Mara: Mwanafunzi agoma kwenda shule kisa hana akili

Ulichoandika kina mantiki. Maana haiwezekani mwanafunzi ajibu mtihani kwa kuandika majibu yasiyo sahihi makusudi halafu eti matokeo yatoke akiwa kafaulu. Labda matokeo ya wanafunzi wa shule, eneo au jinsia fulani upikwa ili kuridhisha mtu au kundi fulani la watu wapenda sifa au wanaotaka kukwepa dhana ya uwajibikaji.
 
Tatizo linalojitokeza kwa sasa ni kwamba watoto hulazimishwa kwenda kidato cha kwanza, awe kafaulu au la. Wapo wengine hata wao wanabaki wakishangaa. Hawajui kusoma wala kuandika. Wanajiuliza hivi ni nani kawafanyia huo mtihani. Sasa hicho Kiingereza cha kusomea huko Sekondari wanakipata wapi. Ninaye rafiki yangu ambaye ni mwalimu wa Sekondari. Anasema wanapata wakati mgumu sana kuwaelemisha wanafunzi wa aina hii. Lakini kwa vile ni lazima wasome, basi ni bora liende. Wafikapo kidato cha nne, matokeo yao yanaharibu kabisa wastani wa matokeo ya shule nzima.
 

What a waste of time and money


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Iliwahi kutokea hivo SHULE YA SEKONDARI MNAZI MMOJA, Dsm, miaka ya nyuma! Wanafunzi wale Walihojiwa BBC
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Majibu ya kuchagua na ku-shade vyumba.
Hesabu somo ambalo ndio kipimo cha uelewa nalo ni la kuchagua majibu, nani atafeli huo mtihani?
Ndio maana matokeo yanatoka wiki tatu tu tangu ufanyike mtihani, sio kama sisi tuli subiri hadi sikukuu ya mwaka mpya...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi nampongeza kwa maamuzi aloyachukua,hii Ni kwasababu kusoma Ni utashi na wengine husema kusoma Sana Ni woga wa maisha, ikumbukwe kuwa nchi yetu inaamini Kuna elimu rasmi na isiyo rasmi, hivyo huyo dogo yupo sawa afundishwe Ufundi nguo Kisha ataanza kudizaini nguo za mitindo Kisha atapata hela na muendesha maisha yake, Inshaallah atafikia malengo yake.
 
Kabisaa.. hili suala lisiishie hapa.
Hebu tupate matokeo pamoja na mitihani yake.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao anao ishi nao na kumtaka afanye yao ndiyo hawana akili, ya kushindwa kumuelewa yaani wazazi, waalimu, na mkuu wa wilaya ni wajinga.

Kwani kusomea, uana mitindo/ cherehani siyo shule?

hamuoni kuwa akili zenu zimefungwa na domain ujinga?
 
Mtoto ana akili sana kuliko kupoteza miaka minne ya kukaririshwa "what is chemisyry" halafu aje mtaan hakuna hata hy chemistry au akaambulie zero
Bora akajisomee ufundi baada ya miaka minne anakua na ujuzi wenye kumuingizia pesa .
Kongole kwa mwanafunzi kwa kutambua mapema hatma ya maisha yake
 
Kama nilivyoeleza hapo juu, hata walimu wanaofundisha sekondari wanawashangaa baadhi ya wanafunzi ambao hawajui alifu wala beta lakini wameshinda mitihani yao ya kumalizia shule za msingi. Lahaullah la kwata!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…