Queen V
JF-Expert Member
- Jan 19, 2012
- 775
- 1,332
Mkuu wa mkoa wa Mara Bw Magesa Mulongo, ameliagiza Baraza la Madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Butiama kumsimamisha kazi mara moja mhandisi wa maji wa Halmashauri hiyo Juma Makore kwa madai ya kusema uongo kuwa familia ya Baba wa Taifa wakiwemo wananchi wa kijiji cha Butiama wanapata huduma ya maji wakati akitambua taarifa hizo si za kweli.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara ambao umefanyika hadi saa moja na nusu usiku, wenye lengo la kujitambulisha pia kusikiliza kero zinazowakabili wananchi wa kijiji hicho, mkuu huyo wa mkoa wa Mara ameonesha kusikitishwa na mhandishi huyo wa idara ya maji kutoa taarifa ambazo zimepingwa na wananchi wote wakiongozwa na mkuu wa wilaya ya Butiama Bi Annarose Nyamubi.
Kwa sababu hiyo kiongozi huyo wa Serikali mkoani wa Mara, amesema inasikitishwa kwa watumishi wa umma kutoa taarifa zisizo na ukweli juu ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo hatua ambayo amesema imekuwa ikisababisha chuki kati ya Serikali na Wananchi hivyo kuagiza baraza hilo kumsimamisha kazi kisha ufanyike uchunguzi wakina kuhusu utekelezaji wa mradi huo.
Awali mkuu wa wilaya ya Butiama Bi.Annarose Nyamubi ameungana na wananchi wake katika kijiji hicho na kusema kijiji hicho kinakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa maji na hivyo kusababisha kero kwa wananchi, Mama Maria Nyerere, mkuu wa majeshi mstaafu David Msuguri yakiwemo kwa makazi ya mkuu wa wilaya.