Marafiki na Visa vyao[emoji23]

makota1809

Member
Jan 2, 2015
51
32
Habari wana jukwaa,Leo nimewaza Sana ni mara ngapi maisha yamenipa furaha nkahesabu lakini sikuweza kumaliza wala kukumbuka siku nlizofurahi maana ni nyingi Sana

Lakini nkajiuliza tena Mara ngapi mihangaiko ya maisha imenitenganisha na rafiki zangu wa dhati kabisa iwe kwa umbali wa macho yangu au kwa mwenye huu ulimwengu kuwachukua kabisa

Nikaona nifungue Uzi maalumu kwa Wana jf kukumbuka visa na Mikasa vya marafiki tuliokuwa nao ama kukumbuka maeneo mlokuwa mnasongesha life pamoja ,hatuwezi jua huenda tunaowakumbuka wapo humu ila sio kwa majina tuliofahamiana nao. Nawasilisha

Nakumbuka nilimshawishi bimkubwa amsaidie rafiki yangu ambae maskan kwao hali ilikuwa duni Sana ukilinganisha na familia yangu,akaanza kumpa miradi mbalimbali kumjua Zaid kwakuwa hakuwa na elimu,alianza na biashara ya mayai,baadae maji na alipomuamin akampa mradi mkubwa wa kuuza samaki wabichi aliokuwa anachukilia tanga...asee mwanzo alianza vizuri sana lakini Kuna siku tumekaa had saa tatu Elias hajarud nyumbani...tukaenda ofisi ya bimkubwa tukakuta mlango uko waz...tukasema atarudi kesho ....kesho ikapta ....simu ukipga haipatkani hatukuwaza Kama atakuwa kakimbia kwa maana jamaa alikuwa mstaaraabu Sana na tulikaa nae Zaid ya miaka 2 ...ilikuwa ngumu kuamini Ila jamaa alikuwa kampga bimkubwa 200000 mwaka 2012 kiukweli aliua biashara kabsa...niliumia sana
 
  • Thanks
Reactions: _ly
Mi rafiki mmoja aliniibia suruali yangu na simu geto huko magetoni Mabatini Mbeya 2012....nikaja kukutana nae Buzuruga Mwanza 2016 alivoniona akanichangamkia sana akanionyesha baa fulani ambapo alikuwa ndo meneja...akanisaidia vitu fulani fulani lakini sikuwa na imani nae tena...siku ya siku naenda pale baa kumuulizia naambiwa kawaibia milioni 4 kasepa. Mshikaji alikuwa ni mtu wa Morogoro..toka hapo marafiki nawaangaliaga kwanza kwa macho ya rohoni.
 
huu uzi mzuri san tena ungeweza kufika mbali lkn mleta uzi ndo umezingua, ilibidi ulte kisa chako ndio na wachangiaji wangefunguka sana...
 
Sijaelewa bado ngoja ninywe chai nitarudi kusoma tena
IMG_20200707_074940.jpg
 
Nilipoanza harakati marafiki walikuwa karibu nami,lakini kila nilivyozidi kupiga hatua nzuri katika shughuli zangu za kujitafutia kipato ndivyo walivyozidi kupungua.
Muda huu naandika sina rafiki hata mmoja,wote wamenitenga na wengine wamethubutu hata kwenda kwa sangoma ili kunizima kisha wananipigia simu na kuniuliza, "Bro vipi maendeleo ya mradi wako".... Daima jibu langu lilikuwa moja tuuu "Aisee mambo yako safi sanaa"...... Nia yake ajue jee alichoenda kukifanya kuharibu shughuli zangu kimefanikiwa ama la!!!
Nikiwa sipo ndo wanakuja kuangalia nimefikia hatua gani katika shughuli zangu,nikiwepo hakanyagi mtu.
Naishukuru serikali kwa kuweka sheria ngumu katika umiliki wa silaha na kuthibiti silaha kuzagaa hovyo mitaani maana ningeshajidakia yangu na kuwafagia hawa wajinga wote.
Marafiki ni moja kati ya kundi linaloweza kukukwamisha kuelekea mafanikio. Tupa kule haraka sanaa ukishaona viashiria tuu.
Jitahidi sanaa kuwa msiri wa mipango yako kimaisha.
 
Tangu nikiwa shule ya msingi, baada ya marafiki kunifanyia usinichi ikabidi nipige chini mpka leo. Sina rafki na sitegemei kuwa na rafki
 
Mi rafiki mmoja aliniibia suruali yangu na simu geto huko magetoni Mabatini Mbeya 2012....nikaja kukutana nae Buzuruga Mwanza 2016 alivoniona akanichangamkia sana akanionyesha baa fulani ambapo alikuwa ndo meneja...akanisaidia vitu fulani fulani lakini sikuwa na imani nae tena...siku ya siku naenda pale baa kumuulizia naambiwa kawaibia milioni 4 kasepa. Mshikaji alikuwa ni mtu wa Morogoro..toka hapo marafiki nawaangaliaga kwanza kwa macho ya rohoni.
Mshkaj ni muhuni .... Amezoea kupiga...shukuru Sana ungemzoea tena ungewasaidia polisi
 
Kuna rafiki yangu bhna nmelea sana alikuwa anashinda home asubuhi mpaka jioni kula mpaka siku nyingine kulala kavaa nguo zangu sana naona kapata kazi ya ualimu kaanza nyodo ata simu hapokei kaanza kunifundisha roho mbaya sana
Wana wanajisahau Sana,Nlikuwa nae mshikaj mwingne tena, baada ya wakwanza kumuibia bimkubwa familia ikasahau ikamsaidia mwingine kumsomesha taratibu akaanza kukamata vijisent hatimae akaanza kuwaongelea ovyo wazee wangu...kiukweli had leo najtahid kumsamehe....aliongea ovyo Sana licha ya msaada walompa,alipoona kapata vijisent vya tour guide akaona laif kalimudu....
 
huu uzi mzuri san tena ungeweza kufika mbali lkn mleta uzi ndo umezingua, ilibidi ulte kisa chako ndio na wachangiaji wangefunguka sana...
Nimeuapdate bro...ndo Uzi wa kwanza kupost ...ni mgeni katika kushusha Uzi....mapungufu ni mengi bado najfunza
 
Nilipoanza harakati marafiki walikuwa karibu nami,lakini kila nilivyozidi kupiga hatua nzuri katika shughuli zangu za kujitafutia kipato ndivyo walivyozidi kupungua.
Muda huu naandika sina rafiki hata mmoja,wote wamenitenga na wengine wamethubutu hata kwenda kwa sangoma ili kunizima kisha wananipigia simu na kuniuliza, "Bro vipi maendeleo ya mradi wako".... Daima jibu langu lilikuwa moja tuuu "Aisee mambo yako safi sanaa"...... Nia yake ajue jee alichoenda kukifanya kuharibu shughuli zangu kimefanikiwa ama la!!!
Nikiwa sipo ndo wanakuja kuangalia nimefikia hatua gani katika shughuli zangu,nikiwepo hakanyagi mtu.
Naishukuru serikali kwa kuweka sheria ngumu katika umiliki wa silaha na kuthibiti silaha kuzagaa hovyo mitaani maana ningeshajidakia yangu na kuwafagia hawa wajinga wote.
Marafiki ni moja kati ya kundi linaloweza kukukwamisha kuelekea mafanikio. Tupa kule haraka sanaa ukishaona viashiria tuu.
Jitahidi sanaa kuwa msiri wa mipango yako kimaisha.
Nmecheka Sana Kama mazuri vile, et n naishukuru serikali
 
Nasikitika sijawahi kutenda jambo lolote kwaajili ya marafiki zangu ila mimi napokea sana kutoka kwao. Marafiki zangu popote mlipo Mungu awabariki sana
 
Mimi Nina washkaji tu, Sina marafiki na wala sitakaa nijihesabu nina rafiki ingawa washkaji zangu nacheka nao na kuishi nao vizuri tu.
Na Kikubwa zaidi ambacho nimejifunza ni kwamba urafiki kati ya Me na Ke kwakweli naweza kuthubutu kusema HAUPOGO!!
 
Mi rafiki mmoja aliniibia suruali yangu na simu geto huko magetoni Mabatini Mbeya 2012....nikaja kukutana nae Buzuruga Mwanza 2016 alivoniona akanichangamkia sana akanionyesha baa fulani ambapo alikuwa ndo meneja...akanisaidia vitu fulani fulani lakini sikuwa na imani nae tena...siku ya siku naenda pale baa kumuulizia naambiwa kawaibia milioni 4 kasepa. Mshikaji alikuwa ni mtu wa Morogoro..toka hapo marafiki nawaangaliaga kwanza kwa macho ya rohoni.
Mabatini mbeya unanikumbusha long time sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom