marekani haijasaini mkataba wa icc

marekani haijasaini mkataba wa icc

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,255
Reaction score
64,840
Nashangaa viongozi wa kiafrica wanavyo lalamika kwamba ICC hawawakamati wazungu wanang'ang'ania viongozi wa afrika so wameamua kujilinda. Mimi sikubaliani nao kwa sababu1. marekani wanayoisema haijawahi kukubali mkataba wa roma kuhusu ICC.2. Afrika demokrasia haijakua na kuna unyanyasaji wa kitu kuliko sehemu yoyote duniani3. afrika ndio kuna mapinduzi ya kijeshi na marais kung'ang'ania madarakani.5. Marais wa afrika hawajaanzisha mahakama nyingine mbadala ya ICC. Naomba mchango wako. mia
 
Sasa hivi tony Blair anachunguzwa nchini mwake juu ya vita ya iraq kwa sababu ile vita haikua na baraka za UN. Lakini bush hachunguzwi sababu Nchi yake kutokusaini mkataba wa roma kuhusu ICC.ili Viongozi wa afrika wapone ni lazima kwanza waanzishe mahakama ya afrika inayo fanya kazi kama the hegue kama walivyo anzisha kuhusu mauaji ya halaiki ya rwanda ambapo mahakama yake ipo arusha. so wanatakiwa waanzishe mahakama yenye kazi kama ICC kwa ajili ya afrika ndo walaumu. mia
 
merekani haikusaini mkataba ule ila wenyewe ukiwaona wanavyoshurutisha viongozi wa kiafrika wakamatwe utadhani wenyewe ndio wenye hiyo ICC.
 
ndiyo, marekani haijasaini mkataba wa Roma wa icc, lakini that does not bar their leaders from prosecution kama wakifanya makosa. ndio maana hata al bashir wa sudan nchi yake haijasaini mkataba lakini alitolewa arrest warrant. niongee tu hivyo kwa kifupi.
 
Ma-VIONGOZI ya KIAFRIKA ni MAPOYOYO tu, hata sijui huko AU Addis Ababa sijui huwa yanaongea nini?

Leo Museveni hataki Uhuru Kenyatta aende ICC, lakini ni Museveni huyo huyo aliyemwambia Al Bashiri Rais wa Sudan kwamba akikanyaga tu Uganda anamkamata na kumpeleka ICC kwasababu kwanza Uganda ni Mwanachama wa ICC na lazima itekeleze amri ya ICC.

Sasa haya Mapoyoyo ya KIAFRIKA (SIC!) yatakwambia nini? Kama yalikuwa hayaitaki ICC si yasingekuwa mwanachama kama USA na Israel.

Tukubali WAAFRIKA tuna matatizo tena makubwa sana.
 
WAKUU mbona ziara ya OBAMA kuja tanzania haijatangazwa kama ya rais wa china, ccm wamekubali kuiachia hiyo promo ama kweli mchina katukamata sawaswa watanzania chezea rushwaaaaaaaaaaaaaaaaaaeee.Obama kuja kimya kimya!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
merekani haikusaini mkataba ule ila wenyewe ukiwaona wanavyoshurutisha viongozi wa kiafrika wakamatwe utadhani wenyewe ndio wenye hiyo ICC.

hata afrika nchi ambazo hazijasaini viongozi hawakatwi wanasubiria hadi aingie kwenye nchi iliyo sighn ndo akamatwe. kipindi kile bush kaja afrika ilibidi akamatwe tatizo icc haijatoa kibali cha kukamatwa kwa bush.
Lakini viongozi wa afrika wamezidi kutofuata haki. kama kikwete inabidi apelekwe icc. mia
 
hivi bila ICC haya maandamano ya chadema si wangekuwa wanawafyatulia risasi na kuwaua waandamanaji wote? ICC ipo lakini wanao andamana tanzania bado wanapigwa risasi na kuuwawa. mia
 
Mie mwenyewe sijawaelewa, walivyokuwa wanasaini walifikiri wanasaini kupewa mikopo?
 
Back
Top Bottom