chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 20,404
- 24,990
Jeshi la Polisi kanda maalum ya Tarime mkoani Mara limefanikiwa kuwakamata watu kumi wakazi wa kijiji cha Kinesi wilayani Rorya kwa tuhuma za kumkamata na kutoa adhabu ya kumtandika viboko hadharani mwanamke mmoja mkazi wa kijiji hicho kwa madai ya kutoa lugha ya matusi dhidi ya mama ake mzazi.
Kamanda wa Polisi wa kanda maalum ya Tarime na Rorya, kamishina msaidi wa jeshi la polisi ACP Andrew Satta, amesema mwanamke huyo alitandikwa viboko hivyo hadharani na wajumbe wa baraza la mila la kabila la Wasimbiti jamii ya Wakurya kufuatia malalamiko yaliyofikkishwa katika baraza hilo na mama mzazi wa mwanamke huyo.
Kwa sababu hiyo kamanda huyo wa jeshi la polisi kanda maalum ya Tarime na Rorya, amesema tayari jeshi hilo limewakata watu kumi wakiwemo wazee na viongozi wa baraza la mila kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria.
Hata hivyo kamanda huyo wa polisi kanda maalum ya Tarime na Rorya, ameitaka jamii katika kanda hiyo kuacha mara moja vitendo vya kujichulia sheria mkononi huku viongozi wa vijiji wakitakiwa kuchukua hatua pindi matukio hayo yanaotokea katika maeneo yao.
Chanzo : ITV