MARANGU: Wafugaji waandamana kupinga kufungwa kwa kiwanda cha maziwa

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
Wafugaji wa ng’ombe wa maziwa katika kata ya Marangu, Mwika wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro wameandamana baada ya kiwanda cha kusindika maziwa,cha Kondiki Dairy Milk kufungwa na mamlaka ya chakula na dawa TFDA na TBS na hivyo kulazimika kumwaga maziwa baada ya kukosa soko.

Wananchi hao wamesema kwa muda wa wiki mbili sasa wamepata hasara ya zaidi ya shilingi milioni 40 kutokana na kukosa soko la maziwa hali ambayo inawalazimu kumwaga maziwa kila siku huku wakishindwa kuhudumia ng’ombe hao wa maziwa kupata chakula.

Wamesema tangu mwaka 2008 wamekuwa wakiuza maziwa katika kiwanda hicho na hivyo kuondokana na umaskini baada ya kupata soko la uhakika tofauti na hapo awali walipokuwa wanauza maziwa nchi jirani ya Kenya.

Mratibu wa maendeleo ya sekta ya maziwa nchini na Mshauri wa kiwanda cha maziwa Kondiki Dk Sadikiel Kimaro amesema wanasikitishwa na hatua ya kufungwa kwa kiwanda hicho na nkwamba mpaka sasa wamepata hasara kubwa kwa kuwa lengo lake ni kumsaidia mkulima mdogo kupata soko la uhakika la maziwa ili kujikwamua na umaskini.
 
Wafugaji wa ng’ombe wa maziwa katika kata ya Marangu, Mwika wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro wameandamana .

Afya kwanza pesa baadae.
La afya halina mjadala. Rekebisheni kwanza.

Jiulize Wafanyabiashara wa Wakichina waliotengeneza maziwa feki yakadhuru watoto walifanywaje?
 
Wafugaji wa ng’ombe wa maziwa katika kata ya Marangu, Mwika wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro wameandamana baada ya kiwanda cha kusindika maziwa,cha Kondiki Dairy Milk kufungwa na mamlaka ya chakula na dawa TFDA na TBS na hivyo kulazimika kumwaga maziwa baada ya kukosa soko.

Wananchi hao wamesema kwa muda wa wiki mbili sasa wamepata hasara ya zaidi ya shilingi milioni 40 kutokana na kukosa soko la maziwa hali ambayo inawalazimu kumwaga maziwa kila siku huku wakishindwa kuhudumia ng’ombe hao wa maziwa kupata chakula.

Wamesema tangu mwaka 2008 wamekuwa wakiuza maziwa katika kiwanda hicho na hivyo kuondokana na umaskini baada ya kupata soko la uhakika tofauti na hapo awali walipokuwa wanauza maziwa nchi jirani ya Kenya.

Mratibu wa maendeleo ya sekta ya maziwa nchini na Mshauri wa kiwanda cha maziwa Kondiki Dk Sadikiel Kimaro amesema wanasikitishwa na hatua ya kufungwa kwa kiwanda hicho na nkwamba mpaka sasa wamepata hasara kubwa kwa kuwa lengo lake ni kumsaidia mkulima mdogo kupata soko la uhakika la maziwa ili kujikwamua na umaskini.
Maelezo mengi sana, ila sijaona sababu za kufungwa kwa hicho kiwanda, au umerekebisha/ chuja taarifa? Je TBS na TFDA waliamka tu na kufunga kiwanda bila sababu yoyote?
 
Itawabidi upikie "kenaa" mpaka watakapo fungua hicho kiwanda
 
Back
Top Bottom