Marekani imejiondoa rasmi kutoka kwa mkataba wa Paris wa kupambana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,504
9,284
Marekani imejiondoa rasmi kutoka kwa mkataba wa Paris wa kupambana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

Hatua hiyo inatimiza ahadi ya Rais Donald Trump ya kuiondoa Marekani ambayo ndio mchafuzi mkubwa wa hewa kote duniani, kutoka kwa mkataba huo.

Hata hivyo, aliyekuwa Makamu wa Rais Joe Biden, ameahidi kurejesha Marekani kwenye mkataba huo, endapo atashinda Uchaguzi Mkuu, ambao matokeo yake bado yanasubiriwa.

Rais Donald Trump alitangaza nia ya kuindoa Marekani kutoka mkataba huo, June 2017, kwa madai kwamba unaathiri uchumi wa Marekani.

Marekani inakuwa nchi pekee kati ya wanachama 197 kujitoa kwenye mkataba huo wa kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa ulioundwa mwaka 2015.

Uingereza, Ufaransa, Chile na Italy, zimesema kwamba hatua ya Marekani ni ya kusikitisha.
 
Safi sana D.Trump lkn nina wasiwasi kama huyo mzee mgonjwa Biden akiingia atairudisha USA kwenye huo mkataba wa kinyonyaji, ...
 
Kila inachokifanya USA ni kwa maslahi yake tu not otherwise.

Ukiona kelele zao zimezidi mahali jua ni maslahi yao yameguswa.

Sasa kuna wajinga wanafikiri wanapendwa wao au USA inapenda haki.

USA imewapiga ban maafisa wa ICC kisa tu wanachunguza uhalifu dhidi ya binadamu uliofanywa na vikosi vyao huko middle East.
 
Kwahiyo mkuu unataka kusema hata haya matamko tamko wanayotoa kuhusiana na uchaguzi wetu Tz ni kwamba si kwamba hufanya hivyo kwa sababu wanapenda demokrasia na kuona haki ikitendeka?
 
Back
Top Bottom