Marekani: Bunge la seneti laishinda turufu ya Trump

Marekani: Bunge la seneti laishinda turufu ya Trump

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,881
Reaction score
6,378
Rais Donald Trump alipata fedheha katika bunge la seneti Ijumaa baada ya maseneta wa chama chake, Republican, kuwaunga mkono wenzao wa Democratic kuishinda kura ya turufu ya rais kwa mara ya kwanza katika uongozi wake.

Maseneta hao wameupitisha mswada wa sera ya ulinzi ambao Trump alikuwa ameupinga, wiki chache kabla kuondoka madarakani.

Walipokuwa wakikutana katika kikao cha nadra katika siku ya maadhimisho ya mwaka mpya, maseneta 81 dhidi ya 13 wamepiga kura na kupata theluthi mbili inayohitajika ili kuishinda kura hiyo ya turufu.

Kura za turufu zilizopita za Trump ziliungwa mkono na seneti​

Kulingana na sheria za Marekani, kura ya turufu ya rais ya kupinga muswada fulani inaweza kushindwa iwapo muswada unaojadiliwa unaungwa mkono na thuluthi tatu ya wabunge katika mabunge yote ya congress.

Kura nane za turufu za Trump zilizopita ziliungwa mkono na seneti.

Trump alikuwa amekataa kuutia saini na kuufanya kuwa sheria mswada huo wa matumizi ya ulinzi wa dola milioni 740 kwa kuwa ulikuwa haujaondoa sheria kadhaa za kulinda mitandao ya kijamii.

Wabunge wa Republican wapinga kuongezwa malipo kwa Wamarekani​

Sababu yake nyengine ilikuwa kwamba mswada huo ulikuwa na kipengee kinachotoa nafasi ya kubadilishwa kwa majina ya kambi za jeshi, zilizokuwa zimepewa majina ya mejenerali walioongoza vikosi vya muungano wa majimbo ya kusini, yaliyokuwa yanaunga mkono utumwa, wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Wabunge wa Republican pia wamepinga shinikizo la wabunge wa Democratic kuongeza malipo ya misaada kwa Wamarekani kwa ajili ya virusi vya corona kutoka dola 600 hadi dola 2000. Rais Trump pia anaunga mkono nyongeza hiyo ya fedha.

Trump amekuwa haelewani na wabunge wa chama chake cha Republican tangu apoteze uchaguzi wa mwezi Novemba baada ya wengi wao kutomuunga mkono katika madai yake yaisokuwa na ushahidi ya wizi wa kura.
 
Maendeleo hayana chama.

Ingekuwa huku kwetu hao wabunge wangefukuzwa wote.

Kesi za uhujumu uchumi zingeongeka.
 
Back
Top Bottom