  CCM wakipokea tuzo kutoka umoja wa mataifa UN
   
 12. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #12
  Jun 25, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,673
  Trophy Points: 280
  Wewe ndo unajua leo?Pole sana ndugu!
   
 13. b

  bob nasta Member

  #13
  Jun 25, 2011
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 69
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 25
  Eee bwana ee DSN we ni noma mi nazani katika hao vijana uliowataja na wewe nakuongezea
  japo sijui age yako
  Napenda sana ninapoona kuna watu wanauwezo wa kuona mbali
  kama hivi [blavo]
   
 14. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #14
  Jun 25, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Sasa nagundua kuwa sihitaji kuwachukia sana Wamarekani ila viongozi wangu kwa uwezo wao katika maamuzi na wamarekani. Ingawa nao wanatumia mwanya wa viongozi dhaifu kutudhurumu/kutuibia malizetu.
   
 15. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #15
  Jun 26, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Viongozi wetu ndio tatizo, ndugu Lincolmtza, kiongozi wetu anakuwa mtawala [aka kiongozi] mpaka anatoka madalakani ajaandika kitabu chochote kinachozungumzia maisha yake na utendaji wake wa kazi kwa siku zote alivyokuwa madalakani,tena kwa lugha ya kiswahili na vikatumika mashuleni kuwafandishia vijana wetu huko shule za msingi na sekondali mpaka vyuo kuona ni namna zipi viongozi wetu walitumia maamuzi yao na utendaji wao kubolesha maisha ya watanzania na binadamu wote kwa ujamla.

  Mfano mama Hilaly Rodham Clinton katika kitabu chake cha LIVING HISTORY ukulasa wa 403 anawaambia wamarekani wenzie na dunia nzima kwa ujumla kupitia kitabu chake ni jinsi gani ziala yake Afrika alichojifunza na ushauri aliotoa kwa viongozi wetu Tanzania.

  anasema '' I left Harare feeling dispirited at the deterioration of services and facilities and the manefest failures of a leader who had stayed too long in power.But my spirits lifted at our next stop,Victoria Falls,.......................................................................................................
  Africa's breathtaking beauty and natural resources must be protected while econmic opportunities for people expand.But ithat is no simple challenge,as I learned during my visit to Tanzania, a sprawling East Africa country formed in 1964 from two former colonies whose names entranced me as a child [she was born in 26: October 1947].Tanganyika and Zanzibar.In the capital,Dar es salaam,I met President Benjamin Mkapa,a cheerful former journalist who had worked hard to develop a national economy that benefited from the country's natural resources and strategic location on the Indian Ocean.With the vigorous assent of his wife,Anna Mkapa,and the women ministers in attendance at our meeting,I encouraged the President to eliminate laws that not only were unfair but hobbled the economic potential of half the country's population.In 1999,Tanzania passesd the Land Law Act and the Village Act,repealing and replacing the laws that had previsouly discriminated against women.

  Kazi hipo.

  Tanzania is also a crucial actor in bringing peace and stability to war-torn cenntral Africa......

  Je Kama Mtanzania tutapata wapi ufahamu wa kujua viongozi wetu wakikutana na Viongozi wa Mataifa wengine wanawaambia nini na kupokea ushauri gani.Ili kesho na keshokutwa vijana wa leo wapite kwenye mstari safi wa maamuzi kama ambao mama huyu wa kimalekani yeye kaweka kumbukumbu tayari kwenye kitabu mmarekani yoyote mwenye kujua kusoma kiingeleza ambayo kwao ndio lugha ya Taifa atajua mama huyo alifanya nini kwa niaba ya Taifa lake ndani ya Taifa la Tanzania.

  Kiasi kuwa Kajivuniia Mabadiliko ya sheria ya Ardhi nchini Tanzania ni bidii ya ushawishi wake hivyo kuthibitisha anauwezo wa kusababisha,na hiyo ni sifa kubwa ya kiongozi wa Taifa la Marekani daima.
   
 16. u

  ureni JF-Expert Member

  #16
  Jun 26, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,272
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  I hate that word tumeshalemaa na misaada.
   
Loading...