Marejesho ya mkopo NMB Bank

gnagna

Member
Sep 9, 2015
36
18
Wadau naombeni ufafanuzi;

Nilichukua mkopo NMB takribani miezi sita iliyopita makubaliano yalikua kukata kiasi cha marejesho kila mwisho wa mwezi lakini cha ajabu wanakata pesa mara mbili kwa mwezi mmoja iyo imekaaje???

Yaani hawakati kwa tarehe inayoeleweka kwa mwezi mmoja mmoja badala yake wana kata mara mbili kwa mwezi mmoja yaani (double). Naomba ufafanuzi kwa mwenye ufahamu zaidi. Kwa sasa niko mbali na hilo tawi nililochukulia mkopo
 
Sasa ufafanuzi gani?, mkataba ulijaza wewe na makubaliano yenu ni baina yenu. Ugumu upo wapi kuwataarifu wafanyacho sio makubaliano yenu?
 
Sasa ufafanuzi gani?, mkataba ulijaza wewe na makubaliano yenu ni baina yenu. Ugumu upo wapi kuwataarifu wafanyacho sio makubaliano yenu?
Yawezekana kuna anayejua kujua mfumo wa marejesho nmb aliyekwisha kupitia hilo atafafanua. Kwa sasa niko mbali na hilo tawi matawi yao mengine hawawezi kutatatua hilo jambo
 
Asanteni wadau niliwatembelea na wamekiri kukata kimakosa na walizokata zitafidia miezi ya mbele.
 
Mimi kesho naenda kuvuta, mkopo wa biashara. Marejesho nitapeleka kwa mujibu wa mkataba
 
Lakini si ndiyo vizuri au?ili uwahi kumaliza deni mimi naona wanakusaidia ili ujitoe kifungoni mapema.

Sina idea na mambo ya mikopo mnisamehe kama nimetoka nje ya mstari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli nawahi kumaliza deni lakini wakiendelea kukata bila utaratibu pia itaathiri mipango yako na budget yako kwa ujumla. Bora utaratibu ufuatwe inampa mteja kupanga budget yake vizuri na wao watachukua wanachostahili kwa wakati sahihi wa makubaliano.
 
Back
Top Bottom