Mara ya Pili... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mara ya Pili...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by major mkandala, Mar 22, 2010.

 1. m

  major mkandala Member

  #1
  Mar 22, 2010
  Joined: Mar 6, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mara ya Pili...  [​IMG] Fikiria wewe ni mwanamke ambaye baada ya kuishi na mwanaume kwa muda unaoujua wewe na kwa sababu unazozijua wewe mwanaume hayupo tena na wewe.
  Amekuacha na mtoto/watoto na baada ya kuponya majeraha ya kuondokewa au kubaki mwenyewe sasa unajiona upo katika hali ya kutafuta mwanaume anayefaa awe mume wako na ikiwezekana iwe ndoa yenye Baraka na inayokuridhisha.

  Inawezakana ulifanya makosa huko nyumba ndo maana sasa upo “single mom” au inawezekana hukufanya makosa bali imtokea tu na unejikuta ni “super single mom” na unataka ujipe second chance na kwamba hupenda ufanye makosa ili kumpata mume anayefaa tena na ikiwezekana awe baba mzuri kwa watoto ambao tayari unao.

  TAHADHARI
  Kumbuka hapa kuna mambo mawili wakati unaendelea na taratibu zako za kumsaka mume, kuna suala la kumpenda (fall in love) au kutimiziwa mahitaji uliyonayo (fall into needs)
  Hii ina maana gani?
  Inawezekana unahitaji baba mpya wa kutimiza mahitaji ya watoto wako au unahitaji mtu wa kukusaidia ili mambo ya fedha yawe sawa au unahitaji mtu wa kukupikia au unahitaji mtu wa kukufulia nguo au unahitaji mtu wa kukusaidia kulipa kodi ya nyumba au unahitaji mtu wa kukutimizia mahitaji yako ya mwili.
  Kujiingiza kuolewa ukidhani ni njia bora ya kutatua matatizo uliyonayo ni kujiingiza kwenye crisis ya hali ya juu.


  Kuolewa kunatakiwa kuwe na msingi wa upendo wa kweli wa kumpata mtu ambaye atakuwa mwenzi (companion) kwa upendo wa kweli ambao unavutia na kumkubali kama alivyo.
  “Deal with the problems first and then get married”
  Je, ni mambo gani ya msingi kuyafuata ili kumpata mume mwema tena.

  Nenda polepole:
  Ili kumpata mwanaume anayefaa basi nenda polepole katika process zote mara tano ya ile ulifanya mara ya kwanza kwa mwanaume uliishi naye.
  Usijirushe haraka haraka kwa mwanaume wakati hujui hata jina lake la ukoo.
  Pia usijiingize haraka na Kuamini yule alikuacha atakoma kuringa kwani ndoa ni yako si yake na itachekesha sana siku ukisikia hata huyo mwanaume iliyejiingiza haraka sasa unajuta.

  Nenda polepole na penda kidogokidogo, usikubali mapenzi kukufanya kuwa blind.

  Funga kufuli lako:
  Ulishakuwa sexually active hadi ukawa na watoto.
  Unaweza kujikuta unaingia kupasha moto mashuka ya kulalia na usijisikie kukosa adabu au kuona ni kitu cha kawaida.
  Akishakushika na kukupa kisses kwenye shavu unajiona mwili una “warm up” na unajisikia raha, usilemae utaweka rekodi mpya!
  Kama ulishajua utamua wa tunda ni ngumu sana kupiga brake usilivamie tena hata hivyo kuwa na msimamo ndiyo silaha.
  Mwambie wazi kabisa mchana kweupe kwamba
  “Nakupenda, sitafanya sex hadi niwe nimeolewa na kama inakupa shida naomba uwe wazi maana sitabadilisha msimamo wangu hii ni kwa mwanaume yeyote anayetaka kunioa”

  Iwe siri:
  Usiwaambie watoto wako mapema eti umepata baba mpya au ndugu zako kwamba nimempata handsome wangu wakati hata hujui tabia yake vizuri.
  Kama unaweza panga mipango yako nje ya nyumbani na huyo mtarajiwa wako na kama unaweza subiri hadi siku uone kweli una engagement ring kidoleni na matayarisho ya harusi yapo mlangoni.

  Kubaliana naye wapi mtaishi:
  Je, baada ya kuoana mtaishi kwenye nyumba yake au yako au mpya?
  Je, mtakuwa mnalala kitanda kile ulikuwa unalala la jamaa yako wa zamani?
  Je, mtakuwa mnalala chumba kilekile ulikuwa unalala na mzee?
  Je, kama na yeye ana watoto na wewe unawatoto na watoto wa mmoja wakawa wanawaambia watoto wageni “hii siyo nyumba yenu” utajisikiaje?

  Uwe mvumilivu:
  Kitu chochote kizuri hutumia muda zaidi na wakati mwingine husuasua hata hivyo uvumilivu hulipa.
  Inaweza kuwa ngumu kuliko unavyotegemea kwani kumpata mwanaume atayaekuwa responsible kwa watoto wa mwanaume mwingine si rahisi.
  Hivyo jiandae kulipa gharama na usitegemee mambo makubwa sana kwa ndoa yako mpya.
   
 2. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #2
  Mar 22, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  asante major mkandala,ushauri wako ni mzuri,tutauzingatia iwapo wachumba watatuacha!umeongea kweli tupu.endelea kutupa mambo mazuri kama haya.!
   
 3. m

  major mkandala Member

  #3
  Mar 22, 2010
  Joined: Mar 6, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimependa avator yako
  inaonekana mzoefu !!
   
 4. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,741
  Likes Received: 3,178
  Trophy Points: 280
  Source 'the hill of wealth' blog
   
 5. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  mzoefu wa nini kaka yangu???
   
 6. Noname

  Noname JF-Expert Member

  #6
  Mar 22, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,269
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Very useful information thanks for sharing...... the other day I was talking to a woman she told me " u know if I get divorced I will wait for three months only then will marry another man" I was like :eek: why is tht? she said because I cant stay without man... I was like mhhh how about ur kids? this kept me thinking ...
   
 7. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #7
  Mar 23, 2010
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Jamani ni vizuri kama mawazo ni yetu tuseme na kama si yetu tu-acknowledge......kutoa source si udhaifu ni ujasiri.....!itaonyesha kuwa unasoma pia kazi za watu wengine
   
Loading...