Ahsante kwa udundulizaji.
Unafahamu matumizi ya alama "Sawa sawa/The equals sign or equality sign (=) "?.
Yaani hapo umemaanisha mungu ni sawa sawa na Mungu. Humu tunakosea mno, nikiwa mmojapo. Si unajua msiba wa wengi?...
Usiandike mungu. Andika, aidha Mungu/MUNGU. Labda kama hum'maanishi Mungu muumba wa Mbingu na Nchi. Ukimwandia kwa kuanza na herufi ndogo, basi fasili hubadilika.
Kumradhi.
Nirudi kwa Miss Naomi.
Unapoomba Ajira--siyo kazi jitahidi kuwa makini sana. Nina uhakika, huu uandishi wa sampuli hii hukufundishwa katika madarasa ya awali. Andika kwa hati nadhifu, na usionyeshe uhitaji kupita kiasi.
Uhitaji kupita kiasi unaweza kutumiwa kama daraja kwa mwenye nia mbaya kutimiza hitaji lake ovu kwa kuutumia huu udhaifu. Si unalia sana?. Humu matapeli tumo, waso--na haya, mafisadi, wenye roho mbaya, inda, kedi, wapenda mteremko na mengine mengi.
Umeandika "kaz yakujitolea kwenye vituo yva watoto yatima", Je ulipo (Mwanza) hakuna vituo vya kulea watoto yatima ukajitolee?. Au hata kujitolea hawataki?.
God bless you dabo dabo.